Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 18.08.2022
Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji Mmarekani Christian Pulisic, 28, kutoka Chelsea kwa mkopo wa msimu mzima(Times - subscription required)
Manchester United imekataliwa dau la pauni milioni 110 na Atletico Madrid kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 22. (AS - in Spanish)
Mshambulizi Antony sio chaguo tena kwa kwa Manchester United huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 akisema kuwa ana furaha katika kilabu ya Ajax, licha ya kuhusishwa na klabu hiyo ya Ligi ya Premia katika kipindi chote cha uhamisho wa wachezaji. (De Telegraaf - in Dutch, subscription required)
Everton wanafikiria kumsajili fowadi wa Chile Ben Brereton Diaz kutoka Blackburn Rovers huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akizingatiwa kama mbadala wa fowadi wa Uingereza aliyejeruhiwa Dominic Calvert-Lewin, 25. (Sky Sports, via Express)
Klabu ya Ufaransa Nice ilikuwa imetoa ofa ya £8.5m kwa Brereton Diaz mapema wiki hii, ambayo Blackburn bado hawajaikubali au kuikataa, huku West Ham pia wakionyesha nia ya kumtaka Mchile huyo. (Sun, via Metro)
Mchezaji wa Leicester City Wesley Fofana anaamini kwamba Foxes wanamwekea gharama ya juu ili asipate uhamisho- huku klabu hiyo ikisemekana kuomba ada ya rekodi ya zaidi ya pauni milioni 80 walizopokea kwa beki wa Manchester United Harry Maguire, 29 - kwa mchezaji huyo wa miaka 21
Nottingham Forest wamekubaliana masuala ya kibinafsi na Houssem Aouar wa Lyon lakini bado hawajafikia makubaliano ya ada ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, ambaye hapo awali alivutiwa na Arsenal. (L'Equipe - In French)
Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 67 kwa kiungo wa kati wa Real Madrid Casemiro, 30 na mara mbili ya mshahara wa Mbrazil huyo hadi £360,000 kwa wiki, baada ya mazungumzo na kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, 27, kuvunjika. . (Relevo - in Spanish)
Lakini sasa dili la Casemiro inasemekana kuwa haiwezekani kwa United, huku mchezaji huyo akisemekana hataki kuhama na Chelsea pia ikionyesha nia. (Talksport)
United pia wanafikiria kumsajili beki wa kulia wa Ubelgiji Thomas Meunier, 30, kutoka Borussia Dortmund kama watamuuza beki wa pembeni wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka, 24, kurudi Crystal Palace kwa £10m. (Telegraph - subscription required)
The Red Devils wanajipanga kumnunua mlinda lango wa kimataifa wa Uswizi wa Borussia Monchengladbach Yann Sommer, 33, ili kumpa changamoto David de Gea. (Blick, via Sun)
Sporting Lisbon wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amewaambia mara kwa mara Manchester United kwamba anataka kuondoka. (90min)
Willian anaweza kurejea Ligi ya Premia kwani ripoti zinaonyesha yuko tayari kuanza mazungumzo na Fulham, winga huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 34 hivi karibuni aliondoka Corinthians na anaweza kusajiliwa bila malipo. (Mail)
Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang angependelea kuondoka Barcelona na kwenda Chelsea kuliko Manchester United, kulingana na ripoti ambazo pia zinaonyesha kwamba Barcelona wanamthamini kwa pauni milioni 25, kiasi ambacho Chelsea inasita kumlipa mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon, 33. (Telegraph, via Express)
Tottenham wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ukraine Ruslan Malinovskyi kutoka Atalanta, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atakuwa wa nane kusajiliwa na Spurs katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (TuttoAtalanta - In Italian)
Southampton na Newcastle zote zinataka kumsajili mshambuliaji wa Benfica Goncalo Ramos, 21, wa Ureno. (Telegraph - subscription required)
Kiungo wa kati wa Liverpool na Guinea Naby Keita, 27, anaweza kuwa tayari kuondoka, huku klabu ya zamani ya RB Leipzig ikionyesha nia. (Sky Sports Germany)
Lakini inafahamika kuwa Liverpool hawana nia ya kumwachia Keita kabla ya mwisho wa dirisha hili la usajili na wanatumai kumfanya asaini kandarasi mpya, ingawa wanaweza kuhatarisha kumwacha huru msimu ujao. (Goal)
West Ham wameachana na nia yao ya kumnunua beki wa kushoto wa Chelsea Emerson, 28, kutokana na madai ya mshahara mkubwa wa Mbrazil huyo. (Guardian)