Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 03.06.2024

Bayern Munich wanataka kumsajili Bruno Fernandes, Jadon Sancho anaweza kuichezea tena Manchester United na Victor Osimhen anasubiri ofa kutoka kwa Arsenal.

Bayern Munich wanatafuta saini ya kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 29, kutoka Manchester United . (O Jogo - kwa Kireno)

Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 24, yuko tayari kurejea United kufuatia kipindi cha mkopo cha winga huyo wa Uingereza katika klabu ya Borussia Dortmund - lakini tu ikiwa Erik ten Hag ataondoka msimu huu wa joto(Mirror)

Mshambulizi wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, mwenye umri wa miaka 25, anasubiri ofa kutoka kwa Arsenal au Saudi Arabia. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekutana na mkurugenzi wa michezo wa Crystal Palace Dougie Freedman mjini London kuchunguza msimamo wao kuhusu uwezekano wa kuwauza beki wa Uingereza Marc Guehi, 23, kiungo wa kati wa Uingereza Eberechi Eze, 25, na winga wa Ufaransa aliye Michael Olise 22, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Palace italenga kumsajili winga wa Leeds Mholanzi Crysencio Summerville mwenye umri wa miaka 22, ikiwa itabidi kumuuza Olise au Eze msimu huu wa joto.(Mirror)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, ambaye atafikisha miaka 33 baadaye mwezi huu, anatarajiwa kupokea ofa za kuondoka Manchester City msimu huu wa joto. (Football Insider)

Cristiano Ronaldo amezungumza na wachezaji wenzake wawili wa zamani kwa lengo la kuwashawishi wajiunge naye katika klabu ya Al Nassr - beki wa Real Madrid na Uhispania Nacho Fernandez, 34, na kiungo wa kati wa Manchester United na Brazil Casemiro, 32. (Marca - kwa Kihispania).

Tottenham wanaweza kuwasilisha ofa kwa winga wa Nottingham Forest wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 23, kabla ya mwisho wa mwezi. (Football Insider)

Newcastle United itajaribu kukamilisha mpango wa kumnunua beki wa kati wa Bournemouth Lloyd Kelly, 25, wiki hii. (Telegraph)

West Ham wamekaribia kuafikia mkataba wa pauni milioni 25.5 kumsaini mshambuliaji wa Brazil Luis Guilherme kutoka Palmeiras , 18(Times)

Fulham wamemweka Emile Smith Rowe wa Arsenal kuwa mojawapo ya vipaumbele vyao vya uhamisho wa majira ya joto na wako tayari kuwasilisha ofa kwa kiungo huyo wa kati wa Uingereza, mwenye umri wa miaka 23, mapema katika kipindi cha uhamisho (Telegraph)

Los Angeles Galaxy wametuma ofa ya mkataba kwa kiungo wa zamani wa Ujerumani Marco Reus, 35, ambaye anatazamiwa kuwa mchezaji huru baada ya kucheza mechi yake ya mwisho Borussia Dortmund . (Fabrizio Romano)

Kocha wa Leicester City Enzo Maresca atatangazwa kuwa kocha mpya wa Chelsea siku ya Jumatatu, baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano. (Fabrizio Romano)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte anatarajiwa kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Napoli wiki hii. (Nicolo Schira)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah