Qutbuddin Aybak: Mtumwa Muislamu aliyeongoza dola la India

Qutbuddin Aybak alikuwa sultan wa kwanza wa Delhi, na baadaye akachukua uongozi wa Ufalme wa Ghulam huko Pakistan, Afghanistan na India.
Yeye ndiye mwanzilishi wa jengo maarufu la Qutub, lililoko katika mji mkuu wa Delhi, lililowekwa alama na maeneo ya kihistoria.
Mtumwa huyo wa zamani ndiye aliyeongoza utawala wa Kiislamu nchini India kwa takriban miaka 600.
Qutbuddin alikuwa ni nani?
Alizaliwa katika Asia ya Kati na asili yake kutoka Uturuki.
Akiwa na umri mdogo aliuzwa utumwani na kuchukuliwa na mkuu wa mji wa Nishapur katika mkoa wa Khorasan, Iran.
Mnunuzi huyo aliwatendea kama watoto wake mwenyewe, na alikuwa akiongea Kiarabu na Kiajemi kwa ufasaha, kupanda farasi na kurusha mishale.
Wakati tajiri wake alipofariki, watoto wake waliokuwa wamechukizwa na jinsi Qutbuddin alivyopokelewa, walimuuza tena kama mtumwa. Alibahatika kuangukia mikononi mwa Sultan Mohamed Ghori, ambaye wakati huo alitawala kaskazini magharibi mwa Afghanistan.
Baada ya muda, Qutbuddin alimsaidia Sultani kupata eneo zaidi, hasa kaskazini mwa India.

Chanzo cha picha, UNIVERSAL HISTORY ARCHIVE
Utawala wa Qutbuddin
Baada ya kifo cha Sultan Mohamed Ghori mwaka 1206, Qutbuddin alichukua madaraka baada ya mapambano mafupi.
Hakuna aliyechaguliwa na Ghori kurithi kiti cha enzi. Alijenga ufalme mkubwa ambao kwa mara ya kwanza ulitekeleza ukusanyaji wa kodi, uhuru na utawala wa sheria katika eneo hilo.
Anasifiwa kwa kuwaleta Wahindi na Waislamu karibu na nchi wakati wake na kuajiri Wahindi wenye ujuzi katika majengo yake.
Kifo cha Qutbuddin
Wanahistoria wanaandika kwamba Qutbuddin alikufa ghafla alipokuwa akishiriki mechi ya polo, baada ya kugongwa na farasi wake.
Amezikwa Lahor, Pakistani, ambako hutembelewa kila mwaka. Qutbuddin alielezewa kuwa shujaa aliyefanikisha mambo muhimu, na pia alijulikana kwa ukarimu wake, aliyepewa jina la utani la mtu ambaye alitoa mamia ya maelfu.
Wanahistoria wa Kiislamu wanamuelezea kama mwabudu mzuri, na wakati wa utawala wake aliifanya India kuwa kitovu cha Uislamu huko Asia.












