Tetesi za Soka Ulaya: City, Madrid zamgombania Szoboszlai

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester City na Real Madrid zote zinavutiwa na kiungo wa Liverpool na Hungary Dominik Szoboszlai, mwenye umri wa miaka 25. (AS - in Spanish)

Kiungo wa Manchester United na Uingereza Kobbie Mainoo, mwenye umri wa miaka 20, yuko tayari kuhamia Napoli kwa mkopo mwezi Januari lakini mashetani wekundu hawataruhusu aondoke kwa uhamisho wa kudumu. (Teamtalk)

Winga wa Brazil wa Real Madrid Vinicius Jr, mwenye umri wa miaka 25, anataka kulipwa sawa na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 26, na mvutano wa mkataba wake na klabu unaendelea jambo linalomuweka kwenye hati hati ya kuondoka Bernabeu. (Sport - in Spanish)

Chelsea wamewasiliana na klabu ya Italia Como kuhusu upatikanaji wa mchezaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 21, Nicolas Paz. (Caught Offside)

Liverpool wako tayari kuilipa Inter Milan £88m (euro milioni 100) kwa ajili ya beki wa kati wa Italia Alessandro Bastoni mwenye umri wa miaka 26. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Beki wa kushoto wa Liverpool na Scotland Andy Robertson, mwenye umri wa miaka 31, ataondoka Anfield mkataba wake utakapomalizika msimu ujao wa kiangazi na tayari amefanya mazungumzo na Celtic. (Fichajes - in Spanish)

Bayern Munich hawana nia ya kukatisha mapema mkopo wa mshambuliaji wa Senegal mwenye umri wa miaka 24 Nicolas Jackson kutoka Chelsea, lakini huenda wasimnunue moja kwa moja mwishoni mwa msimu. (Bild - in German)

Wolfsburg wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa West Ham Niclas Fullkrug mwezi Januari, huku Augsburg pia wakivutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32 ambaye amepewa ruhusa ya kuondoka Hammers. (Florian Plettenberg)

Kocha wa Newcastle Eddie Howe anaungwa mkono kikamilifu na wamiliki wa Saudi wa klabu hiyo na afisa mtendaji mkuu mpya David Hopkinson licha ya kuwa na mwanzo mbaya wa msimu. (The I)

Antonio Conte hatajiuzulu kama kocha wa Napoli lakini atakutana na mmiliki wa klabu Aurelio de Laurentiis katika siku chache zijazo ili kutafuta suluhisho la changamoto za timu msimu huu. (Il Mattino - in Italian)