Nchi kumi ambazo watu wake wana silaha nyingi zaidi duniani

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtu akibeba bunduki

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya risasi nchini Marekani na kusababisha vifo vya watu wengi na wengine kujeruhiwa. Mara kwa mara mashambulizi hayo yanatokana na idadi kubwa ya silaha mikononi mwa watu.

Katika mwaka wa 2023 pekee, kumekuwa na ufyatuaji risasi wa watu 130 nchini Marekani. Moja ya shambulio hilo lilikuwa la hivi punde zaidi lililolenga shule moja huko Nashville Jumatatu asubuhi.

Watu sita wakiwemo watoto watatu waliuawa katika shambulio hilo lililofanywa na mtu mwenye silaha.

Idara inayokusanya takwimu za matumizi ya silaha mikononi mwa raia inasema kuwa katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la ufyatuaji risasi.

Katika kila moja ya miaka mitatu iliyopita kumekuwa na zaidi ya matukio 600 nchini Marekani ya ufyatuaji wa risasi, ambayo ni sawa na wastani wa kupigwa risasi mara mbili kwa siku.

Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu namna ya kudhibiti silaha mikononi mwa wananchi, huku kukiwa bado hakuna muafaka wa kutekeleza sheria ya kupiga marufuku silaha.

Wamarekani wana bunduki ngapi?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ingawa ni vigumu kuhesabu idadi ya silaha na bastola mikononi mwa raia duniani kote, uchunguzi wa hivi punde zaidi wa shirika la utafiti wa silaha ndogo ndogo lenye makao yake makuu nchini Uswisi liitwalo Small Arms Survey unakadiria kuwa takriban bunduki milioni 390 ziko mikononi mwa Umma nchini Marekani.

Shirika hili lilifanya makadirio hayo mwaka wa 2018, na inawezekana kwamba idadi hiyo sasa ni kubwa kuliko hiyo.

Makadirio ya jumla yanaonyesha kuwa idadi hii inamaanisha kuwa kuna bunduki 120.5 kwa kila raia 100.

Mnamo 2011, kulikuwa na bunduki 88 kwa kila watu 100. Hii ni zaidi ya idadi ya silaha mikononi mwa watu wa nchi zingine ulimwenguni.

Nchi ya Yemen, ambayo ndio ya pili baada ya Marekani kwa umiliki wa bunduki miongoni mwa raia, ina chini ya nusu ya idadi ya silaha ambazo watu wa Marekani wanamiliki.

Nchi kumi ambazo raia wake wana silaha nyingi zaidi

.

Chanzo cha picha, Getty Images

United States: 120.5% ya Wamarekani anamiliki bunduki

Yemen: Watu 100 wanamiliki bunduki 52.8

Serbia: Watu 100 wanamiliki bunduki 39-1

Montenegro: watu 100 wanamiliki bunduki 39-1

Uruguay: 34.7% wanamiliki bunduki

Canada: 34.7% wanamiliki bunduki

Cyprus: 34% wanamiliki bunduki

Finland: 32.4% wanamiliki bunduki

Lebanon: watu 100 wanamilikini bunduki 31.9

Iceland: 31.7% wanamiliki bunduki