Bomba la Mafuta kutoka Urusi hadi China, fursa mpya kwa Urusi kukwepa vikwazo?

Chanzo cha picha, Getty Images
China inataka kubadilisha nishati inayohitajika na mamilioni ya viwanda vyake. Urusi inataka kumtosa mteja wake - Ulaya - ambaye inakosoa uvamizi wake huko Ukraine na haitaki kulipia gesi ya Urusi kwa pesa ya rubles (ya Urusi).
Jambo la msingi, inaweza kuonekana kuwa mataifa hayo mawili yanaweza kuelewana na kuwa washirika wakubwa wa kibiashara, hasa wakati ambapo wawili hao wanakabiliwa na uhusiano mgumu na nchi za Magharibi.
Ile ambayo ingefaidika zaidi, wachambuzi wanasema, itakuwa Urusi, ambayo inaweza kukwepa kwa kiasi vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa kutokana na vita vya Ukraine. Pia itaweza kuweka sehemu ya uzalishaji wa gesi ambayo haitiatuma tena Ulaya, ambaye ndiye mteja wake mkubwa zaidi.
Serikali za Ulaya zimetumia miezi michache iliyopita kutafuta kupunguza utegemezi wao wa nishati ya Urusi, ambayo hadi wakati huo asilimia 40% ya gesi inayotumiwa Ulaya inatoka Urusi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini kutengeneza washirika kwenye sekta hii inaweza kuchukua muda mrefu,miaka, haswa linapokuja suala la miundombinu ya nishati. Mfano wa wazi zaidi ni uhusiano huu wa muda mrefu wa bomba la Power of Siberia 1 ambalo makampuni ya nishati ya serikali, Gazprom ya Russia na China National Petroleum Corp, yamekuwa yakijenga kwa takriban miaka minane sasa.
Bomba hilo linaloweza kusafirisha gesi kutoka Siberia hadi Shanghai zaidi ya kilomita 3,000 liko katika hatua za mwisho, ingawa tayari lisambaza mafuta njiani katika maeneo mbalimbali ya kaskazini mwa China.
Urusi imekuwa ikipeleka gesi zaidi nchini China tangu mwezi Februari, wakati uvamizi wa Ukraine ulipoanza.
"Bomba hilo linaweza kusambaza hadi mita za ujazo bilioni 38 (bmc) kwa mwaka, lakini kabla ya mzozo, Urusi ilisambaza takriban ujazo wa bilioni 4 au 5.
Usafirishaji sasa umeongezeka kwa asilimia 63.4% na wazo ni kwamba ifikapo mwaka 2023 iweze kusambaza asilimia 100," Pablo Gil, mwanamkakati mkuu wa wakala wa XTB wa Uhispania na Amerika Kusini, aliiambia BBC Mundo.
Je, Urusi inataka kuifanya China kuwa mteja mkuu wa gesi kuibadili Ulaya?

Chanzo cha picha, Getty Images
"Huo ni mpango wa Urusi, lakini haionekani kuwa utawezekana kwa muda mfupi," anaelezea Ángel Saz-Carranza, mkurugenzi wa Kituo cha Uchumi wa Kimataifa na Geopolitics huko Esade.
"Mnamo 2021, Urusi iliuza tu 3.5% ya gesi kwenda Uchina na zaidi ya 40% kwa Ulaya (EU). Hivi sasa, kwa bomba la gesi pekee - Power of Siberia 1 - uwezo wa kupeleka gesi China kupitia bomba ni 60,000 bcm," anaongeza Saz-Carranza.
Ikiwa tunalinganisha takwimu hizi na karibu mita za ujazo milioni 150,000 za uwezo wa jumla wa mabomba ambayo huunganisha Urusi na Ulaya, inaeleweka kwa nini kuchukua nafasi ya wateja kutoka Bara hilo haitakuwa rahisi sana.
Mtandao mpya wa bomba la gesi
Urusi inatathmini ujenzi wa mabomba kadhaa ya gesi ambayo yataruhusu kupanua uwepo wake katika soko la Asia, lililopuuzwa kwa miaka kutokana na mahitaji makubwa ya Ulaya.
"Tunajua kuwa soko la China ndilo soko lenye nguvu zaidi duniani na katika miaka 20 ijayo ongezeko la matumizi ya gesi nchini China litachangia 40% ya ongezeko la matumizi ya gesi duniani," Mkurugenzi Mtendaji wa Gazprom Alexei Miller alisema hivi karibuni.
Moja ya miradi maarufu hivi sasa ni tawi la pili la bomba la Siberia, inayoitwa Siberia 2. Bomba jipya linaloweza kusafirisha gesi asilia ya mita za ujazo milioni 50,000 kwa mwaka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Bomba la Power of Siberia 1 halijaunganishwa na bomba linalosafirisha gesi Ulaya, ambapo inamaanisha kwamba haiwezi kbadili uelekeo wa gesi inayozalishwa na kupelekwa mahali pengine. Haitakuwa hivyo wakati bomba la Power of Siberia 2 litajengwa, au angalau huo ndio mpango." "anasema Garcia Herrero. "Mwishowe, Urusi inachotaka ni kuwa na uwezo wa kupeleka gesi nchini China wa takriban 100,000 bcm kwa mwaka wakati ina miundombinu yote hii," anasema Gil.
"Ni miundombinu mipya, ambayo Urusi italazimika kufanya uwekezaji mkubwa. Ni mchakato ambao nadhani umepangwa kwa mwaka 2027, ambao Ulaya imependekeza kufunga utegemezi wake wote wa matumizi ya nishati. Mafuta ya Urusi. Tunazungumzia juu ya mradi wa miaka mitano, "anaongeza mchambuzi wa XTB.
"Ikiwa Urusi inataka kuchuma mapato ya rasilimali zake za gesi katika siku zijazo, inapaswa kuwekeza katika miundombinu mipya na italazimika kutafuta wanunuzi wapya, ikiwemo China," anaeleza Norbert Rücker, mkuu wa utafiti wa kiuchumi katika benki ya Uswizi Julius Baer.
Vikwazo vya Magharibi, vilivyoanza wakati Urusi ilipotwaa Crimea mwaka wa 2014, vinaisukuma kutafuta wateja wapya, ikiwemo China na India. Hakuna nchi yoyote kati ya hizi mbili iliyojiweka wazi kuunga vikwazo vilivyowekwa na Marekani na Ulaya.
China kunufaika na bei nzuri

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo, vikwazo hivi vinairuhusu China kununua gesi ambayo Urusi haiwezi kuiuza mahali pengine kwa bei nzuri. Na katika shauku yake ya kupanua vyanzo ambavyo inanunua nishati, Beijing imekataa kulaani Moscow kwa uvamizi wake wa Ukraine. "Vikwazo vya Magharibi kwa nishati ya Urusi vinaweza kuisaidia China kufikia makubaliano kwa bei ya chini ya soko," Natixis anaamini hivyo.
Wachambuzi wanaamini kuwa Urusi inahitaji wazi kuungwa mkono na China, sio tu kununua gesi kutoka kwake lakini kuiruhusu kuagiza vifaa vingine vingi. "Kuna sababu kwa nini bomba la "Power of Siberia 2" haijajengwa bado. Hii ni bomba refu sana, lenye utata mkubwa na kwa hiyo pia ni ghali sana, "anasema Rücker.












