Uturuki na Syria zakumbwa tena na tetemeko la ardhi la ukubwa wa 6.4

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.4 katika kipimo cha Richter limepiga eneo la mpaka wa Uturuki na Syria jioni ya Jumatatu, na kusababisha hofu na uharibifu wa majengo katika mji wa Antakya nchini Uturuki wiki mbili baada ya tetemeko baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kupoteza maisha.

Mashahidi wawili waliambia shirika la habari la Reuters, tetemeko kubwa la ardhi na uharibifu zaidi kwa majengo katikati mwa Antakya, ambapo lilikuwa kitovu cha tetemeko.

Ilisikika pia huko Misri na Lebanon, waandishi wa habari wa Reuters wameongeza.

Kituo cha Ulaya cha Seismoloji (EMSC) kilisema tetemeko hilo lilipiga kwa kina kidogo cha kilomita 2 (maili 1.2).

Polisi walishika doria Antakya huku magari ya kubebea wagonjwa yakikimbilia eneo lililokumbwa na tetemeko karibu na katikati mwa jiji.

Watu wawili walizirai, huku wengine wakijaza mitaa kuzunguka mbuga hiyo ya kati wakipiga simu za dharura.

Walioshuhudia wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa kumekuwa na uharibifu zaidi wa majengo huko Antakya.

Kiwango cha 7.8 kilipiga eneo hilo mnamo 6 Februari, na kuua zaidi ya watu 44,000 nchini Uturuki na Syria.

Mamlaka ya Uturuki imerekodi zaidi ya mitetemeko 6,000 baada ya tetemeko hilo kutokea, lakini timu ya BBC katika eneo hilo ilisema tetemeko hilo la leo lilikuwa na nguvu zaidi kuliko za awali.

Mashahidi walisema kutikisika zaidi kulionekana pia katika maeneo ya Syria, Misri na Lebanon.

Kwa sasa haijulikani imesababisha uharibifu kiasi gani au ikiwa kuna majeruhi wowote.

Antakya, mji mkuu wa Mkoa wa Hatay nchini Uturuki, ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi tarehe 6 Februari.

Mwandishi wa habari wa AFP aliripoti juu ya matukio ya hofu huko Antakya - ambayo tayari ilikuwa imeharibiwa na tetemeko la ardhi lililopita - huku mitetemeko ya hivi punde ikiibua mawingu ya vumbi katika jiji hilo.

Kuta za majengo yaliyoharibiwa vibaya pia zilibomoka, AFP inaripoti, huku watu kadhaa waliojeruhiwa wakiomba msaada.

Ali Mazlum alisema alikuwa akitafuta miili ya wanafamilia kutoka kwa tetemeko la ardhi lililopita wakati lile la hivi punde lilipotokea.

"Hujui cha kufanya... tukashikana na mbele yetu, kuta zilianza kuanguka. Ilionekana kama ardhi inafunguka ili kutumeza," alisema.

Antakya, mji mkuu wa Mkoa wa Hatay nchini Uturuki, ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi tarehe 6 Februari.

Nchini Syria, kundi la msaada la White Helmets lilisema watu kadhaa walijeruhiwa na majengo yaliyoanguka.