Ufahamu 'udhaifu' katika mwili wako unaokosolewa na wanasayansi

Human

Chanzo cha picha, Getty Images

Sigmund Freud alitaja uwepo wa nadharia mbili za kisayansi zilizoathiri sana saikolojia ya binadamu: Ya kwanza, ni kwamba dunia si kitovu cha ulimwengu.

Pili, ingawa dunia iliundwa angalau miaka bilioni 4.5 iliyopita, wanadamu wamekuwa wakiishi kwenye sayari hii kwa muda mfupi sana.

Kabla yake, kulikuwa na kila kitu duniani isipokuwa binadamu.

Na jambo la kushangaza ambalo linahitaji kuongezwa ni kwamba sisi binadamu sio wakamilifu, hatujakamilika tuna mapungufu makubwa. Hii inamaanisha kwamba muundo wa kimwili au muundo wa binadamu.

Wanasayansi wameona katika tafiti mbalimbali, baada ya mageuzi mengi, 'kasoro' kadhaa zilizobakia katika mwili wa mwanadamu.

Na hizi ni baadhi ya kasoro hizo kati ya nyingi.

Mfumo wa uzazi wa mwanaume

human

Chanzo cha picha, Getty Images

Mfano wa kwanza wa jinsi mwili wa mwanadamu alivyo na kasoro kisayansi ni kwenye mfumo wa uzazi wa kiume.

Ingekuwa bora kama kiungo hiki kingelindwa kama mapafu au moyo, ksingekuwa wazi, kingefichwa na kinaonekana wakati wa kujamiana tu.

Tatizo ni kwamba mbegu za kiume, haziwezi kukua vizuri kwa joto la kawaida la mwili, yaani nyuzi joto 36.5.

Wanyama wengine, hasa wale ambao hawana damu joto, kama vile vyura, viungo vyao vya uzazi vya kiume vinalindwa vyema kwa ndani.

Hata wanyama wengine wenye damu joto, kama vile tembo, wana viungo vya uzazi ambavyo ni salama kabisa.

Uti wa mgongo na maumivu yake

Human

Chanzo cha picha, Getty Images

Bila shaka mfano mwingine wa jinsi mwili wa mwanadamu ulivyo na kasoro kisayansi ni 'mgongo'.

Je, huwezi kupata mtu ambaye hajawahi kukutana tatizo au kuumwa mgongo katika maisha yake.

Mifupa ya mgongo hukaa kando kando ili kuunda upinde unaoshikilia vyema muundo wote wa mwili wa mnyama pamoja akiwemo binadamu.

Lakini kwa kuwa binadamu ni aina ya mnyama mwenye miguu miwili, pingili za mgongo zimepangwa kihalisi katika safu za 'longitudinal'.

Kutokana na aina hii ya mpangilio, vingili katika sehemu ya chini ya mwili 'vertebrae' inapaswa kubeba uzito zaidi.

Ndio maana tatizo la maumivu ya kiuno na mgongo kwa binadamu ni la kawaida sana.

Upofu wa macho

Jicho la mwanadamu pia ni mfano wa udhaifu wa mwili wa mwanadamu.

Retina ya binadamu imefunikwa. Kazi ya retina ni kunasa au kupokea taarifa nyepesi na kutuma taarifa hizo kwenye ubongo wetu kupitia mshipa wa macho.

Shida ni kwamba hakuna vipokezi vya picha katika hatua ambapo neva ya macho huvuka retina, hii inamaanisha kuwa tuna 'sehemu isiyoonekana' au 'upofu' katika kila jicho.

Wanyama wengine hawana madoa machoni kama sisi, kwa mfano Pweza.

Katika macho ya pweza, nyuzinyuzi za macho ziko nyuma ya retina, hivyo neva ya macho haihitajiki kupeleka taarifa nyepesi kwenye ubongo.

Kwa sababu hii, hakuna doa achoni pa pweza kama ilivyo kwa binadamu.

pweza

Chanzo cha picha, Getty Images

Koo na kukohoa

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ukosefu wa hewa ni sababu kuu ya kifo kisicho cha kawaida katika spishi za wanyama zenye afya.

Mwaka jana, idadi ya watu waliokufa kutokana na kukosa hewa ilikuwa mara mbili zaidi ya idadi ya watu waliokufa kwa ajali za gari huko nchini Hispania.

Mirija ambayo hubeba chakula na hewa katika miili yetu imeunganishwa kwa namna hatari katika sehemu kadhaa za mwili.

Pharynx ni kiungo muhimu sana. Pharynx ni kama bomba ambalo huanzia puani kwa ndani kwenda chini ya shingo na koo.

Kwa kawaida, maji na chakula vinakwenda kwenye kitu kinaitwa esophagus wakati hewa inakwenda ama kupitia kwenye trachea.

Lakini kuna wakati mwingine mambo yanaweza kwenda vibaya katika mfumo huu.

Ikiwa hata kiasi kidogo cha chakula kinaingia kwenye trachea kwa bahati mbaya wakati wa kula, inaweza kusababisha madhara makubwa kama vile kifo kwa kukosa hewa.

Na hii inathibitisha kwa mfano binadamu hawezi kula zabibu kwa haraka kwa sababu mwili wake haujaundwa vizuri kisayansi.

human

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna mbinu za kusaidia kumuweka mtu sawa ambaye amepaliwa na kukohoa

Muhimu: Kisayansi yapo mapungufu mengi ya kimwili na kimfumo ambayo hayaingiliani na kiimani. Na kwa mantiki hii, makala haya hayana sababu ya kukosoa uumbaji, kutokana na imani za wanadamu, bali kuonyesha dhana ya kisayansi katika mwili wa mwanadamu.