Ndege yenye misheni ya nyuklia inayotisha

Majaribio ya bomu la atomiki huko Bikini Atoll mnamo 1946 yalikuwa hatari sana kwa ndege za kawaida.

Uanzilishi wa ndege zisizo na rubani zinazodhibitiwa kwa mbali, hata hivyo, ilikuwa ndio wakati muafaka kutumika.

Haikuwezekana kuondoa macho yako kwenye uzuri wa kutisha na uchafu wa mlipuko wa silaha za nyuklia - wa tano tu katika historia ya binadamu.

Au kuonekana kwa meli za kivita zilizolengwa hadi saizi ya vinyago kwa ukubwa wa wingu zito umbo la uyoga, na kutoweka kwenye vilindi vyeupe vya baharini.

Mnamo Julai 1946, Marekani ililipua mabomu mawili ya nyuklia huko Bikini Atoll katika kile kilichoitwa ‘Operation Crossroads’.

La kwanza lililipuka hewani, la pili chini ya maji. Haya yalikuwa majaribio ya kwanza ya silaha za nyuklia tangu jaribio la Utatu la Mradi wa Manhattan mnamo Julai 1945, na ulipuaji wa kwanza tangu uharibifu wa Nagasaki mwezi uliofuata - na ulihusisha kikosi kazi cha wafanyikazi zaidi ya 42,000, meli 250 na ndege 150, kupanga, kuendesha, kufuatilia, kurekodi na kuchanganua majaribio.

Lakini unawezaje kufuatilia jaribio la nyuklia wakati mlipuko na mionzi ni hatari sana kwa binadamu? Bila shaka jibu ikawa ni kupitia ndege zisizo na rubani.

Jarida moja lilipiga picha ndege ya kivita yenye injini moja iliyokuwa ikipaa kwenye mionzi iliyopita katika wingu la uyoga, lakini haikuwa ndege ya kawaida.

Ilikuwa ndege isiyo na rubani, na haikuwa ndege pekee iliyotumwa wakati wa majaribio.

Mbali na kamera, kulikuwa na kundi la ndege za Grumman Hellcats zisizo na marubani na Boeing B-17 Flying Fortresses.

Ndege hizi za kivita, zikiwa ndio tu zimetoka kutengenezwa mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, zilikuwa na "sauti ndogo" na kuongezwa kwa seti ya vyombo vinavyodhibitiwa na redio, na katika ndege aina ya B-17, kamera za televisheni pia zilijumuishwa kuruhusu rubani kuendesha ndege kutoka kwa "kudhibiti" mbali.

Mabomu na bunduki zilibadilishwa na vyombo kama vile mifuko yenye hewa, mifuko ya plastiki yenye maji, masanduku ya chujio, kamera zinazodhibitiwa na redio, telemeta na vyombo vya kurekodi vya kielektroniki, kupima mionzi katika mifuko ya plastiki yenye maji na athari ya mlipuko kwenye ndege yenyewe.

Kwa jaribio lao la kwanza la umma ndege isiyo na rubani ililazimika kufanya safari hatari zaidi kuliko zote. Walilazimika kuruka kupitia wingu la uyoga.

Mwanasayansi Nikola Tesla na mwanzilishi wa simulizi za hadithi za uwongo HG Wells walibuni silaha za angani zinazodhibitiwa na redio kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia.

Mnamo 1917, maono haya yalikuja hatua moja karibu na ukweli wakati Uingereza ilipofaulu kuwa na ndege ya kwanza isiyo na rubani.

Kufikia 1899-1900, tayari kulikuwa na majadiliano kuhusu wazo kwamba ndege inaweza kuongozwa na redio na kugeuzwa kuwa silaha," anasema Roger Connor, msimamizi katika Idara ya Aeronautics, Makumbusho ya Kitaifa ya Smithsonian ya Anga za Mbali .

"Na katika Vita vya Kwanza vya Dunia, karibu dola zote zinazopigana ziliwekeza nguvu yake kwenye majaribio ya hili."

