Watoto Pekee: Sayansi inasema nini hasa kuhusu athari za kutokuwa na Ndugu

Chanzo cha picha, Getty Images
Ubinafsi, kupenda kutawala,wagumu kueleweka katika jamii, wivu, kutaka mambo yako ndio yafanyike na, hasira ya mara kwa mara.
Sifa zao mbaya huwatangulia. Hata hivyo, tafiti nyingi zinaonyesha kwamba hizi si sifa zinazoonekana miongoni watoto pekee, na kwamba watoto pekee, kwa njia nyingi, hawana tofauti hasa na watoto ambao wana ndugu.
"Ushahidi, kwa ujumla, hauungi mkono wazo kwamba watoto wanaokua kama watoto pekee wana upungufu wa aina fulani katika ujuzi wao wa kijamii, ikilinganishwa na watoto wanaokua na ndugu," Alice Goisis, profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha London.
Watoto hao "wanalinganishwa katika utu, uhusiano na wazazi wao, mafanikio, vichocheo na mazoea ya kibinafsi na watoto ambao wana ndugu," anaongeza mtafiti.
Utafiti uliofanywa na Goisis na wenzake unaonyesha kwamba mambo mengine ya umuhimu mkubwa huathiri ukuaji wa watoto, kama vile, kwa mfano, hali ya kijamii na kiuchumi ya familia au rasilimali za kihisia zinazopatikana kwa wazazi.
Ingawa baadhi ya utafiti unaonyesha tofauti, Goisis anadokeza kuwa sababu zinazosababisha hitilafu hizo ni kutokana na muktadha na si ukweli halisi wa kuwa mtoto wa pekee.
"Tuligundua, kwa mfano, kwamba nchini Uingereza, ambapo mtoto wa pekee ni kiashiria cha kukua katika familia yenye faida, watoto hawa walikuwa na afya sawa au bora baadaye maishani ikilinganishwa na watoto ambao walikuwa na ndugu."

Chanzo cha picha, Getty Images
"Ingawa katika Uswidi, ambako desturi ya kuwa na watoto wawili imeenea na watoto pekee wanaelekea kutoka katika familia zilizo katika hali mbaya ya kiuchumi, watoto hao huwa na afya mbaya zaidi baadaye maishani," asema Goisis.
Faida
Ingawa athari katika suala la utambuzi au urafiki inaweza kuwa muhimu, na inatokana na kiwango kikubwa zaidi na muktadha ambapo mtoto huyo hukua, hii haimaanishi kwamba hatuwezi kuona tofauti.
Kila nafasi ndani ya familia - iwe katika nafasi ya mtoto mkubwa, wa kati au mdogo - ina faida na hasara zake, Linda Blair, mwanasaikolojia wa kimatibabu anayeishi Uingereza, anaelezea BBC.
Na hali hii ya faida zaidi au kidogo sio tofauti kwa mtoto wa pekee, ingawa "hiki ndicho kikundi cha familia ambacho kimebadilika zaidi katika miaka 40 au 50 iliyopita,"
Mojawapo ya faida alizoziona Blair katika tajriba ya zaidi ya miaka 40 ni ubora wa kiisimu ambao huwa nao watoto pekee.
"Hii hutokea kutokana na mchango wa lugha wa wazazi, ambao hauingiliki na ule wa watoto wengine, ambao hautokani na wenzao, na ambao ni muhimu kwa ukuaji wa ubongo katika miezi 24 au 36 ya kwanza ya maisha."
Hii inawapa watoto faida kubwa ya kitaaluma , anaongeza

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa upande mwingine, wao ni kawaida sana katika kupanga na kutumia wakati wao wa ziada , kwa kuwa hawana ndugu au dada, wanapaswa kutafuta na kuamua nini cha kufanya nayo.
Hatimaye, Blair asema, “wana uhusiano kwa urahisi zaidi na watu wenye umri mkubwa zaidi, kwa sababu wao hufanya hivyo nyakati zote.”
Hasara
Kwa upande mwingine, kutokuwa na ndugu kunaweza kumweka mtoto katika hali mbaya zaidi.
"Kuna utafiti unaoonyesha kwamba ndugu wanaweza kuwa na athari ukali wakati kuna uhusiano usio mzuri kati ya wazazi nyumbani ," Adriean Mancillas, mwanasaikolojia, anaelezea BBC Mundo.
Mancillas anasema ni muhimu katika hali kama hii kuzingatia kutafuta msaada zaidi ya wazazi, kama vile marafiki wa karibu au wanafamilia ili kutoa ushauri zaidi kwa ajili ya manufaa ya mtoto pekee.

