Rubani wa Afghanstan aliyewapatia Taliban helikopta ya kivita

"Baadhi ya watu huenda wasinifurahie. Maoni yanaweza kutofautiana lakini nawaambia nchi ni kama mama na hakuna mtu anayepaswa kuisaliti ," anasema Mohammad Edris Momand.

Momand ni miongoni mwa wanajeshi wachache waliochaguliwa na jeshi la Afghanstan ambao walipokea mafunzo nchini Marekani. Lakini wakati Taliban walipokaribia kuuteka mji mkuu Kabul, aliwageuka washirika wake na kuendesha ndege hadi kijijni kwake na kuikabidhi helikopta kwa maadui wake wa zamani.

"Lengo langu lilikuwa ni kulinda mali ya Afghanstan ,"aliiambia BBC. Mwaka mmoja baadaye, anaelezea uamuzi wake.

Mafunzo ya Marekani

Momand alijiunga na jeshi la Afghanistan mwaka 2009 na kuondoka kuelekea Marekani ambako alipitia mpango wa mafunzo kabambe ya kijeshi katika Shule ya mafunzi ya kijeshi ya Marekani American Military Academy - inayofahamika kama West Point.

Mwanzioni, alipelekwa kufanya kazi katika eneo la Herat lililopo Magharibi mwa Afghanistan, ambako aliendesha helikopta iliyotengenezwa nchini Urusi Mi-17 . Miaka michache baadaye alipumzika tena.

"Mwishoni mwa mwaka wa 2018, kikundi kidogo cha marubani vijana ambao walikuwa wamesomea teknolojia ya hivi karibuni ya ndege za kijeshi walichaguliwa kuendesha helikopta za aina ya Black Hawk. Tangu wakati huo nilikuwa naendesha Black Hawks."

Black Hawks zilikuwa zinatumiwa kwa shughuli ya usambazaji wa huduma kwa wanajeshi na usafiri.

Biden kutangaza kuondoa wanajeshi wa Marekani

Katika mwaka 2021, alikuwa katika Mazar-e-Sharif wakati Rais Biden alipotangaza nia ya kurejesha nyumbani wanajeshi wote wa Marekani kabla ya maadhinisho ya miaka ishirini ya mashambulio ya Septemba 11 dhidi ya Marekani.

Katika mwezi Julai tarehe ya kuondoka ilisongeshwa mbele hadi tarehe 31 Agosti.

Tumaini liligeuka kuwa ndoto ambazo hazikuweza kutimia. Jeshi la Afghanistan lilipoteza udhibiti wa nchi kwa Taliban kwa kasi ya ajabu.

Taliban walizingira maeneo ya vijijini mwezi wa Julai. Tarehe 6 Agosti, mji mkuu wa kwanza wa jimbo uliangukia mikononi mwao.

Baada ya kuteka majimbo mengi, Taliban iliuteka mji mkuu Kabul bila kupingwa tarehe 15 Agosti.

Kikundi hicho cha wanamgambo wa Kiislamu kiliyateka maeneo ya viungani mwa mji huo ya bonde la Janjshir yaliyokuwa yamesalia, hadi kaskazi ni mwa mji huo mkuu, tarehe 7 Septemba.

Wakati nchi ikiingia katika ghasia, miezi sita ya kuishi Mazar-e-Sharif iliisha mwezi Julai. Iliripoti katika ngome ya kikosi ya anga ya Kabul tarehe 14 Agosti.

Hali ilikuwa ya wasi wasi, huku kukiwa na uvumi kuhusu kutoroka kwa viongozi wa ngazi ya juu wa kisiasa na kijeshi.

Taliban walikuwa nje tu ya malango ya Kabul. Uwanja wa ndege ulikuwa chini ya udhibiti wa jeshi la Marekani, lakini ilikuwa haijulikani ni lini utakombolewa.

"Kamanda wa kikosi chetu aliwaamrisha marubani kuondoka nje ya mji. Alituagiza twenda Uzbekistan," Momand anakumbuka.

Momand alikasirishwa na amri. Aliamua kutoiheshimu. "Kamanda wangu alikuwa ananitaka niisaliti nchi yangu, ni kwanini niheshimu amri ya aina hiyo? Kusaliti nchi yako ulikuwa ni uhalifu mbaya zaidi. Ndio maana sikutii amri hiyo ," Momand anaeleza.

Aliomba ushauri kutoka kwa familia. Ushauri wa baba yake ulikuwa wenye nguvu zaidi.

"Alionionya kwamba hatawahi kunisamehe iwapo nitaondoka nchini ."Baba yake alieleza : "Helikopta ni mali ya Afghanistan. Haipaswi kuondoka nchini,'" Kuwakwepa wahudumu wake.

