Baikonur: Kituo cha pekee jangwani na msingi wa binadamu kufika anga ya juu

.

Chanzo cha picha, VEGITEL

Kituo cha anga za juu cha Baikonur, ambacho ni kituo cha kwanza na cha siri zaidi duniani, kiko katikati ya jangwa kubwa la Asia ya Kati, kilomita 2,600 kusini mashariki mwa Moscow na kilomita 1,300 kutoka kwa wauguzi na Almaty, miji miwili muhimu ya Kazakhstan.

Ilikuwa ni kutoka eneo hili la mbali la Magharibi ambapo Umoja wa Kisovyeti ulifanikiwa kuanzisha Sputnik 1, setilaiti ya kwanza ya bandia, katika anga mwaka 1957. Miaka minne baadaye, mwaka 1961, Yuri Gagarin alikuwa mtu wa kwanza kuingia angani kutoka kituo hiki na mnara wa Vostok.

Na mwaka 1963 Valentina Trushkova alikuwa mwanamke wa kwanza kuanza safari yake kutoka kituo cha Baikonur.

Baada ya NASA kufungua kituo cha anga za juu mwaka 2011, kituo hiki ndio kilikuwa cha pekee katika uzinduzi wa Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

Sasa, miaka 60 baada ya safari ya kihistoria ya Yuri Gagarin, kituo cha anga za juu cha Baikonur kinabaki kuwa kituo kikuu cha kutoa huduma za anga za juu.

Lakini ilikuwaje na kwa nini kituo hiki kizima kilichopo katika jangwa la Kazakhstan ya magharibi kiliendelea kuwa mahali ambapo binadamu anapata fursa ya kipekee?

Ili uweze kupata nafasi unahitaji vitu viwili: Kuwa mbali na maeneo yenye idadi kubwa ya watu na kama karibu na ikweta kadiri inawezekanavyo ili kuchukua fursa ya kasi ya mzunguko wa Dunia, ambayo ni ya kasi katika safu ya nje.

Kwa upande wa mpango wa anga za juu wa Marekani, pwani ya mashariki ya Florida ilikuwa na sifa zote mbili, na kwa hiyo kituo cha anga za juu cha Kennedy kilijengwa wakati huu.

Wakati huo huo, Umoja wa Kisovyeti ulikwenda Jamhuri ya Kisovyeti ya Kazakhstan kutafuta eneo la ndani ya mipaka ya Kazakhstan ambalo litakuwa na vifaa muhimu vya kufanyia majaribio ya makombora ya masafa marefu na kuanzisha roketi.

.

Chanzo cha picha, VEGITEL

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Umoja wa Kisovyeti ulikuwa ukifanya majaribio ya ujenzi na mwongozo wa roketi tangu miaka ya 1920 na ulipata teknolojia ya roketi ya Ujerumani ya V-2 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Mafanikio haya yamechangia kwa kiasi kikubwa katika uimarishaji wa mpango wa Kisovyeti.

Eneo la Tivartam, lenye idadi kubwa ya watu na liko katika sehemu za kusini mwa Kazakhstan, kando ya Mto Syrdarya, Soviets alichagua eneo kubwa lililofunikwa na uchafu na vifusi ambalo pia lilikuwa na abiria wa ndani ya nchi na reli ya mizigo.

Reli hii ilijengwa awali kwa matumizi ya wataalamu wa jiolojia na wale waliokuwa wanatafuta mafuta.

Sehemu iliyochaguliwa na Soviets ilikuwa ni nchi isiyo na milima, isiyo na miti, maji wala nyasi.

Dhoruba ya vumbi ilikuwa mara kwa mara na joto hufikia juu ya nyuzi 50 wakati wa joto na dhoruba za barafu hushusha baridi hadi nyuzi 30 chini ya sifuri wakati wa baridi.

Katika hali ya kushangaza, sehemu hii ya mbali na isiyokaliwa na watu, ambayo ni sehemu ya mwisho ya wanaanga hukaa kabla ya safari na sehemu ya kwanza wanayoiona wakirudi duniani, iligeuka kuwa chaguo sahihi.

Sovieti walikuwa na uwezo wa kutumia reli kuwaleta maelfu ya wafanyakazi kwenye tovuti kujenga na kukusanya vifaa na kujenga vituo vya anga ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shimo kubwa la bandia katika sayari, urefu wa mita 250, upana wa mita 100, na kina cha mita 45, ambayo iliundwa kwa namna ambayo inaweza kuwa na moto na moshi utokanao na roketi kubwa.

