Kitu gani kilifanyika wakati wa hafla ya kumtangaza Charles III mfalme

g

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, MfalmeCharles III na Camilla, Malkia Consort wakati wa sherehe za kihistoria za kumtangaza mfalme, Jumamosi hii

Mfalme mpya ametangazwa rasmi na baraza maalum Jumamosi, katika hafla ambayo haijawasi kushuhudiwa kwa Zaidi ya miaka 70.Kuanzia nderemo mpaka hotuba na viapo vya kina na heshima walizotoa wapiga tarumbeta, hiki ndicho kilichofanyika katika kasri la St James.

Charles III ametangazwa rasmi mfalme katika hafla ya kihistoria kwenye kasri la St James mjini London.

Wakati wa hafla hiyo Jumamosi asubuhi iliopeperushwa rasmi kwenye televisheni kwa mara ya kwanza -, bendera ambazo zilikuwa zikipepea nusu mlingoti katika kumuomboleza Malkia zilikweza juu kikamilifu katika kumsherehekea mfalme mpya.

Matangazo mengine yatafanyika kote Uingereza mpaka Jumapili wakati bendera zitarudi kupeea nusu mlingoti katika kipindi cha maombolezi kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II mnamo Septemba 8.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kumshangilia Mfalme

Tangazo lenyewe ni nini?

Charles tayari alikuwa ni mfalme - kwa mujibu wa sheria ya bunge 1701 – punde tu mamakee alipofariki. Kwahivyo jukumu la baraza hilo maalum ni la heshima tu kutangaza rasmi jina la Mfalme mpya.

Kwa kawaida hili hufanyika katika saa 24 za kifo cha Malkia. Lakini mara hii muda wa ziada umepita kuanzia kifo cha Malkia Elizabeth II na hafla hiyo katika kasri la St James katikati ya London na karibu na kasri la Buckingham.

Katika utaratibu ambao haukuzoeleka, Mfalme Charles akaamua kwamba kikao hicho cha baraza kumtangaza rasmi Mfalme kitapeperushwa kwenye televisheni.

Ni nani aliyehudhuria?

Wanachama Zaidi ya 200 wa baraza kuu – taasisi inayojumuisha washauri kwa ufalme, wengi wakiwani wanasiasa wa zamani n awa hivi sasa – walikusanyika katika kasri la St James pamoja na viongozi wa kidini.

Baraza hilo liliidhinishwa tangu enzi za wafalme wa Norman. Huku likiwa na wanachama 70, ila ni 200 tu waliokusanyika.

Mawaziri wakuu wa zamani Gordon Brown, David Cameron, Boris Johnson na Theresa May – waliokutana na Malkia katika nyakati nyingi katika miaka mingi – wote walihudhuria, pamoja na Meya wa mji wa London, majaji wakuu na maafisa wengine.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongozi wa labour Sir Keir Starmer na mawaziri wakuu wa zamani Tony Blair, Gordon Brown, Boris Johnson, David Cameron, Theresa May na John Major walihudhuria
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 Camilla Parker Bowles, mkewe Charles waliooana kwa miaka 17 mpaka sasa (ambaye sasa ana wadhifa wa Malkia, mkewe mfalme) na mwanawe mfalme, William, ambaye sasa ni Mwanamfalme mpya wa Wales, pia walikuweko.

Awamu ya kwanza: mfalme atajwa

Baraza limegawanyika mara mbili, Charles alikuwepo kwenye awamu ya pili ya kikao cha baraza hilo.

Katika awamu ya kwanza, rais wa baraza hilo – mbunge wa Conservative Penny Mordaunt, aliyeteuliwa na Waziri mkuu Liz Truss mnamo Septemba 6 – alitangaza kifo cha Malkia.

Baada yah apo alimuomba karani wa baraza asome tangazo rasmi la Mfalme lililojumuisha wadhifa mpya wa Charles, Mfalme Charles III.