Chanzo cha picha, Getty Images
Upungufu mmoja uliobainishwa na Blair ni ukosefu wa kile kinachoitwa "wajanja wa mitaani" kwa watoto pekee . Blair anarejelea aina hiyo ya akili angavu na ya vitendo, “ambayo hukuruhusu kutambua upesi kile ambacho mtu atafanya na kwamba huwezi kujifunza ikiwa huishi na watu wa rika kama hilo.”
Sifa nyingine, anaongeza, ni kwamba kwa vile wanatumia muda mwingi wakiwa peke yao, au wakiwa na watu wazima, hawajisikii vizuri katika hali ya malumbano.
Blair anasisitiza kwamba hizi ni sifa za jumla, na kwamba, kama tulivyotaja mwanzoni, hakuna seti ya sheria zinazoruhusu kuelezea mtoto wa pekee.
Lakini ikiwa sayansi inaondoa ubaguzi unaowazunguka watoto pekee unaowapaka rangi zisizopendeza, kwa nini ni vigumu sana kutokomeza

Chanzo cha picha, Getty Images
"Ugonjwa wenyewe"
Mawazo mabaya kuhusu mtoto pekee yalianzia mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni mwa karne ya 19, wakati saikolojia ya watoto ilikuwa ikiimarisha misingi yake kama uwanja wa masomo ya kitaaluma.
G. Stanley Hall , mwanasaikolojia wa Marekani na mwanzilishi katika eneo hili la utafiti, alichapisha mfululizo wa maandiko ambayo anaelezea watoto wasio na ndugu na sifa nyingi ambazo utamaduni maarufu unawapa leo.
Hata hivyo, mwanasaikolojia mwingine, anayejulikana sana kuliko Hall, alikuwa na ushawishi mkubwa katika kuendeleza dhana mbaya karibu na watoto pekee: Alfred Adler wa Austria, Mancillas anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Adler alikuwa mwanasaikolojia wa kwanza kuchunguza na kuandika kwa kina kuhusu mpangilio wa kuzaliwa na jinsi muundo wa familia unavyoathiri ukuaji wa watoto," anaiambia BBC.
"Katika maandishi ya Adler kuhusu uchunguzi wake mwenyewe wa watoto hawa ambapo , alielezea kwamba sio tu watoto hawa walioharibiwa, lakini kwamba wazazi ambao walichagua kutokuwa na watoto zaidi walikuwa wakimfahamisha kuhusu madhara wanayoyapitia kisaikolojia watoto pekee,” anaongeza.
Upepo wa mabadiliko
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ingawa mbinu za utafiti za watafiti hawa zilitiliwa shaka baadaye na nadharia zao kukanushwa na tafiti nyingi zilizofuata, ni hekaya ambayo ni vigumu kuitokomeza.
Goisis anaamini kwamba ni kwa sababu familia inayoundwa na watoto wawili bado inatawala kama kawaida, ambayo mtoto wa pekee anaendelea kuwa kitu nje ya kawaida na, kwa hivyo, inachukuliwa kuwa tofauti (na isiyofaa).
PICHA: Idadi ya familia zenye mtoto mmoja tu inaongezeka.
Kwa Mancillas, kujadili masuala haya na kuleta utafiti na taarifa sahihi kwa umma ndiyo njia ya hatimaye kubadili mitazamo.
"Hii ni kweli kwa ubaguzi wowote ," asema.
"Wakati mtizamo fulani wa upendeleo dhahiri unaonekana wazi, ndipo tunaweza kuzibadilisha ili kusahihisha fikra zenye upendeleo na potofu ambazo zingedhuru mtu au kikundi kingine."
"Tunapotumia hili kwa watoto na wazazi pekee, hii inamaanisha kuhakikisha kwamba habari zinapatikana kwa wingi ili wazazi waweze kujiamini katika uamuzi wao wa kupata mtoto mmoja pekee," Mancillas anamalizia.
Bado, mitazamo kuhusu watoto pekee inabadilika sana, kwa sababu ya mabadiliko katika mtindo wa sasa wa familia, Blair anasisitiza.
Ingawa siku za nyuma kuwa mtoto wa pekee lilikuwa jambo lisilo la kawaida, “leo hali ni tofauti sana.
Nchini Uingereza, kwa mfano, asilimia 40 ya familia zina mtoto mmoja tu, na inakadiriwa kufikia 2030, hii itakuwa nusu ya familia,” anasema Blair.















