Maelfu wajitolea kupiga picha za utupu ili kuongeza ufahamu wa saratani

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu wapatao 2,500 wamejitolea kupiga picha za utupu wakati jua lilipochomoza mapema asubuhi kwenye ufukwe wa Bond mjini Sydney Australia kwa ajili ya kazi ya Sanaa iliyoandaliwa ili kuongeza ufahamu wa saratani ya ngozi .
Shughuli hiyo imeandaliwa na ya hivi karibuni ya mradi wa mpigapicha Mmarekani Spencer, inayolenga kuwatia moyo Waastralia kupimwa mara kwa mara saratani ya ngozi.
Sheria ilibadilishwa ili kuruhusu watu kuwa watupu mahala pa umma kwenye fukwe kwa mara ya kwanza.
Australia ni nchi inayoathiriwa na saratani ya ngozi zaidi duniani, Mfuko wa utafiti wa dunia wa saratani unasema.

Chanzo cha picha, EPA

Chanzo cha picha, EPA
Kuanzia saa tis ana nusu alfajiri, maelfu ya watu waliojitolea kuandaa kazi hiyo ya Sanaa walikusanyika kwenye ufukwe kushiriki shughuli hiyo, iliyofanyika kwa ushirikiano na shirika la msaada linalopipa saratani ya Ngozi -Skin Check Champions katika wiki ya saratani ya ngozi.
"Tuna fursa ya kutoa uelewa zaidi kuhusu uchunguzi wa ngozi na nimepewa heshima…kuja hapa, nitengeneze Sanaa yang una kusherehekea tu mwili na ulinzi wake ," alisema msanii maarufu Tunick katika nukuu ya Reuters.
Bruce Fisher, mwenye umri wa miaka 77, ambaye alishiriki katika tukio hilo , aliliambia shirika la habari la AFP: "Nusu ya maisha yangu nimeishi katika jua na uvimbe kadhaa wa saratani ya ngozi uliondolewa mgongoni mwangu.
"Nilidhani ilikuwa ni sababu nzuri na ninapenda kuvua nguo zangu kwenye ufukwe wa Bondi ."
Tunick anafahamika vyema kwa kutengeneza picha za watu wengi watupu katika baadhi ya maeneo asili maarufu zaidi duniani.















