Kwanini kombora hili la masafa marefu linalosifiwa na rais Putin lilikataa kuruka?

Chanzo cha picha, Planet Labs
Kuna uwezekano kulikuwa na ajali mbaya katika kituo cha anga za juu cha jeshi la Urusi, Plesetsk mnamo Septemba 20.
Watafiti na wataalamu wa OSINT wanaamini kwamba kuna uwezekano mkubwa lilikuwa jaribio lisilofaulu la kombora la masafa marefu la RS-28 Sarmat, ambalo inaonekana lililipuka kwenye silo. Kulingana na taarifa zilizopo, BBC imejaribu kuunda upya matukio hayo.
Picha za setlaiti zimeonesha shimo kubwa lililosababishwa na mlipuko katika upande mmoja wa mtambo wa kufyatua kombora hilo. Idhaa ya BBC nchini Urusi ilichunguza picha hizo za setaliti zilizochukuliwa mwezi Julai na Septemba 23 za eneo hilo. Zinaonyesha kuwa sehemu moja ya mtambo wa kufyatua kombora hili iliharibika vibaya
Kwa kuongeza, huduma ya NASA FIRMS , ambayo inafahamisha mara moja kuhusu moto mkubwa duniani kote, iliripoti kuwa mnamo Septemba 20, moto mkali ulionekana kwenye eneo hili.
Hadi sasa, ni jaribio moja tu la kombora la RS-28 Sarmat ambalo limeripotiwa rasmi, na lilionekana kuwa limefaulu.
Wataalamu kadhaa wanaofuatilia shughuli za kimkakati za nyuklia za Urusi wameripoti kuwa eneo hilo lilitumiwa hapo awali kujaribu kombora la Sarmat.
Miongoni mwao ni mkuu wa mradi " Silaha za Nyuklia za Urusi " Pavel Podvig na Maxim Starchak kutoka Kituo cha Sera ya Kimataifa na Ulinzi katika Chuo Kikuu cha Queen.

Chanzo cha picha, PLANET LABS
"Mtambo ambao ulitumika kwa jaribio hili ulibadilishwa kisasa kwa kurusha kombora la Sarmat," Pavel Podvig alisema. Kwa hivyo, hana shaka kwamba lilikuwa kombora hili haswa.
Ukweli kwamba Urusi ilikuwa ikipanga kurusha kombora la Sarmat katika siku hizo pia ilibainishwa na mtafiti kutoka Ufaransa Etienne Marcuse, ambaye alichapisha chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X mnamo Septemba 17, ambapo alielezea kutolewa kwa tahadhari ya kwa marubani.
NOTAM (notisi kwa maafisa wa anga) ni mfumo wa arifa za maandishi kuhusu mabadiliko katika hali ya anga na urambazaji, ambayo husambazwa na mashirika mbalimbali yanayohusika na trafiki ya anga.

Chanzo cha picha, Reuters
"Mlipuko ulitokea moja kwa moja kwenye mgodi. Mbali na hayo, ni vigumu kusema chochote. Ajali kama hizo zimetokea hapo awali. Na ziliunganishwa na ukweli kwamba roketi haikuweza kuruka, kwa kusema, "alisema Pavel Podvig.
Hii inaonyeshwa na uharibifu wa mgodi, ambao, kwa kuzingatia picha za satelaiti, uliharibiwa.
Mlipuko kama huo unaweza kutokea kinadharia tu kwa sababu ya mafuta. "Sarmat" ni roketi iliyo na injini za kioevu (pia kuna zile mafuta magumu). Kawaida, mafuta huwa na vipengele viwili vinavyochanganya wakati wa ufanyaji kazi wa injini, mafuta yenyewe na oxidizer.
Muundo wa mafuta ya Sarmat haujawekwa wazi rasmi. Hata hivyo, mafuta, na hasa oxidizer katika roketi za kioevu, mara nyingi ni kemikali yenye sumu na inayowaka.
"Ulinzi wa kombora sio kizuizi"
"Sarmat" ikawa moja ya aina hizo za silaha ambazo Vladimir Putin alizizungumzia katika hotuba yake maarufu mnamo Machi 1, 2018. Kisha, katika hotuba yake ya 14 kwa Bunge la Shirikisho, bila kutarajia alitumia karibu nusu ya hotuba yake kuzungumza juu ya aina mpya ya silaha.
Mmoja wapo ilikuwa kombora la Sarmat. Putin alisema kuwa Wizara ya Ulinzi, pamoja na makampuni ya biashara ya roketi na sekta ya anga, walikuwa wameanza awamu ya kazi ya majaribio ya Sarmat.
Wakati wa majaribio kama haya, roketi ya mfano inarushwa kutoka kwa silo. Roketi halisi, baada ya risasi kama hiyo, kwenye mwinuko fulani angani, huwasha injini zao na kuanza kuruka kuelekea kwenye eneo lengwa. Wakati wa majaribio ya kushuka, roketi ya mfano inaweza pia kuwasha injini zake, lakini ndege yake haidumu kwa muda mrefu,huanguka chini kwenye parachuti.

Chanzo cha picha, Kremlin.ru
Akizungumzia sifa za kombora hilo, Putin alirejelea video, sio ripoti ya majaribio ya isipokuwa kwa picha za kompyuta ambazo makombora mawili yaliruka kuzunguka ulimwengu kutoka pande mbili.
"Kama inavyoonekana kwenye picha za video, ina uwezo wa kushambulia shabaha kupitia Ncha ya Kaskazini na Kusini. Sarmat ni silaha ya kutisha sana; kutokana na sifa zake, hakuna mifumo ya ulinzi wa makombora, hata ya juu zaidi, inaweza kuwa. kikwazo kwake," Putin alisema.
Hatahivyo, wakati huo hakukuwa na jaribio urushaji wa kombora la Sarmat.
Jaribio moja
Mnamo Aprili 20, 2022, jaribio la kwanza na la pekee la mafanikio la kombora la Sarmat lilifanyika. Hiki ni kisa cha kipekee katika historia ya ukuzaji na utengenezaji wa makombora ya balestiki ya mabara.
"Mnamo Aprili 20, 2022, urushaji uliofaulu wa kombora la masafa marefu la Sarmat lilifanyika kutoka kwa Jaribio la 1 la Jimbo la Cosmodrome Plesetsk, la kwanza katika mpango wa majaribio ya ndege ya serikali. Kazi za urushaji zilikamilishwa kikamilifu.

Chanzo cha picha, Reuters
Degtyar aliliita Sarmat, kombora ambalo limekuwa na jaribio moja tu la mafanikio, "sababu kuu ya kuzuia nyuklia" na "hakikisho la kudumisha amani."
Hata hivyo, "ripoti kwamba iko kwenye jukumu la kupigana inapaswa kutumika kwa tahadhari," anasema Pavel Podvig.
Kulingana na mtaalamu huyo, pamoja na uzinduzi wa kwanza uliofanikiwa, kulikuwa na mwingine ambao haukufanikiwa mnamo 2023, ambao uongozi wa Urusi ulificha.
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga












