"Ukraine ni taifa bandia lililoundwa na Stalin": Kauli 6 mashuhuri katika mahojiano ya Vladimir Putin na Tucker Carlson

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangu aanzishe uvamizi wake nchini Ukraine mnamo Februari 2022, Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa hajafanya mahojiano na waandishi wa habari wa Magharibi mpaka sasa.
Alhamisi wiki hii, Bw Putin alifanya mahojiano yasiyo ya kawaida na mwandishi wa habari wa Marekani mwenye utata Tucker Carlson ambayo yalitangazwa.
Carlson alifanya kipindi kilichotajwa kuwa chenye hadhi ya juu zaidi kwenye televisheni ya Fox News tangu mwezi Aprili 2023, wakati kampuni hiyo ilipomfuta kazi kazi bila maelezo. Leo, ana kampuni yake huru, Mtandao wa Tucker Carlson, na pia anatangaza kwenye X.
Hutangaza zaidi mahojiano ya kirafiki na wanasiasa wa mrengo wa kulia, akiwemo rais wa zamani Donald Trump.
Wakati wa mahojiano ya Alhamisi hii, Putin alihoji tabia ya kitaifa ya Ukraine na kuhalalisha "operesheni yake maalum ya kijeshi" dhidi ya Kiev kwa hoja zake zinazojulikana kuhusu tisho dhidi ya Urusi la upanuzi wa NATO.
Tangu aanzishe uvamizi wake nchini Ukraine mnamo Februari 2022, Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa hajafanya mahojiano na waandishi wa habari wa Magharibi mpaka sasa.
Alhamisi wiki hii, Bw Putin alifanya mahojiano yasiyo ya kawaida na mwandishi wa habari wa Marekani mwenye utata Tucker Carlson ambayo yalitangazwa.
Carlson alifanya kipindi kilichotajwa kuwa chenye hadhi ya juu zaidi kwenye televisheni ya Fox News tangu mwezi Aprili 2023, wakati kampuni hiyo ilipomfuta kazi kazi bila maelezo. Leo, ana kampuni yake huru, Mtandao wa Tucker Carlson, na pia anatangaza kwenye X.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hutangaza zaidi mahojiano ya kirafiki na wanasiasa wa mrengo wa kulia, akiwemo rais wa zamani Donald Trump.
Wakati wa mahojiano ya Alhamisi hii, Putin alihoji tabia ya kitaifa ya Ukraine na kuhalalisha "operesheni yake maalum ya kijeshi" dhidi ya Kiev kwa hoja zake zinazojulikana kuhusu tisho dhidi ya Urusi la upanuzi wa NATO.
Zaidi ya hayo, ametoa hakikisho kwamba hana nia ya kuivamia Poland au nchi nyingine yoyote ya NATO.
Mahojiano hayo yalitanguliwa na mabishano. Baadhi ya wachambuzi wanayatafsiri kama jaribio la Putin la kuwashawishi wapiga kura wa Marekani katika mwaka ambao wanamchagua tena rais wao.
Pia wanasema kwamba mahojiano hayo yanatokea wakati ambapo Bunge la Marekani linatatizika katika mazungumzo ya kuidhinisha fedha zaidi za kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine kutokana na kukataa kwa wabunge wa Republican walio karibu na Donald Trump kuendelezwa kwa ufadhili huo.
Rais huyo wa zamani amelalamikia msaada wa mabilioni ya dola ambayo Washington imetuma Ukraine na ameshauri kukomeshwa kwa mzozo huo.
Kulikuwa pia na utata kuhusu video ya matangazo iliyotolewa hapo awali na Carlson ambapo alisema kwamba "hakuna mwandishi wa habari wa Magharibi" ambaye amekuwa na nia ya kumhoji Putin tangu 2022 ili kusikiliza hoja zake.
Maoni yake yalizua ukosoaji kwani kuna idadi kubwa ya waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti vya habari ambao wanadai kuwa wameomba mara kwa mara mahojiano na rais wa Urusi ambayo hayakuwahi kutekelezwa. Miongoni mwa hawa ni Steve Rosenberg, mhariri wa BBC Russia.
Msemaji wa Kremlin Dimitry Peskov alithibitisha kuwa wamekataa mahojiano mengine kabla ya Carlson.
Hizi zilikuwa baadhi ya jumbe mashuhuri za Putin wakati wa mahojiano.
1. Kuivamia Poland, Lithuania au nchi nyingine ya NATO ni jambo ambalo "haliwezekani kabisa"

