Mataifa 5 ambayo yatakusaidia kujua chimbuko la ukoo wako

.

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Lindsey Galloway
    • Nafasi, BBC News
  • Muda wa kusoma: Dakika 7

Kadri zilivyo kuwa rahisi na nafuu, vifaa vya kupima msimbojeni kama vile Ancestry na 23&Me vimeleta umaarufu mkubwa kwa “utalii wa turathi,” ambao ni safari za kutafuta na kuunganishwa na maeneo ya asili ya familia.

Kwa kutumia vipimo vinavyotoa makadirio ya asilimia kuhusu asili ya DNA yako, watu ambao hawana ufahamu kuhusu ukoo wao sasa wanaweza kuchunguza chimbuko la familia zao na kujua walikotokea.

Zaidi ya hayo, ongezeko la utalii wa kutafuta ukoo linachukuliwa kama mbadala endelevu wa utalii wa kupita kiasi (overtourism). Umoja wa Ulaya, ambao unaongoza kwa viwango vya juu vya utalii (na kwa hivyo utalii wa kupita kiasi), umehimiza nchi wanachama wake kukuza utalii wa kujua ukoo. Huu mara nyingi huwahamasisha wageni kutembelea vijiji vidogo na maeneo ambayo hayatembelewi sana na watalii, na hivyo kusaidia kukuza maendeleo ya kiuchumi ya mikoa hiyo.

Mawakala wa kusafiri wanaofanya ziara za utalii wa kutafuta ukoo pia wameongezeka mara dufu.

Pia unaweza kusoma:

Kwa mfano mwaka 2021 ,kampuni za kusafiri ya Kensington ilishirikiana na shirika la Ancestry.com kuanzisha ziara za kujua nasaba katika maeneo kama vile italia,Ujerumani,Japan na Ghana na kuambatana na mtaalam wa masuala ya ukoo ambaye angefafanua kiundani zaidi historia za maeneo hayo ambayo yanajivunia kumbukumbu za jadi na kusaidia kutambua chimbuko la watu ,"ziara hizi zilianza kupata umaarufu 2022 baada ya janga la korona kuisha na vibali vya kusafiri vikaanza kutumika kote ulimwenguni," alisema Debra Loew ambaye anafanya kazi Kensington Tours. "huu ndio wakati tuloshuhudia mseto wa familia ulivyoanza kutembeleana ili kubaini chimbuko lake baada ya kutoonana kwa miaka au hata miezi kadhaa."

Huku mataifa ya ulaya yakiendelea kuimarisha ziara za kujua na kutafuta ukoo,nchi zingine zina njia za kipekee za kuwasaidia raia wake kujua chimbuko lao.

Haya hapa ni maeneo yanayosaidia watalii kugundua chimbuko lao.

Italia ina matumaini watu walio na asili yao watarejea kujua utamaduni na mila zao

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Italia ina matumaini watu walio na asili yao watarejea kujua utamaduni na mila zao

Italia

Takriban watu milioni 80 kote ulimwenguni wanaweza kutafuta na kupata nasaba yao Italia,waziri wa utalii nchini humo amewasihi wanaoishi nje ya nchi warejee nyumbani akitaja ni mwaka wa kutambua nasaba za kitaliano ulimwenguni.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tayari wamezindua tovuti ya italia ili kurahisishia mambo watalii kupata ujumbe kuhusu maeneo 20 ,na maelezo ya jinsi ya kutambua hadithi za ukoo.

Maafisa wa ziara wameanza kufurahia faida ya mikakati iliyowekwa kuhusu usafiri.

”safari za ukoo zimekuwa nguzo muhimu kwa biashara yangu,na Kuwa mahususi kwa asilimia 95 ,”anasema Marino Cardelli ambaye ni mwanzilishi wa kampuni ya usafiri ya Experience BellaVita tangu mwaka 2018.

"kazi hii imekuwa Zaidi ya biashara -ni jambo la kuchangamkia kuhakikisha watalii wanaunganishwa na vizazi vyao haswa ukoo wa kitaliano.Watalii wengi wanaozuru mji huu wana maeneo mahususi hupendekeza wapelekwe kuzuru na tunajitolea kupitia huduma zetu za kutambua msimbojeni ili kuwasaidia kikamilifu.

