Tetesi za Soka Ulaya: Arsenal, PSG zinamtaka Ndicka, Newcastle Mbeumo

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wanamtaka mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, mwenye umri wa miaka 25, lakini wana wasiwasi kuhusu ada yake ya uhamisho ya £60m. (Telegraph)
Newcastle pia hawatakuwa na nia ya kumfuatilia kwa muda mrefu beki wa kati wa Bournemouth Dean Huijsen, mwenye umri wa miaka 20, baada ya kujifunza kutokana na juhudi za mwaka jana za kushindwa kumsaini beki wa England Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 24 kutoka Crystal Palace. (i paper)
Arsenal wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Paris St-Germain kumsaini beki wa Roma kutoka Ivory Coast Evan Ndicka, mwenye umri wa miaka 25, ambaye thamani yake iko kati ya £25-34m. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanataka kumsajili beki wa kati wa Ujerumani Jonathan Tah, mwenye umri wa miaka 29, majira ya kiangazi baada ya mkataba wake kumalizika na Bayer Leverkusen. (Sky Sports)
Chelsea hawana mpango wa kumuuza kiungo wao kutoka Argentina Enzo Fernandez, mwenye umri wa miaka 24, aliyesajiliwa kwa rekodi ya £107m, ambaye pia anafuatiliwa kwa muda mrefu na Real Madrid. (Sky Sports)
Manchester United wamekubaliana kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Enzo Kana-Biyik, mwenye umri wa miaka 18 kutoka Le Havre. (Fabrizio Romano)
Bayer Leverkusen wanataka kumzuia kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz kujiunga na Bayern Munich majira haya ya kiangazi, huku Manchester City na Real Madrid pia wakivutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Germany)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wako tayari kumruhusu kipa wa Ukraine Andriy Lunin, mwenye umri wa miaka 26, kuondoka msimu huu, huku kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga, Mhispania mwenye umri wa miaka 30, kwa sasa akiwa mkopo Bournemouth, akizingatiwa kuwa mbadala wake. (Mundo Deportivo)
Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 33, ambaye ataondoka Manchester City mwishoni mwa msimu. (Football Insider)
Crystal Palace watataka zaidi ya £80m kama wataamua kumuuza kiungo wa England Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 21, majira haya ya kiangazi. (Teamtalk)