Chanzo cha picha, Reuters
Kiongozi wa Urusi alitoa uamuzi wa kuivamia Lithuania, Poland au nchi nyingine yoyote ya NATO, akisema kwamba uwezekano huu "hauwezekani kabisa."
Uvamizi wa Ukraine ulizidisha hofu miongoni mwa mataifa ya Baltic, Poland na nchi nyingine za Ulaya kwamba Urusi inaweza kuanzisha vikosi vyake dhidi yao pia.
Kwa kweli, zikiwa na wasiwasi juu ya uwezekano huu, Ufini na Uswidi, nchi ambazo kijadi hazikuegemea upande wowote katika vita kati ya Moscow na Magharibi, ziliamua kuomba uanachama katika NATO.
Katika mahojiano hayo, Putin aliondoa uwezekano wa uvamizi mwingine. Alisema kwamba ingetokea tu katika kesi moja, "ikiwa Poland itashambulia Urusi."
Katika wiki kadhaa kabla ya mashambulizi ya wanajeshi wa Urusi dhidi ya Ukraine, Moscow pia ilikanusha mara kwa mara kwamba ilikuwa ikipanga uvamizi huo ambao Marekani na idara zake za kijasusi walikuwa wakionya kuhusu.
Ingawa rais wa Urusi alikataa uwezekano wowote wa shambulio dhidi ya nchi ya NATO, alisisitiza kwamba muungano wa Atlantiki lazima ukubali kwamba Urusi inahifadhi maeneo ya Ukrain ambayo imeshinda tangu mwanzo wa uhasama.
2. Iwapo Marekani inataka vita viishe "inabidi iache kusambaza silaha [kwa Ukrainia]. Ingeisha baada ya wiki chache"

Chanzo cha picha, Reuters
Carlson alimuuliza rais wa Urusi ikiwa amefikiria kuzungumza moja kwa moja na rais wa Marekani, Joe Biden, kutafuta makubaliano ya kumaliza vita nchini Ukraine.
Putin alionekana kusisitiza kuwa kuna mawasiliano kati ya baadhi ya mashirika ya Urusi na Marekani lakini "hakuna la kuzungumza" wakati Marekani inaendelea kupeleka silaha Ukraine, sera aliyoitaja kuwa "kosa la kimkakati."
"Nitakuambia kwa kweli kile tunachojaribu kuufanya uongozi wa Marekani kuelewa: iwapo kweli unataka kuacha mapigano, lazima uache kusambaza silaha vita ingeisha baada ya wiki chache, "alisema.
Majibu ya Putin yanakuja wakati Bunge la Seneti la Marekani liliidhinisha mswada wa kupanua msaada wa kijeshi kwa Ukraine kwa dola bilioni 61, lakini linakabiliwa na upinzani mkali katika Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na chama cha Republican, wakiwemo makumi ya washirika wa Trump ambao wamepiga kura mara kwa mara kupinga msaada huo kwa Kyiv.
Tofauti na msimamo huu wa Putin, wafuasi wa Ukraine mara nyingi wanasema kwamba ni Moscow ambayo inapaswa kuweka chini silaha zake.
"Ikiwa Urusi itaacha kushambulia, vita vimekwisha. Lakini ikiwa Ukraine itaacha kujilinda, Ukraine imekwisha," wanasema.
3. "Hawawezi kuleta ushindi wa kimkakati kwa Urusi"
Kiongozi wa Urusi alirejelea jinsi Urusi ilivyojiimarisha wa silaha.
Alihalalisha hili kwa kuzingatia kukataa kwa serikali za Marekani zilizofuatana kukubali mapendekezo yake ya kupokonya silaha na kuangamizwa kwa silaha za nyuklia.
Ingawa alikataa kwamba nchi yake inapanga kuanzisha hatua za uchokozi dhidi ya mtu yeyote, Putin alielezea kile anachokiona kuwa maendeleo katika tasnia ya kijeshi ya Urusi, kama vile mifumo ya silaha za hypersonic, ya kiwango cha juu zaidi, alisema, kuliko ile ya nchi zingine.
Alionya kwamba watawala wa Magharibi wametambua kwamba "hawawezi kuisababishia Urusi kushindwa kimkakati," alisema.
4. "Ukraine ni taifa bandia ambalo liliundwa kwa mapenzi ya Stalin"