Pia amedokeza kuwa kuunganisha ukoo sio shughuli rahisi ina changamoto zake.

Waitaliano wengi walihama na huenda makazi yao yaliharibiwa katika Vita vya dunia.

Hata hivyo Italia inarekodi za kisheria na parokia ambazo zinaweza kufuatiliwa hadi miaka ya 1400s ambazo zinatumika kusambaza na kueleza historia ambayo mara nyingi husaidia kuunganisha watalii wengi.

Kasri ya Elmina na maeneo yaliyokuwa soko la watumwa ni maeneo muhimu ya kujua mila ya Bara la Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kasri ya Elmina na maeneo yaliyokuwa soko la watumwa ni maeneo muhimu ya kujua mila ya Bara la Afrika

Ghana

Nchi hii ya Afrika Magharibi, iliyowahi kuwa kitovu cha biashara ya utumwa katika Bahari ya Atlantiki, kwa muda mrefu imekuwa ikiwakaribisha watu wanaoishi nje ya Afrika kurudi kwenye chimbuko lao, ikiwa ni pamoja na Mwaka wakuruhusu waafrika walio nchi za ughaibuni Kujumuika pamoja ili kudumisha undugu almaarufu the year of return na mradi wa kuunganisha waathiriwa wa ulaghai wa binadamu na huduma za kisheria almaarufu The Joseph Project mwaka 2007. Kuongezeka kwa upimaji wa DNA imekuwa kichocheo mahususi cha ukuaji wa vizazi vya Kiafrika vinavyotafuta kuelewa zaidi maeneo au makabila mahususi ambayo familia zao zimetoka.

Kwa sababu ya historia yake kama bandari muhimu wakati wa biashara ya watumwa, Ghana mara nyingi inaashiria kituo muhimu katika safari ya kutafuta ukoo Afrika. Kati ya Karne ya 16 na 18, makumi ya maelfu ya watu waliokuwa watumwa kwa mwaka walipitia maeneo kama Elmina Castle, seli za mwisho za bara kabla ya kutumwa kwa meli kwenda Amerika Kaskazini na Kusini.

Kwa sasa, ziara za kutafuta ukoo kama vile"Door Of No Return Ancestral Journey" hutoa nafasi kwa watalii kutembelea maeneo ya jadi na kuelezwa historia yao pamoja mila na tamaduni zao.

Scotland imeshuhudia ongezeko la ziara za kitalii zakutafuta ukoo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Scotland imeshuhudia ongezeko la ziara za kitalii zakutafuta ukoo

Scotland

Zaidi ya watu milioni 40 wanaoishi ulimwenguni wanaweza kusema chimbuko lao ni Scotland na wengi hutembelea taifa hili kupata ufafanuzi na historia ya kizazi chao.

Naa wengi wanaofika taifa hili husema wanajihisi kuwa wako nyumbani ama ni wakaazi wa Scotland japokuwa ni wageni.

Kwa wale wanaojua majina ya wazee wao wa jadi mtandao unaomilikiwa na serikali ya Scotland huwapa rekodi kuhusu taarifa yao jina na mwaka walioishi eneo hili.

Na wanaojipata kujua jina moja ya familia wana utafiti unaofahamika kama scots clan ambao una taarifa zote kuhusu ukoo wao walichokiamini na wale wa karibu nao na maeneo walikoishi.

Wakijivunia kua na ufahamu wa maeneo 30 ya kuzuru na miaka nakuwa nahistoria ya miaka 5000 iliyopita ,shirika la The Explorer Pass ambalo hutumiwa sana na mazingira ya jadi ya Scotland ina uwezo wa kutambua ukoo wako na chimbuko lako haswa kwa maeneo kama vile Campbell Castle au eneo la zamani la Jarlshof prehistoric and norse settlement.

India inajivunia kuwa eneo la kitalii la kutafuta ukoo linalopiga jeki utalii

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, India inajivunia kuwa eneo la kitalii la kutafuta ukoo linalopiga jeki utalii

India

Zaidi ya watu milaioni 18 waliozaliwa India wanaishi mataifa ya ughaibuni ,na kuipa hadhi ya watlii kuzuru maeneo ya kihistoria kujua mila na utamaduni wao.Hivi majuzi serikali ilizindua mpya inayotumiwa na raia wakihindi pekee inayofahamika kama Pravasi Bharatiya Express .