Mnamo tarehe 15 Septemba 1924, kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani ndege iliyokuwa ikidhibitiwa na kiongoza mbali ilipaa, ikafanyiwa ujanja na kutua salama bila rubani binadamu ndani yake.

Miaka kumi na moja baadaye, Waingereza waliendesha ndege kwa jina DH.82B Queen Bee kulingana na ndege ya mafunzo ya Tiger Moth kwa kutumia kidhibiti mbali.

Zaidi ya ndege hizi 400 zilitengenezwa kufikia 1943.

Ikichochewa na mafanikio ya Uingereza, Jeshi la Wanahewa la Marekani (USAAF) na Jeshi la Wanamaji la Marekani zote zilitengeneza ndege zisizo na rubani: jeshi la anga lilitumia mashine ndogo zaidi.

Katika Vita vya Pili vya Dunia, walipanua wazo hilo kwa mabomu makubwa, yenye injini nyingi na droni ndogo za "mashambulizi".

Mwanzoni mwa programu hizi, rubani binadamu alilazimika kuendesha mashine hizi nje ya njia ya ndege na kisha kupaa.

Kufikia mwisho, rubani angeweza kufanya operesheni nzima akiwa mbali. Ndege hizo ndogo zisizo na rubani, zilizotengenezwa kwa makusudi ziliweza kurusha bomu au topido kwenye shabaha ya umbali wa maili 425 (kilomita 684) - na kuona hatua fulani dhidi ya Japan katika Bahari ya Pasifiki.

Katika majaribio yote mawili, ndege zisizo na rubani zilikwenda mahali ambapo binadamu waliogopa. Zilipitia mawingu yenye umbo la uyoga mashariki hadi magharibi, kwenye mwinuko kutoka 10,000ft hadi 28,000ft (3,040 hadi 8,534m).

Ilikuwa tu wakati wingu la uyoga la jaribio la pili halikupanda kama ilivyotarajiwa na kubainika kuwa baadhi ya droni hazikugundua mionzi yoyote.

Meli za ndege zisizo na rubani zilifanya vyema wakati wa majaribio. Ndege aina ya Hellcats ilizinduliwa kutoka kwa chombo cha ndege, na zote isipokuwa moja ndiyo ilifanikiwa kurejea nchi kavu.

Udhibiti wake ulifeli kabla ya kulipuka kwa bomu. Nyingine, aliibuka kutoka kwa wingu la uyoga jeupe kabisa, lililofunikwa na barafu, na ndege ya kudhibiti ilikaribia kupata maafa, wakati rubani alipoielekeza karibu sana na wingu hilo.

Ilikuwa operesheni ya kwanza ndege aina ya B-17 ambapo safari zote za ndege za kupaa na kutua zilifanyika bila marubani, na misheni ya droni ilifanikiwa bila matukio muhimu.

Milango na madirisha machache kwenye ndege iliingia ndani - na breki za bomu moja ziliharibiwa katika mlipuko huo, na kulazimika kupinduka wakati inaurudi.

Data ilikusanywa kuhusu asili ya wingu la uyoga kwa kupima viwango vya mionzi, sampuli za hewa, na kuchukua picha zilizosawazishwa na uelewa wa kisayansi wa milipuko ya nyuklia - kama vile Geiger inavyosoma mionzi kwenye ndege yenyewe wakati ilikuwa ilitua.

"Majaribio hayo yaliashiria mara ya kwanza kwamba ndege zisizo na rubani zilitumiwa kwa njia muhimu kukusanya data," anasema Connor.

"Ndege zisizo na rubani zingeweza kwenda mahali ambapo hakuna ndege ya binadamu ingeweza kwenda.

Hakukuwa na chaguo jingine la kufaa kwa aina ya sampuli zilizofanywa na ndege hizi zisizo na rubani.

Hii ilianzisha dhana ya Vita Baridi ya kutumia ndege zisizo na rubani kwa misheni ambayo ilikuwa 'chafu, au hatari kwa ndege nyingine."