Takriban watu 200 waliokusanyika katika ukumbi huo walitamka 'God save the King' yaani Mungu mlinde mfalme kabla ya nyaraka kutiwa Saini.

Mwanamfalme William, Waziri mkuu Liz Truss askofu mkuu Justin Welby walifuatilia kwa kutazama.

Tangazo hilo baadaye lilitiwa saini na familia ya kifalme, Waziri mkuu, askofu mkuu wa Canterbury, kiongozi mkuu bungeni, msimamizi mkuu katika ofisi ya ufalme au Earl Marshall - Duke wa Norfolk – anayesimamia hafla za serikali.

Baada ya utiaji saini, Mordaunt aliomba watu wanyamae kimya alafu akasoma shughuli nyingine zilizosalia, ikiwemo utoaji wa heshima kwa ufeytuaji wa bunduki katika bustani ya Hyde katikati ya London na katika jumba refu maarufu London Tower.

Sehemu ya pili: Mfalme anazungumza

Sehemu ya pili ya baraza hilo ni wakati wanachama wa baraza hilo walipomsalimia mfalme kwenye chumba chenye kiti cha enzi katika kasri la St James.

Ulikuwa mkutano wa kwanza wa baraza hilo uliofanywa na Mfalme mpya.

Getty

Chanzo cha picha, PA Media

Sehemu ya pili ya baraza hilo ni wakati wanachama wa baraza hilo walipomsalimia mfalme kwenye chumba chenye kiti cha enzi katika kasri la St James.

Ulikuwa mkutano wa kwanza wa baraza hilo uliofanywa na Mfalme mpya.

Wanachama walisimama kwenye mstari na kumkaribisha , kila mtu huwa amesimama kwa mujibu wa utamaduni wa baraza hilo.

 Katika hotuba ya kwanza iliyojaa huzuni Mfalme huyo alizungumza kuhusu "huduma aliyojitolea maishani mamake" na kuahidi kufuata nyayo zake.

"Dunia nzima imehuzunika pamoja nami kwa kuondokewa huku.

 "Utawala wa mamangu haikuwa na mithili katika muda wake, uwajibikaji na kujitolea kwake. Hata tunapomuomboleza tunatoa shukrani kwa Maisha haya ya kuaminika."

P

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Wanajeshi walishiriki katika kufyatua mizinga kwa heshima ya Mfalme Charles III
P

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Heshima ya mizinga ilifanyika kote London na maeneo mengine ya nchi
P

Chanzo cha picha, PA Media

Sehemu ya pili ya baraza hilo ni wakati wanachama wa baraza hilo walipomsalimia mfalme kwenye chumba chenye kiti cha enzi katika kasri la St James.

Ulikuwa mkutano wa kwanza wa baraza hilo uliofanywa na Mfalme mpya.

Katika hotuba ya kwanza iliyojaa huzuni Mfalme huyo alizungumza kuhusu "huduma aliyojitolea maishani mamake" na kuahidi kufuata nyayo zake.

"Dunia nzima imehuzunika pamoja nami kwa kuondokewa huku.

"Utawala wa mamangu haikuwa na mithili katika muda wake, uwajibikaji na kujitolea kwake. Hata tunapomuomboleza tunatoa shukrani kwa Maisha haya ya kuaminika."

Mfalme aliendelea kuzungumza kuhusu majukumu yake.

"Ninafahamu kwa undani kuhusu urathi hu una majukumu makubwa na wajibu niliokabidhiwa sasa."

 Alitoa pia heshima zake kwa Camilla, Malkia – mkewe mfalme. "Ninatiwa moyo sana kwa usaidizi wa mke wangu mpendwa," alisema.

Nini kinachofuata?

Mfalme Charles alikula kiapo kipi?

Kwa mujibu wa sheria, Mfalme mpya anapaswa kula kiapo kuendeleza na kuhifadhi kanisa la Uskochi.