Masharti ya kuabiri treni hiyo ni kama vile uwe na umri wa miaka 45 hadi 65 ,inatarajiwa kuondoka na kuanza safari yake mwaka ujao januari tarehe 9 ,tarhe iliyotengwa kumkumbuka kurejea kwa Mahatma ghadhi alipotoka Afrika Kusini mwaka 1915.

Pia unaweza kusoma:

Ingawa treni hiyo ina viti 156 za abiria ,ziara hiyo ya wiki tatu itawapa watalii nafasi ya kuzuru maeneo mbalimbali na maeneo ya kidini kote nchini ,kama vile Ayodhya, Patna, Gaya, Varanasi, Mahabalipuram, Rameshwaram, Madurai, Kochi, Goa, Ekta Nagar (Kevadia), Ajmer, Pushkar and Agra.

Iwapo ungependa kujumusihwa kwa ziara hiyo utawasilisha ombi lako kwa serikali ambao watagharimikia kila kitu.

Kulingana na Trevolution Group kumenakiliwa ongezeko la watalii nchini kwa asilimia 46 .Idadi hiyo imezidishwa na raia wa Marekani alio na asili ya kihindi wanaorejea India kujua utamaduni wao.

Macon na Georgia ilikuwa ni miongoni mwa vijiji 60 vilivyounda taifa la Muscogee (Creek)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Macon na Georgia ilikuwa ni miongoni mwa vijiji 60 vilivyounda taifa la Muscogee (Creek)

Marekani

Ingawa Marekani na Canada zilishuhudia uhamiaji mkubwa kutoka Ulaya wakati wa utawala wao chini ya Uingereza, gharama za uhamiaji huo kwa watu wa asili imekuwa mara nyingi ikipuuziliwa mbali.

Watu wa asili walilazimishwa mara nyingi kuhamishwa mbali na maeneo yao ya asili, na hawakuwa na chaguo lingine isipokuwa kuishi mahali pengine.

Leo, baadhi ya mashirika ya utalii yamefanya juhudi kubwa za kuwakaribisha warithi wa watu wa asili kurudi, kwa kushirikiana na viongozi wa asili wa maeneo hayo ili kuhifadhi na kushiriki historia muhimu na warithi waliotawanyika na wageni wengine wa kanda hiyo.

Mfano mmoja ni eneo linaloitwa sasa Macon, Georgia, ambalo awali lilikuwa vijiji 60 vilivyounda Taifa la Muscogee (Creek). Hata hivyo, Sheria ya Uhamishaji wa Wahindi ya 1830 ililazimisha Taifa la Muscogee kuhamia Oklahoma.

Hata hivyo, umuhimu wa eneo la kihistoria la awali haujapotea, na ofisi ya utalii ya Visit Macon imekuwa ikishirikiana na Taifa la Muscogee ili kuhifadhi maeneo ya kihistoria kama mbuga la kitaifa la historia Ocmulgee Mounds, ambayo ni nyumbani kwa historia ya miaka 17,000 ya watu wa asili.

Wadau wote wamekuwa wakisisitiza kuwa eneo hili liweze kuteuliwa kuwa hifadhi ya kitaifa, na ikiwa itakubaliwa, itakuwa mojawapo ya mbuga za kwanza nchini ambazo zitakuwa zinashirikiana katika usimamizi na kabila la asili.

Wananchi kutoka Taifa la Muscogee wamekuwa wakirejea kwenye ardhi yao si tu kama wageni, bali kama washiriki i katika kujenga mipango na sherehe za mji wa Macon.

Huduma za kitaifa za wanyamapori inawaajiri mara kwa mara wananchi wa Muscogee (Creek), na kipaumbele kinatolewa kwa wanachama wa Taifa la Muscogee kwa nafasi zinazopatikana za ajira.

Mwezi Septemba mwaka huu , alama za kwanza za barabara zilizoshirikisha majina ya Kiingereza na Creek zilifunguliwa, na alama 100 zaidi za barabara zitafungwa katika wilaya ya katikati ya mji katika miezi ijayo.

Soma zaidi:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid na kuhaririwa na Yusuf Jumah