Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Man City kufungua ligi ya Premia dhidi ya Chelsea msimu wa 2024/25
Manchester City wataanza kwa kuwa wageni wa Chelsea katika wiki ya kwanza ya msimu wa 2024/25 wa ligi kuu ya premia nchini England
Kwa upande wa Ipswich Town, ambayo ni miongoni mwa timu tatu mpya zinazojiunga na ligi ligi hiyo wataanza kwa kuwakaribisha Liverpool.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ipswich kucheza Ligi ya Premia baada ya miaka 22, ikitarajiwa kushuka uwanjani mnamo Agosti 17, 2024.
Lakini msimu huo utaanza na ufunguzi wa pazia la shindano hilo kwa mechi kati ya Manchester United na Fulham katika uwanja wa Old Trafford mnamo Ijumaa, Agosti 16.
Arsenal, waliomaliza katika nafasi ya pili kwenye ligi, watawakaribisha Wolverhampton katika uwanja wa Emirates siku ya Jumamosi, huku Aston Villa wakisafiri kuelekea West Ham.
Southampton, ambao walirejea kucheza Ligi ya Premia, baada ya msimu mmoja kwenye ligi ya Championship, watamenyana na Newcastle katika uwanja wa St James' Park.
Everton watakuwa wenyeji wa Brighton huku Nottingham Forest na Bournemouth zikuchuana siku ya Jumamosi.
Mechi zitakazochezwa Jumapili ya wiki ya kwanza ni pamoja na ile ya Brentford na Crystal Palace na mshindi wa ligi ya Championship , Leicester City ambao watakuwa wenyeji wa Tottenham Jumatatu ya Agosti 19.
Mara ya mwisho kwa Ipswich kushiriki ligi ya Premia ilichapwa mabao 5-0 na Liverpool kwenye uwanja wa Anfield siku ya mwisho ya msimu wa 2001/02.
Mwezi Mei mwaka huu, Manchester City ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya nne mfululizo, baada ya kumaliza msimu uliopita ikiwa na pengo la pointi mbili kati yake na Arsenal waliokuwa wa pili katika jedwali.
Mechi za Ligi Kuu wiki ya kwanza
- Ijumaa tarehe 16 Agosti
- Manchester United vs Fulham
Jumamosi ya 17 mwezi Agosti
- Ipswich Town vs Liverpool
- Arsenal vs Wolverhampton
- Everton vs Brighton
- Newcastle United vs Southampton
- Nottingham Forest vs Bournemouth
- West Ham United vs Aston Villa
Jumapili ya 18 mwezi Agosti
- Brentford vs Crystal Palace
- Chelsea vs Manchester City
Jumatatu ya 19 mwezi Agosti
Leicester City and Tottenham
Baadhi ya masuala muhimu yanayohusiana na Ligi Kuu 2024/25
Manchester City itacheza michezo miwili kati ya saba kabla ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo itacheza mechi tatu katika viwanja vya Etihad, Aston Villa, Arsenal na Liverpool.
Mechi ya mbali zaidi kuchezwa itakuwa umbali wa maili 200 mnamo Desemba 26 wakati Arsenal watakapoitembelea Newcastle United katika uwanja wa St James Park.
Wiki ya mwisho ya kuwania Kombe la FA ni Jumamosi, Mei 17, siku hiyo haitaongezwa kwenye mechi za Ligi Kuu.
Wiki ya tatu ya msimu huu, Aston Villa watakuwa wageni dhidi ya Tottenham, huku Liverpool wakiwakaribisha Chelsea kwenye uwanja wa Anfield.
Wiki ya nne, Manchester City itaenda nyumbani kwa Tottenham na kisha kumenyana na Liverpool.
Manchester United watakuwa wenyeji wa Liverpool kabla ya mapumziko ya kalenda ya Fifa mwezi Septemba, huku Arsenal wakiitembelea Tottenham mwishoni mwa mapumziko.
Everton watacheza mechi yao ya mwisho katika uwanja wa Goodison Park - kisha kuhamia Bramley-Moore Dock - kabla ya kumenyana na Southampton Jumapili ya tarehe 18 Mei ikiwa ni wiki moja kabla ya fainali ya Kombe la FA.
Je, Ligi Kuu 2024/25 itaanza lini?
Msimu wa Ligi Kuu wa 2024-25 utaanza Ijumaa tarehe 16 Agosti na kumalizika Jumapili Mei 25, 2025 ambapo mechi 10 zitachezwa siku moja kwa wakati mmoja.
Kutakuwa na likizo itakayotolewa na Fifa mnamo mwezi Septemba, Novemba na Machi, wakati raundi ya tatu ya Kombe la FA ikichezwa wiki ya Januari.
Ili kupata mechi katikati ya Agosti, hakuna mapumziko ya msimu wa baridi, na vilevile hakutakuwa na marudio ya mechi siku moja kabla ya Krismasi kama ilivyofanyika msimu uliopita kati ya Wolves na Chelsea, kwa mara ya kwanza tangu 1995.
Timu zitakazocheza Ligi Kuu zimefahamishwa kuwa hakuna hata moja kati yao itakayocheza michezo miwili mfululizo kwa chini ya saa 60 kati ya siku kuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Timu tatu zilizoingia Ligi Kuu na tatu zilizoaga ligi hiyo.
Timu tatu zilizopanda Ligi Kuu ni pamoja na Leicester City, iliyotwaa Ubingwa na Ipswich, ya pili.
Ya tatu ni Southampton, ambao walishinda dhidi ya Leeds United kwenye mechi ya kujaza nafasi hiyo.
Walioaga ligi ya premia msimu uliopita ni Luton Town, Burnley na Sheffield United.