Vladimir Putin akiwa na umri wa miaka 70: Nyakati saba muhimu zilizomjenga

Huku Rais Vladmir Putin akikaribia kusherehekea mwaka wake wa 70 tangu azaliwe, ilikuwaje akawa kiongozi wa pekee aliyetekeleza uvamizi mbaya nchini Ukraine? Nyakati saba muhimu katika Maisha yake

Nyakati saba muhimu katika maisha yake zilisaidia kuunda fikra zake na kuelezea ufarakano wake alionao na nchi za Magharibi.

Kujiunga na mchezo wa Judo, 1964

Akiwa Mzaliwa wa Leningrad ambayo bado ilikuwa na kovu kwa kuzingirwa kwake kwa siku 872 katika Vita vya pili vya dunia, Vladimir akiwa kijana mdogo alikuwa mvulana asiyesikia na mgomvi shuleni - rafiki yake wa karibu alikumbuka kwamba "angeweza kupigana na mtu yeyote" kwa sababu "hakuwa na woga" .

hatahivyo, akiwa mvulana mdogo katika jiji lililojaa magenge ya uhalifu alihitaji kuwa mkali, na akiwa na umri wa miaka 12 alijiunga na mchezo wa sambo - sanaa ya kijeshi ya Urusi, na kisha judo. Alikuwa ana dhamira na mwenye nidhamu, na alipokuwa na umri wa miaka 18 alikuwa na mkanda mweusi wa judo na nakushika nafasi ya tatu katika mashindano ya kitaifa ya vijana.

Kwa kweli, hii imetumika kama sehemu yake binafsi , lakini pia ilithibitisha imani yake mapema kwamba katika ulimwengu hatari, unahitaji kujiamini lakini pia utambue kwamba, kwa maneno yake mwenyewe, wakati kuna pigano lisiloepukika, "lazima uanze kupiga wa kwanza, na upige sana ili mpinzani wako asiweze kujibu shambulio hilo".

Alijiunga na shirika la Ujasusi la KGB 198

Kwa ujumla, watu waliepuka kwenda 4 Liteyny Prospekt, Makao Makuu ya KGB huko Leningrad. Wengi walikuwa wamepitia seli zake za kuhojiwa hadi kwenye kambi za kazi za gulag katika enzi ya Stalin hivi kwamba utani mkali ulikuwa kwamba ile inayoitwa Bolshoi Dom, "Nyumba Kubwa", lilikuwa jengo refu zaidi huko Leningrad, kwa sababu mtu angeweza kuona Siberia kutoka kwa ghorofa yake ya chini.

Hata hivyo, alipokuwa na umri wa miaka 16, Putin aliingia kwenye mapokezi ya ofisi ya KGB yenye zulia jekundu na kumuuliza afisa aliyekuwa nyuma ya dawati jinsi angeweza kujiunga. Aliambiwa kwamba alihitaji kuwa amemaliza utumishi wa kijeshi au shahada, na hata alikuwa na ujasiri kuuliza ni shahada gani ilikuwa bora zaidi.

Sheria, aliambiwa - na kutokana na hatua hiyo, Putin alikuwa amedhamiria kuhitimu sheria, baada ya hapo aliajiriwa ipasavyo. Kwa Putin, KGB lilikuwa genge kubwa zaidi mjini, likitoa usalama na maendeleo hata kwa mtu asiye na uhusiano wa Chama.

Lakini pia iliwakilisha nafasi ya kuwa mtu muhimu -kama alivyosema mwenyewe kuhusu filamu za kijasusi alizotazama akiwa kijana, "jasusi mmoja angeweza kuamua hatima ya maelfu ya watu".

Azungukwa na genge la watu , 1989

Kwa matumaini yake yote, kazi ya Putin ya KGB haikuanza kama alivyodhani. Alikuwa mfanyakazi dhabiti, lakini hakufanikiwa sana. Hata hivyo, alikuwa amejitolea kujifunza Kijerumani, na hilo lilimfanya apate miadi ya kujiunga na ofisi za mawasiliano za KGB huko Dresden mwaka wa 1985.

Huko alijikita katika maisha ya starehe ya ugenini, lakini mnamo Novemba 1989, utawala wa Ujerumani Mashariki ulianza kuporomoka, kwa kasi ya kushangaza.

Mnamo tarehe 5 Desemba, kundi la watu lilizingira jengo la KGB la Dresden. Putin alipiga simu kwa n Jeshi lililokuwepo karibu ili kuomba ulinzi, na walijibu bila msaada "hatuwezi kufanya chochote bila amri kutoka Moscow. Na Moscow iko kimya."