Mji wa Tiortam, uliopo kilomita 30 kusini mwa kituo cha uzinduzi, ulipata umuhimu taratibu. Na ili Wamarekani wasiweze kufuatilia shughuli hizi, wanasayansi wa Sovieti walibadilisha jina la mji wa Tiortam na jina la mji mwingine ambao ulikuwa umbali wa kilomita chache. Hivi ndivyo siri iliyofichika ya kituo cha anga za juu cha Baikonur ilivyokuwa.

.

Chanzo cha picha, VEGITEL

Mwanaanga wa Nasa Scott, katika makala yake inayoitwa "A Year in Space", ambayo ilihusu kuvunja rekodi yake kwenye stesheni ya Kimataifa ya Anga za mbali, anaelezea kituo cha Baikonur kama njia ya kuingia angani na anasema kwa kuja Baikonur alihisi kama amechukua hatua ya kwanza kutoka sehemu ya mbali hadi sehemu ya mbali zaidi.

Wakati mwanzoni mwa miaka ya 1960, juhudi za Marekani zisizo na mafanikio za kuwapeleka binadamu angani ziliitia aibu nchi hiyo, usiri wa Kisovieti ulisaidia kuifanya mipango yake kuwa ya mafanikio.

Janga lililotokea kwa Marekani wakati wa uzinduzi wa roketi iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni na vyombo vya habari na watu wa Marekani walilishuhudia.

Lakini usiri uliwapa wanasayansi wa Kisovyeti uhuru wa kuchukua hatari zaidi na kufanya kazi kwa kasi na kwa haraka zaidi.

Kufuatia kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti mnamo Desemba 1991, Kazakhstan ilipata uhuru wake, na ghafla kituo muhimu cha anga za juu cha Urusi kilikuwepo kwenye eneo la nchi ya kigeni.

Mwaka 1994, Warusi walitia saini makubaliano na Kazakhstan ili kukodisha kituo cha Baikonur. Kodi hiyo ilikuwa rubi bilioni 7, sawa na paundi milioni 82.5 kwa mwaka.

Idadi kubwa ya watalii kwa sasa wanatembelea Baikonur kutazama roketi zinazorushwa angani, hasa wakituma wanaanga kwenye stesheni ya kimataifa ya anga, lakini bado kuna hali ya usiri.

Mji huo ni zaidi eneo linalomilikiwa na Urusi ndani ya Kazakhstan, na setilaiti na eneo la kurusha makombora ni eneo lililozuiwa kuendeshwa na Shirika la Anga la Urusi.

Wageni lazima wasafiri kuelekea Baikonur katika ziara ya kuongozwa ambayo inahitaji ruhusa ya awali kwa ajili ya kuingia kupitia kampuni.

Hii ni sehemu ya kivutio cha kutembelea kwa ajili ya uzinduzi wa satelaiti na roketi kwenye anga ya mbali na inakupa fursa ya kuona sehemu ya kipekee kwamba huwezi kuwa na uwezo wa kutembelea mwenyewe, anasema Elena Matveeva, mkurugenzi wa Prezhov vijitel, ambayo ni moja ya waendeshaji wakuu wa ziara ya Baikonur.

Baikonur inajumuisha tovuti zote mbili za kurusha makombora - kipande cha kilometa 7,000 za ardhi upande wa kusini. Kwa njia nyingi, mji wa Baikonur ni tegemeo kamili la Umoja wa Kisovyeti wa miaka ya 1960.

Watalii wengi huja Baikonur kutazama kurushwa kwa roketi. Lakini Hanluca Pardelli, mwanzilishi na mkurugenzi wa "Tour za Kisovyeti", shirika lililobobea katika kuwapeleka watalii kwenye Umoja wa Kisovyeti wa zamani, anasema kwamba Baikonur pia inafurahisha kwa makala zake za kihistoria na kitamaduni. Mji uliojengwa karibu na setilaiti na kituo cha kurusha makombora, ni mfano kamili wa mpango wa Soviet wa kujenga mji katikati ya sehemu ya mbali na isiyojulikana - mji ambao Usovieti iliujenga katikati ya jangwa.

Kufika Baikonur ni safari ya kisiri, kwanza ni safari katika miji mikubwa ya Kazakhstan - Astana au Almaty - na kisha unachukua ndege ya ndani ya mji wa Qazlverda na uendelee na safari ya ardhini ya saa nne kuelekea Baikonur. Ukifika hapa, unachagua kati ya hoteli ya kimataifa ambazo hutumiwa na wanaanga za gharama ya chini bila mapambo za mtindo wa enzi ya Usovieti.