 Hii ni kwasababu huko Uskochi kuna mgawanyiko wa uongozi kati ya kanisa na serikali.

Charles alitia saini nakala mbili za nyaraka mbele ya baraza hilo. Mashahidi pia walisaini kiapo hicho akiwemo mwanamfalme Willian – ambaye ni Mwanamflame mpya wa Wales – akifuatwa na Camila, mkewe mfalme.

Getty

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, mwanamfalme william na Mke wake Catherine wameitwa Mwanamfalme mpya na Bintimfalme wa Wales , huku Camilla akiwa sasa ni Malkia Consort

Kwa mujibu wa sheria, Mfalme mpya anapaswa kula kiapo kuendeleza na kuhifadhi kanisa la Uskochi.

 Hii ni kwasababu huko Uskochi kuna mgawanyiko wa uongozi kati ya kanisa na serikali.

Charles alitia saini nakala mbili za nyaraka mbele ya baraza hilo. Mashahidi pia walisaini kiapo hicho akiwemo mwanamfalme Willian – ambaye ni Mwanamflame mpya wa Wales – akifuatwa na Camila, mkewe mfalme.

 Wakati mashahidi wa mwisho walipokuwa wakisaini tangazo hilo, bendi ilianza kucheza.

Charles angeweza kukataa kula viapo alivyotakiwa kula, hatahivyo mara ya mwisho Mfalme kukytaa kula kiapo ilikuwa ni mnamo 1910 wakati Mfalme George V alikata maneno yasiokuwa ya kikatoliki kwenye kiapo hicho.

Kitu gani kilifanyika kwenye roshani? Shughuli baada ya hapo ilisongea nje ya kasri. Wananchi waliruhusiwa kuingia katika sehemu ya kasri hilo ijulikanayo kama Friary Court ambapo walishuhudia hafla hiyo ya kutangazwa Mfalme Charles III.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kutangazwakwa Mfalme Charles II wa Uingereza kulisomwa katika roshani ya Mahakama ya Friary

Mjumbe alikwenda kwenye roshani juu ya sehemu walikokuwa wananchi na kulisoma tangazo na wapiga tarumbeta wakatoa heshima kwa mfalme.

Wimbo wa taifa ulipigwa huku maneno "God Save the King" yakijumuishwa kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miongo saba. Kisha mbwembwe za pamoja zilifuata na Mfalme akapewa heshima zake kwa nderemo.

Wapiga tarumbeta na wajumbe wakafuatana kwa msururu wa magari. Wakelekea katika jengo la the Royal Exchange mjini London, ambapo tangazo jingine limetolewa.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tarumbeta za kitaifa katika eneo la roshani juu ya Mahakama ya Friary
G
Maelezo ya picha, Sherehe za kutangazwa kwa Mfalme katika Royal Exchange -za pili na za mwisho za aina yake zimefanyika london Jumamosi hii

Kisha mbwembwe za pamoja zilifuata na Mfalme akapewa heshima zake kwa nderemo.

Wapiga tarumbeta na wajumbe wakafuatana kwa msururu wa magari. Wakelekea katika jengo la the Royal Exchange mjini London, ambapo tangazo jingine limetolewa.

Nini kinachofuata?

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lord Rais wa baraza la Privy (kwa sasa Mbunge wa Penny Mordaunt ) aliongoza sherehe

Penny Mordaunt aliikamilisha hafla hiyo kwa kusoma rasimu ya maagizo ya tangazo lililopaswa kuidhinishwa, huku Mfalme Charles III akiidhinisha moja baada ya nyingine. Mojawapo lilikuwa ni la siku ya kuzikwa Malkia kufanywa siku kuu. Lakini huenda ikachukua muda kabla ya sherehe ya Charles kutawazwa ikafanyika. Miezi 16 ilipita kutoka babake Mlakia Elizabeth, Mfalme George VI, alipofariki Februari 1952 ahadi alipotawazwa mnamo Juni 1953.