Mwaka mpya 2024: Zijue nchi za kwanza kuukaribisha mwaka mpya

de

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Mji wa Auckland nchini New Zealand ni mojawapo ya miji ya kwanza duniani kukaribisha Mwaka Mpya 2024

Nyakati za kukaribisha Mwaka Mpya hutofautiana ulimwenguni kulingana na muda wa eneo husika. Nchi au eneo la kwanza kupokea mwaka mpya hupishana na nchi ya mwisho kwa saa 26.

Eneo la Kiribati huko Oceania limekuwa la kwanza Duniani kushuhudia kuzaliwa kwa Mwaka Mpya 2024, likifuatiwa na New Zealand, Tonga, Samoa, na Australia.

Kisha zinafuata nchi za Japan, Korea Kusini, Korea Kaskazini, East Timor na Palau - zote ziliingia mwaka mpya saa 15:00 GMT.

Jiji la Auckland nchini New Zealand liliukaribisha mwaka 2024, na kuwa jiji la kwanza duniani kushuhudia kuzaliwa kwa saa za kwanza za mwaka mpya. Kumefanyika maonyesho ya kila mwaka ya fataki katika mnara maarufu wa Sky Tower.

Visiwa viwili vikuu vya New Zealand - Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini - viko katika wakati mmoja, wakati Visiwa vya Chatham viko katika eneo tofauti la saa kwa dakika 45 mbele.

O

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Sydney, sherehe za Australia kukaribisha Mwaka Mpya 2024

Maonyesho hayo makubwa ya fataki yalimulika Daraja la Bandari ya Sydney, Jumba la Opera na anga nzima ya jiji na sauti za shangwe kutoka kwa watazamaji.

Umati wa watu ulianza kukusanyika kuanzia asubuhi mapema kwa matumaini ya kupata mahali pazuri pa kutazama hafla hiyo. Maeneo mengi yaliripotiwa kujaa kufikia saa moja jioni (19:00) saa za ndani.

Jiji la Sydney lilitumia takribani tani 8.5 za fataki ambazo ziliigeuza anga ya Daraja la Bandari na Jumba la Opera kama mchana kwa rangi tofauti, zilizo maarufu zaidi zikiwa nyekundu na njano.

Onyesho la fataki lilichukua muda wa miezi 15 kulipanga na lilidumu dakika 12.

XS

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Wachina waliukaribisha Mwaka Mpya kwa njia yao ya kitamaduni na gwaride lililobeba vinyago vya dragoni

Maelfu ya watu walijipanga huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning wa China, kutazama gwaride la Mwaka Mpya, vinyago na dragoni na ngoma za dragoni – zilirindima mapema 2024. Sherehe hizo zinaambatana na likizo ya siku tatu ya Mwaka Mpya kuanzia tarehe 31 Desemba 2023.

Ingawa Urusi iko katika bara la Ulaya, ni moja ya nchi za kwanza ulimwenguni kukaribisha Mwaka Mpya 2024, kwani saa za kwanza za mwaka zinaanza Mashariki ya Mbali ya Urusi.

D

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Urusi ni moja ya nchi za kwanza kukaribisha Mwaka Mpya 2024

Mji mkuu wa Urusi, Moscow, ulipambwa kwa taa kukaribisha Mwaka Mpya.

India pia ni mojawapo ya nchi zinazokaribisha Mwaka Mpya mapema, na Wahindi huukaribisha Mwaka Mpya kwa njia tofauti - baadhi ni za jadi na za kihistoria, na nyingine ni njia za kisasa na za ubunifu.

CDFV

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Santa Claus kinyozi akichora nambari 2024 kichwani mwa mteja nchini India ili kusherehekea Mwaka Mpya

Katika picha hii, kinyozi alivaa mavazi ya Santa Claus, akimnyoa mmoja wa wateja kwa kuchora nambari 2024 kichwani mwake, kusherehekea kuwasili kwa mwaka mpya.

Q

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Indonesia ni miongoni mwa nchi zinazoadhimisha Mwaka Mpya 2024 mapema

Waindonesia waliukaribisha Mwaka Mpya kwa maonyesho ya kupendeza ya fataki katika mji mkuu, Jakarta, watu wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ya nchi hiyo, kama moja ya mila ya kihistoria .

Kuwepo kwa Indonesia katika bara la Asia kunaifanya kuwa mojawapo ya nchi za kwanza kukaribisha Mwaka Mpya pia.

S

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Watu wa Japani wanakaribisha Mwaka Mpya wakiwa na bendera za Japan mitaani

Watembea kwa miguu hutembea kando ya barabara tulivu za Ginza katikati ya mji wa Tokyo, wakielekea kwenye viwanja mbalimbali vya sherehe, ambapo bendera za Kijapani zilipandishwa katika mitaa yote na vitongoji vyote, huku taa zikisambazwa kwa ajili ya maandalizi ya kukaribisha saa za kwanza za Mwaka 2024.

SD

Chanzo cha picha, GETTY IMAGE

Maelezo ya picha, Korea Kusini iliukaribisha mwaka mpya 2024 mapema pia

Korea Kusini ni nchi ya tano duniani kukaribisha Mwaka Mpya kwa sababu iko sehemu ya mbali kabisa ya Asia Mashariki. Kumefanyika sherehe kubwa na za kustaajabisha kote nchini humo na mapambo yakitundikwa mitaani.

Watu huvaa vinyago kabla Mwaka Mpya kuanza katikati mwa Seoul. Wengine hutembea katika msafara kama wa sherehe ya Tamu Losar, sherehe ya Mwaka Mpya inayoadhimishwa na jamii ya Gurung huko Kathmandu, Nepal.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Esther Namuhisa