Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Newcastle wajiandaa kwa ofa mpya ya Isak

Muda wa kusoma: Dakika 2

Newcastle wanajiandaa kwa Liverpool kurejea na dau jipya la kati ya pauni milioni 120-130 kumnunua fowadi wao wa Uswidi Alexander Isak, 25. (Teamtalk), kutoka nje.

Wolves wanakabiliwa na vita vya kumbakisha mshambuliaji wa Norway Jorgen Strand Larsen, huku Newcastle wakishinikiza kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa takriban pauni milioni 60. (Express and the Star}

Manchester United wamefahamisha Napoli kwamba wako tayari kumtoa Mshambuliaji wao raia wa Denmark Rasmus Hojlund, 22 kwa mkopo au kupitia makubaliano ya kumuuza kabisa. (Fabrizio Romano)

Everton wana nia ya kumsajili beki wa Manchester City na Uholanzi Nathan Ake, 30, ili kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Mail)

Manchester United wanatumai Tottenham itaingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 21, na kutoa ushindani kwa Chelsea. (Givemesport)

Matumaini ya Roma kumsajili winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, kutoka Manchester United huenda yakategemea iwapo wakala wake atapunguza kamisheni ya euro 10m (£8.6m) wanayotaka ili dili hilo lifanyike. (Corriere della Sport In Itali),

Real Betis bado wana matumaini ya kumsajili winga wa Manchester United na Brazil Antony, 25, lakini wameweka jukumu kwa klabu hiyo ya Premier League kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake. (Mail)

Tottenham wanavutiwa na kiungo mshambuliaji Mfaransa Maghnes Akliouche, 23, wa Monaco pamoja na mchezaji wa Como na Argentina Nico Paz, 20. (Subscription required }

Spurs pia inachunguza uwezekano wa kumsajili fowadi wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, kutoka Chelsea. (TeamTalks)

Nottingham Forest imewasiliana na Aston Villa kuhusu kumrejesha beki wa pembeni wa Poland Matty Cash, 28, kwenye klabu na pia wametoa ofa ya kumsajili beki wa kulia wa Sevilla, Jose Angel Carmona, 23. (Mail)

West Ham wamekubali kumtoa kwa mkopo mchezaji wa kimataifa wa Mexico Edson Alvarez, 27, kwa Fenerbahce na wanamfuatilia kiungo wa kati wa Werder Bremen na Austria Romano Schmid, 25, na wanavutiwa na kiungo wa kati wa Lens Mfaransa Andy Diouf, 22. (Guardian),

Hata hivyo, Inter Milan wana uhakika wa kumpata Diouf kwa kandarasi ya miaka mitano katika mkataba ambao unaweza kuwa na thamani ya euro milioni 25 kwa klabu hiyo ya Ligue 1. (£21.6m). (La Gazzetta dello Sport In Itali}

Crystal Palace itajaribu kuwashinda Everton katika mbio za kumsajili winga wa Southampton Muingereza Tyler Dibling, 19, kwa kutoa ofa ya pauni milioni 35 pamoja na kumnunua kijana huyo. (Givemesport)

Borussia Dortmund wanatarajia kukamilisha dili la kumsaini fowadi wa Wolves na Ureno Fabio Silva, 23, hivi karibuni. (Bild in Deutsch)

Imetafsiriwa na Seif Abdalla