Kwa nini wazalishaji wakuu wa mafuta duniani wanapunguza usambazaji wa bidhaa hiyo?

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Urusi inazalisha zaidi ya mapipa milioni 10 ya mafuta kwa siku.

Saudi Arabia imetangaza kuwa itapunguza uzalishaji wake wa mafuta ghafi kwa mapipa milioni moja kwa siku ili kujaribu kuongeza bei.

Wanachama wengine wa kundi la OPEC+ la wazalishaji wa mafuta wamekubali kutobadilisha viwango vya bei baada ya kupunguza pato kwa zaidi ya mapipa milioni moja kwa siku Aprili iliyopita.

Wachambuzi wa wa masuala ya biashara ya mafuta hawatarajii kupunguzwa kwa hivi karibuni kusababishe kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta ghafi duniani.

OPEC+ ni nini?

OPEC+ ni kundi la nchi 23 zinazouza nje mafuta ambazo hukutana mara kwa mara ili kuamua ni kiasi gani cha mafuta ghafi cha kuuza mafuta kwenye soko la dunia.

Wanachama 13 wa OPEC (Shirika la Nchi Zinazouza Petroli), ambazo hasa ni nchi za Mashariki ya Kati na Afrika, ndio kiini cha kundi hili.

OPEC iliundwa mnamo 1960 kama shirika la usawazishaji wa usambazaji wa mafuta na bei, duniani.

Nchi za OPEC huzalisha karibu 30% ya mafuta ghafi duniani. Saudi Arabia ndio muuzaji mkubwa wa mafuta katika kundi hilo, na inazalisha zaidi ya mapipa milioni 10 kwa siku.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Mnamo 2016, wakati bei ya mafuta ilipokuwa chini sana, OPEC iliungana na wazalishaji wengine kumi kuunda OPEC+.

Mmoja wa wanachama wa kundi hili kubwa ni Urusi, ambayo pia inazalisha zaidi ya mapipa milioni 10 kwa siku.

Kwa pamoja, nchi za OPEC+ zinazalisha karibu 40% ya mafuta ghafi duniani.

"OPEC+ hurekebisha usambazaji na mahitaji ili kusawazisha soko," anasema Kate Dourian wa Taasisi ya Nishati. "Inaweka bei ya juu kwa kupunguza usambazaji wakati mahitaji ya mafuta inapopungua.

Shirika pia hilo pia linaweza kupunguza bei kwa kuleta mafuta zaidi sokoni.

Unaweza pia kusoma:

Kwa nini OPEC+ inapunguza uzalishaji wa mafuta?

Upunguzaji wa hiari wa mapipa milioni moja kwa siku ulioamuliwa na Saudi Arabia utaanza kutekelezwa mwezi Julai.

Hii inafuatia kupunguzwa kwa mapipa milioni 1.16 kwa siku mwezi wa Aprili, jambo lililofanywa kwa hiari na wanachama wanane wa OPEC+, na mapipa milioni mbili kwa siku kukatwa kwa kundi kote mwezi Oktoba 2022.

Saudi Arabia, ambayo kwa sasa ni mwenyekiti wa OPEC+, inakadiriwa kuhitaji bei ya mafuta ghafi kupanda hadi $80 (£65) kwa pipa au zaidi ili kufidia garama ya matumizi ya serikali na ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje.

Mnamo 2020, bei ya mafuta yasiyosafishwa iliashuka kwa sababu ya ukosefu wa wanunuzi wakati nchi zilipokuwa zikikabliwa na janga la covid. Iliibidi OPEC+ ikuongeza bei kwa kupunguza kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji, kwa zaidi ya mapipa milioni tisa kwa siku.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Boris Johnston alishindwa kuishawishi Saudi Arabia na nchi nyingine kuongeza uzalishaji wao wa mafuta.

Kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, bei ya mafuta ghafi ilipanda hadi zaidi ya $130 kwa pipa. Lakini kufikia Machi 2023 ilikuwa imeshuka hadi zaidi ya $70 kwa pipa, kikiwa ni kiwango chake cha chini kabisa katika miezi 15.

David Fyfe wa kikundi cha utafiti wa tasnia ya mafuta ya Argus Media anaamini kuwa kupunguzwa kwa hivi karibuni kwa uzalishaji kunaweza kusababisha kuongezeka kwa $80 kwa pipa.

"Tunashuhudia kuzorota kwa kasi kwa ukuaji wa uchumi katika nchi zilizoendelea, hadi kufikia hatua ambayo zimekaribia kuingia kwenye mdororo," alieleza. "Na hatufikirii mahitaji ya mafuta nchini China yataongezeka sana katika miezi michache ijayo, hivyo soko halitakuwa gumu katika nusu ya pili ya mwaka."

Nini kinaendelea kuhusu mafuta ya Urusi?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vladimir Putin na Katibu Mkuu wa OPEC Mohammad Barkindo.

Baada ya Urusi kuivamia Ukraine, nchi za Umoja wa Ulaya ziliacha kuagiza mafuta ya Urusi yanayosafirishwa kwa njia ya bahari, na nchi kama Marekani na Uingereza ziliacha kabisa kuagiza mafuta hayo kutoka nje ya nchi.

Urusi sasa inasafirisha bidhaa ghafi zaidi kwa nchi kama vile India na Uchina, ambazo haziiwekei vikwazo vya Magharibi Moscow.

Hata hivyo, kundi la mataifa ya G7 linajaribu kuweka mapato ya chini ya mafuta ya Urusi kwa kuweka bei ya kikomo ya dola 60 kwa pipa kwa mafuta inayosafirisha nje.