Tetesi za soka Ulaya Jumapili 16.06.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wameanza mazungumzo ya ndani kuhusu uhamisho wa beki wa Bayern Munich Mholanzi Matthijs de Ligt, 24, ambaye ana thamani ya takribani euro 50m (£42.3m). (Sky Sport Germany)
Manchester United hawana nia ya kufikia thamani ya Everton ya pauni milioni 70 kumnunua mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, na watatishia kuachana na mkataba wowote, baada ya ofa ya awali yenye thamani ya hadi £43m kukataliwa. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wana nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Uingereza Keira Walsh, 27. (Athletic )
Valencia wamewasilisha ombi la pauni milioni 25 kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 22, huku mshambuliaji huyo wa Uingereza, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Juventus, akitaka kusalia Hispania baada ya kucheza kwa mkopo Getafe msimu uliopita. (Mirror)
Mlinzi wa Uingereza Jack Grealish, 28, anaweza kutaka kuondoka Manchester City baada ya kuhangaika katika kikosi cha kwanza msimu uliopita lakini mshahara wake mkubwa na mkataba wake hadi 2027 unaweza kuwa kikwazo. (Football Insider)
AC Milan ilituma skauti kumtazama Armando Broja, 22, akiichezea Albania dhidi ya Italia Jumamosi huku klabu hiyo ya Serie A ikitathmini uwezekano wa kumnunua mshambuliaji huyo wa Chelsea. (Sky Sports Italia)

Chanzo cha picha, Getty Images
Lille wamekataa dau la pauni milioni 42.3 kutoka kwa klabu ambayo haijatajwa jina la mlinzi wa kati wa Ufaransa Leny Yoro, 18, ambaye amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Liverpool na Manchester United lakini inasemekana anapendelea uhamisho wa kwenda Real Madrid. . (Express)
Mlinzi wa Manchester United Victor Lindelof, 29, analengwa na mkufunzi mpya wa Fenerbahce Jose Mourinho, ambaye alifanya kazi na mchezaji huyo wa Sweden wakati alipokuwa Old Trafford. (Fotomac)
Manchester United wameungana na AC Milan na Borussia Dortmund kumuwinda mshambuliaji wa RB Salzburg Oghenetejiri Adejenughure, 17, ambaye alifunga mabao manne katika michezo minne akiwa na Austria wakati wa michuano ya hivi karibuni ya Uropa kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17. (Express )

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanalenga kuteka nyara uhamisho wa Real Madrid kwa kiungo wa kati wa River Plate Muargentina Franco Mastantuono, 16, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa cha pauni milioni 45. (Sport via 90 Min)
Hivi karibuni Liverpool walifanya uchunguzi kuhusu mlinzi wa kati wa Stuttgart, Waldemar Anton, 27, ambaye yuko kwenye kikosi cha Ujerumani kwenye Euro 2024 na ana kipengele cha kutolewa cha euro 22.5m (£19m). (Sport Bild )
Juventus wamesonga mbele ya Borussia Dortmund katika kujaribu kumsajili winga wa Manchester United Jadon Sancho, 24, ambaye alitumia kipindi cha pili cha msimu uliopita kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ujerumani. (Football Insider)