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati wa mahojiano, Putin alitoa kumbukumbu nyingi za kihistoria, zingine zikirudi nyuma hadi karne ya 13.
Hata hivyo, alitilia mkazo sana maelezo ya historia ya Muungano wa Usovieti katika miaka ya kabla ya Vita vya Kidunia vya pili.
Hasa, alisema kwamba wazo la Ukraine kama taifa ambalo lilikuwa sehemu ya USSR liliibuka "bila kueleweka" kutoka kwa akili ya kiongozi wa Usovieti Vladimir Lenin.
Alihakikisha kwamba uundaji wa Ukraine ulikuwa zao la mpango wa "mpango wa asili wa uzawa" wa mikoa ambao USSR iliuweka kwenye maeneo yake, ikitaka kukuza lugha na tamaduni za kitaifa.
Aliongeza kuwa mwisho wa vita, chini ya Stalin, Ukraine ilipokea mikoa kutoka Poland na Hungary, ambayo watu waliozungumza Kihungari au Kipolishi.
Hitimisho lake: "Ukraine ni taifa bandia ambalo liliundwa kwa mapenzi ya Stalin."
Hata hivyo, mwanahistoria Matthew Lenoe wa Chuo Kikuu cha Rochester amebainisha kwamba ingawa historia ya jimbo la ukrainne pengine haiwezi kupatikana kabla ya 1918, hakuna shaka kwamba sasa ni taifa.
"Putin anadai kwamba hakuna historia ya Ukraine tofauti na ile ya Urusi, lakini hiyo sio kweli ," Leone alisema katika mahojiano mnamo Machi 2022.
“Kati ya wazungumzani wa Kiukreni na katika ardhi ambayo inaiunda Ukraine kulikuwa na mambo mengi tofauti . Wakati mwingine walikuwa wa majimbo na falme tofauti. "Lakini kulikuwa na mwingiliano kati ya wazungumzaji wa Kiukreni katika sehemu kubwa ya historia hii na walikuza utambulisho mmoja, hasa baada ya katikati ya karne ya 19," aliongeza.
5. "Makubaliano yanaweza kufikiwa" kwa ajili ya kuachiliwa kwa mwandishi wa habari wa Marekani aliyefungwa nchini Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Putin alirejelea hali ya Evan Gershkovich, mwandishi wa habari wa "The Wall Street Journal" aliyefungwa nchini Urusi kwa mashtaka ya ujasusi.
Putin alisema anaamini makubaliano yanaweza kufikiwa kumwachilia Gershkovich, 32, "ikiwa washirika wetu watachukua hatua za kuafikiana . "
"Huduma maalum zinawasiliana. Wanazungumza... nadhani makubaliano yanaweza kufikiwa."
Gershkovich, mwandishi wa Wall Street Journal, alikamatwa katika jiji la Yekaterinburg, takriban kilomita 1,600 mashariki mwa Moscow, mnamo Machi 29 mwaka jana.
Mnamo mwezi wa Januari, Urusi iliongeza tena muda wake wa kuwa kizuizini c cha kuzuia hadi mwisho wa Machi. Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela iwapo atapatikana na hatia.
Carlson alimuuliza Putin ikiwa atakuwa tayari kumuachilia mwandishi huyo mara moja na kusema, "Tutamrudisha Marekani."
Gazeti analofanyia kazi na serikali ya Marekani wanadai kuwa mwandishi huyo alizuiliwa kinyume cha sheria.
Putin alidokeza ni nani Urusi itakubali katika kubadilishana wafungwa. Alitaja "mtu, kutokana na hisia za kizalendo, [ambaye] alimuondoa jambazi katika mojawapo ya miji mikuu ya Ulaya...wakati wa matukio katika Caucasus."
Hakika ilikuwa ni kumbukumbu ya Vadim Krasikov, muuaji wa FSB ambaye kwa sasa amefungwa nchini Ujerumani baada ya kumpiga risasi afisa wa jeshi la Georgia, Zelimkhan Khangoshvili, katika bustani ya Berlin mnamo 2019.
6. "Marekani iliahidi kwamba NATO haitapanuka na imetokea mara tano''

Chanzo cha picha, Reuters
Sehemu ya maelezo marefu ya kihistoria ya Putin kwa Tucker Carlson yalirejelea matukio mbalimbali ambapo Marekani iliripotiwa kuiambia Urusi kwamba NATO haitapanuka kuelekea mashariki hadi jirani na Urusi.
Kulingana na rais wa Urusi, viongozi kadhaa (ingawa siwataji kabisa) waliiahidi Kremlin kwamba NATO haitapanuliwa. Kwa Putin, baada ya kufutwa kwa USSR, hakukuwa na hitaji tena la shirika kama hilo.
Hata hivyo, hoja ya Putin si mpya. Mtangulizi wa Putin, Boris Yeltsin, alidai kwamba upanuzi wa NATO upande wa mashariki ulikuwa "haramu" mnamo 1993.
Yevgeny Primakov, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Urusi, alitoa hoja kama hiyo aliposema kwamba alikuwa amepokea ahadi kwamba "hakuna nchi yoyote ambayo itaondoka kwenye Mkataba wa Warsaw itaingia NATO'' .
Hata hivyo, kulingana na Kristina Spohr, profesa wa Historia ya Kimataifa katika Shule ya Uchumi ya London, ahadi pekee iliyotolewa kwa Urusi ilitokea baada ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin, wakati Moscow ilikubali kuondoa askari 380,000 iliyokuwa imeweka Ujerumani Mashariki na kuchukua nafasi zao. na vikosi vya NATO.
Wakati huo, James Baker, Waziri wa Mambo ya Nje wa George HW Bush, aliripotiwa kumwambia kwamba wanajeshi wa NATO hawatasonga "sio inchi moja kuelekea mashariki," lakini akimaanisha mpaka kati ya Ujerumani Magharibi na Mashariki.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