Kuwakwepa wahudumu wake

Jimbo la Momand la tayari lilikuwa limeangukia mikononi mwa Taliban. Baba yake alizungumza na gavana wa jimbo lao, ambaye alimhakikishia kwamba hakuna madhara yoyote yatakayotokea kwa helikopta iwapo ingesafirishwa hadi pale.

Momand alipanga kutoroka. Lakini kwanza ilibidi akabiliane na kikwanzo kikuu katika njia ya safari.

"Kila Black Hawk ilikuwa na wahudumu wanne. Nilifahamu kuwa nisingeweza kuwaamini na mpango wangu."

"Nilikuwa na uhakika kwamba wasingekubali. Wangehatarisha maisha yangu na hata uharibufu wa helikopta ." Ulipanga mpango wa kuwalaghai.

"Nilimwambia kamanda wa kikosi cha anga kwamba helikopta ilikuwa na matatizo ya kiufundi na kwamba nisingeweza kuiendesha.

Wakati waliposikia hili, wahudumu wote watatu wakaruka kutoka ndani yake na kuingia katika helikopta nyingine ambayo ilikuwa inaandaliwa kuondoka kuelekea Uzbekistan."

Kutorokea Kunar

Baada ya helikopta zote kuondoka, aliwasha injini kwa dakika 30 na kuelekea Kunar.

"Wamarekani walikuwa wanadhibiti anga la safari za ndege . Kwahiyo niliwaambia kwa redio kwamba nilikuwa ninaondoka kuelekea Uzbekistan. Baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege nilizima rada yangu na nikaenda moja kwa moja hadi Kunar."

"Nilitua na helikopta yangu kijini kwetu karibu na nyumba yangu. Baada ya kupata hakikisho kutoka kwa Taliban, nilichukua helikopta mahali ambapo niliwahi kuijaza mafuta zamani."

Anasema familia yake, marafiki na majirani waliuunga mkono uamuzi wake. Momand anasema hajutii matendo yake. Anasema alikuwa na chaguo la kuondoka Afghanistan na mke na watoto wake, lakini aliamua kubaki.

"Washauri wa Marekani walinitumia jumbe mara tatu. Walisema, hata kama huwezi kurejesha helikopta, njoo kwa barabara na watu wa familia yako ili muokolewe. Lakini sikukubali ofa yao."

Uimara wa kikosi cha anga cha Afghanistan

Mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2021, Kikosi cha Afghanistan kilikuwa kina ndege 167, zikiwemo helikopta za mashmabulizi na ndege, kulingana na ripoti iliyotolewa na Inspekta Jenenali wa kwa ajili ya ukarabati wa Afghanistan mwenye makao yake Marekani (Sigar).

Hujuma

Vikosi vya Marekani walifanya wawezavyo kuhujumu nyingi kati ya helikopta na ndege zilizoachwa mjini Kabul.

Haijawa wazi ni ngapi bado zinagafanya kazi katika Afghanistan leo. "Kwa sasa tuna helikopta saba za aina ya Black Hawk ambazo zinatumika. Wahandisi wa Afghanistan Black Hawk kuweza kutumika," Momand anasema.

Anawalaumu wenzake, akisema kuwa walisababisha hasara kubwa kwa Afghanistan kwa kufuata amri ya kuondoka nchini bila kufikiria.

"Wale walisafiri na helikopta na kwenda hadi Uzbekistan waliiangusha nchi. Helikopta ni mali ya nchi yetu. Zilikuwa helikopta ghali. Sidhani tutawahi kamwe kuzirejesha ."

'Nitaendelea kuhudumu'

Aliambia wakati wa mafunzo yake nchini Marekani kwamba inagaribu dola milioni sita mumfunza rubani wa helikopta Momand anathamani fursa hiyo na bado anakumbuka siku alipoweza kwenda nchini Marekani kwa mara ya kwanza. "Nilikuwa mwenye furaha sana na shauku .Sikuamini kwamba siku ile ingekuja maishani mwangu ."

Katika kipindi cha miaka minne ya mafunzo hakuwahi kuitembelea familia yake nchini Afghanistan ana alibakia nchini Marekani.

Momand alipewa mafunzo ya kukabiliana na Taliban, lakini sasa anatumia helikopta ya Black Hawk kwa ajili ya serikali inayodhibitiwa na Taliban. Haoni utata juu ya hilo.

"Serikali kila mara huwa zinabadilika. Watu kama sisi ni wa taifa na tunahudumia taifa. Jeshi halipaswi kujihusisha katika siasa. Nchi iliwekeza pesa nyingi katika watu kama sisi."

Hata kama Taliban wamekuwa wakitawala nchi kwa mwaka mmoja, hakuna nchi iliyokwishawatambua rasmi kama watawala halali. Licha ya hili, Momand amesalia kuwa imara.

"Nitaendelea kufanya kazi yangu kuhudumia nchi yangu hadi siku ya mwisho ya maisha yangu ."