Putin alijifunza kuogopa kuanguka ghafla kwa mamlaka kuu - na akaamua kutorudia tena kile alichohisi kuwa ni kosa la kiongozi wa Usovieti Mikhail Gorbachev, kutojibu kwa kasi na azma anapokabiliwa na upinzani.

Kuanzisha programu ya kubadilishana mafuta kwa chakula 1992

Baadaye Putin angeondoka KGB wakati Umoja wa Kisovieti ulipokuwa umefungwa, lakini hivi karibuni alipata kazi huko kwa Meya wa St Petersburg. Uchumi ulikuwa katika hali duni, na Putin alishtakiwa kwa kusimamia mpango wa kujaribu kusaidia watu wa jiji hilo kujikwamua, akibadilisha mafuta ya thamani ya $100m (£88m) na chuma kwa chakula.

Hakuna mtu aliyeona chakula chochote, lakini kulingana na uchunguzi, Putin, marafiki zake na majambazi waliiba pesa jiji hilo.

Katika "miaka ya 90 ", Putin alijifunza haraka kuwa ushawishi wa kisiasa ulikuwa bidhaa inayoweza kulipwa, na majambazi wanaweza kuwa washirika muhimu. Wakati kila mtu karibu naye alikuwa akinufaika na nafasi zao, kwanini yeye asifaidi?

Uvamizi wa Georgia 2008

Wakati Putin alipokuwa rais wa Urusi mwaka 2000, alitarajia kuwa na uwezo wa kujenga uhusiano mzuri na nchi za Magharibi - kwa masharti yake mwenyewe, ikiwa ni pamoja na nyanja ya ushawishi katika Umoja wa zamani wa Soviet Union. Hivi karibuni alikatishwa tamaa, kisha akakasirika, akiamini Magharibi ilikuwa ikijaribu kuitenganisha na kuidhalilisha Urusi.

Wakati rais wa Georgia Mikheil Saakashvili alipojitolea nchi yake kujiunga na Nato, Putin aliona hatari na jaribio la Georgia kurejesha udhibiti wa eneo lililojitenga la Ossetia Kusini linaloungwa mkono na Urusi likawa kisingizio cha operesheni ya adhabu.

Katika siku tano, vikosi vya Urusi vilisambaratisha jeshi la Georgia na kulazimisha amani huko Saakashvili.

Nchi za Magharibi zilikasirishwa, lakini ndani ya mwaka mmoja, rais wa Marekani Barack Obama alikuwa akijitolea "kuweka upya" uhusiano na Urusi, na Moscow hata ikapewa haki ya kuandaa Kombe la Dunia la kandanda la 2018.

Kwa Putin, ilikuwa wazi kwamba hilo lingeweza kusahihishwa - na Magharibi ilio dhaifu na isiyo na nguvu ingeweza kulalama, lakini hatimaye kurudi chini katika uso wa nia iliyodhamiriwa.

Maandamano ya Moscow 2011 -13

Imani iliyoenea - na ya kuaminika - kwamba uchaguzi wa bunge wa 2011 uliibiwa ilizusha maandamano ambayo yalichochewa tu wakati Putin alitangaza kuwa atatetea tena wadhfa wake mwaka wa 2012.

Yanayojulikana kama "Maandamano ya Bolotnaya" baada ya bustani ya Moscow kujaa , hii iliwakilisha usemi mkubwa zaidi wa upinzani wa umma chini ya Putin.

Aliamini kwamba mikutano hiyo ilianzishwa, ilihimizwa na kuongozwa na Washington, akimlaumu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton binafsi.

Kwa Putin, ilikuwa ni ushahidi kwamba vita vimeanza , na Magharibi ilikuwa ikimjia moja kwa moja, na kwamba, kwa kweli, sasa alikuwa vitani.

Kujitenga wakati wa Corona 2020-01

Wakati Covid-19 ilipoenea kote ulimwenguni, Putin aliingia katika hali ya kutengwa isiyo ya kawaida hata kwa watawala wake wa kibinafsi, na mtu yeyote aliyetaka kukutana naye alitengwa kwa wiki mbili chini ya ulinzi na kisha kupita kwenye ukanda uliowekwa kwenye mwanga wa kuua wadudu na ukungu ili kuua viini.

Kwa wakati huu, idadi ya washirika na washauri walioweza kuwa na wakati na Putin ilipungua sana hadi kwa watu wachache na wandani wake.

Akiwa pekee , Putin alijifunza kwamba mawazo yake yote yalikuwa sawa na chuki zake zote zilihesabika na hapo ndiposa mbegu za uvamizi wa Ukraine zilipandwa.