Mambo 9 yaliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2022

kids
Maelezo ya picha, Viwango vya juu vya uzazi katika baadhi ya nchi vimesaidia kuongeza idadi ya watu duniani zaidi ya watu bilioni nane

Mwaka 2022 umewekwa alama na matukio mbali mbali ambayo hayajawahi kutokea - na sio yote yalifanyika kwenye sayari yetu! Kutoka kwenye "rekodi ya kuzidisha" hadi safari ya kina katika siku zetu zilizopita, haya ni baadhi ya matukio muhimu ambayo yalivutia macho yetu. Nasa inaelekeza umbo dogo la jiwe linalozunguka jua (asteroid) Shirika la anga za juu la Marekani lilifanikiwa kubadilisha njia ya asteroid baada ya kugonga kwenye chombo cha anga tarehe 28 Septemba. Mgongano huo uliundwa ili kujaribu ikiwa miamba ya angani ambayo inaweza kutishia dunia inaweza kusukumwa kwa usalama kutoka njia inayotumia na jibu likawa, Wanaweza.

Microplastics hugunduliwa katika damu ya binadamu

mm
Maelezo ya picha, Athari za microplastics katika mwili wa binadamu hazijulikani

Utafiti uliochapishwa katika jarida la Environment International mwezi Machi mwaka jana uliiona microplastics katika sampuli za damu katika 80% ya watu waliopimwa.

Microplastics ni vipande vidogo vya plastiki ambavyo vina urefu wa chini ya 5mm - huundwa wakati vipande vikubwa vya plastiki vinapoanguka kwenye udongo au baharini na kuchafua mazingira.

Athari za microplastics mwilini hazijulikani, lakini watafiti walisema matokeo mapya yanahusu na kwamba microplastics inaweza kuharibu seli za binadamu.

Mambo ya kwanza kutokea au kufanyika katika Kombe la Dunia

mm

Kombe la Dunia la FIFA la 2022 la Wanaume litaingia katika historia kwa mfululizo wa matukio muhimu ambayo hayajawahi kushuhudiwa. Kwa kuanzia, ilikuwa ni toleo la kwanza la mashindano hayo kuandaliwa na nchi ya Kiarabu au Kiislamu - Qatar.

Pia ilikuwa ni mechi ya kwanza kuwa na mwanamke kama mwamuzi mkuu wa mechi wakati Stephanie Frappart wa Ufaransa aliposimamia mechi ya hatua ya makundi kati ya Ujerumani na Costa Rica. Hakika, Frappart alikuwa nahodha wa timu ya waamuzi wa wanawake wote ambao pia walikuwa na waamuzi wasaidizi Neuza Back kutoka Brazil na Karen Medina wa Mexico.

Nyingine ya kwanza ilikuwa mashindano ya kuvutia ya Morocco hadi nusu fainali, matokeo bora zaidi kuwahi kufanywa na taifa la Kiafrika (na la Kiarabu). Na kwa kuwa tunazungumza juu ya hatua muhimu, Qatar 2022 ilikuwa hatua ambayo hatimaye ilishuhudia Lionel Messi akinyanyua taji la Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya majaribio matano!

Watu bilioni nane kati yetu… kuhesabiwa

nn

Tarehe 15 Novemba 2022. Hiyo ndiyo tarehe ambapo idadi ya watu duniani ilizidi watu bilioni nane kwa mara ya kwanza, kwa mujibu wa UN. "Ukuaji huu ambao haujawahi kushuhudiwa unatokana na ongezeko la polepole la maisha ya binadamu kutokana na kuboreshwa kwa afya ya umma, lishe, usafi wa kibinafsi na dawa. Pia ni matokeo ya viwango vya juu na vya kudumu vya uzazi katika baadhi ya nchi," shirika hilo lilitoa taarifa.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa ulisema wakati idadi ya watu duniani ilichukua miaka 12 kukua kutoka bilioni saba hadi nane, itachukua angalau miaka 15 kufikia bilioni ijayo, kwani viwango vya kuzaliwa kwa pamoja vinaonekana kupungua. 'Dunia kubadilishwa' kwa chanjo ya malaria

mm

Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Oxford walitangaza mnamo Septemba kuwa wametengeneza chanjo ya malaria yenye uwezo wa "kubadilisha ulimwengu". Inatarajiwa kuanza kutumika mwaka ujao, chanjo hiyo mpya ilipatikana katika majaribio na kuwa na ufanisi wa 80% dhidi ya ugonjwa huo hatari, ambao unaua karibu watu 400,000 kwa mwaka. Wanasayansi pia walisema kuwa chanjo yao ni nafuu.

Malaria ni mojawapo ya sababu kuu za vifo vya watoto duniani na kutengeneza chanjo dhidi yake ni vigumu sana, kwani vimelea vinavyosababisha malaria ni vigumu kukabiliana navyo. Ni shabaha inayosonga kila wakati, na kubadilisha fomu ndani ya mwili, ambayo hufanya iwe ngumu kupambana na chanjo.

LeDuc kushiriki Olympiki na kuweka historia katika masuala ya jinsia

m

Mchezaji wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu wa Marekani, Timothy LeDuc, amekuwa mtu wa kwanza ambaye hatambuliki kwa jinsia moja kushindana katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi, ambayo iliandaliwa Februari huko Beijing. LeDuc hakujishindia medali na alimaliza wa saba katika tukio la pamoja na Ashley Cain, lakini alitamba kote ulimwenguni.

Tulisafiri umbali mkubwa kwa wakati - kwa hisani ya darubini ya James Webb

mm

Darubini ya James Webb haikuona aibu kuchukua vichwa vya habari mnamo 2022 - tangu kuanza kufanya kazi mwezi Julai, imetoa picha za kushangaza za ulimwengu. Mojawapo ilikuwa picha ya kina kabisa ya ulimwengu wetu kufikia sasa, ikijumuisha JADES-GS-z13-0, galaxy iliyo na umri wa zaidi ya miaka bilioni 13 na iliyoanzia "siku za mapema" baada ya Big Bang. Kinachoonekana kama uchafu hafifu ni "galaxy ya mbali zaidi" hadi sasa iliyothibitishwa na kipimo cha kiwango cha dhahabu.

Mtu wa kwanza mwenye asili ya Asia kuwa Waziri mkuu wa Uingereza

m

Uingereza iliweka rekodi kadhaa zilizohusisha mawaziri wakuu mnamo 2022: Siku 45 za Liz Truss madarakani ulikuwa muda mfupi zaidi kuwahi kutokea kwa Waziri Mkuu kushika wadhifa huo. Hatua nzuri zaidi iliwekwa na mrithi wake: Rishi Sunak alikua mtu wa kwanza wa rangi kuchukua wadhifa huo tarehe 25 Oktoba.

Tuliona Bakteria bila darubini

mm

Wanasayansi walitangaza mwezi Juni kuhusu ugunduzi mkubwa zaidi wa bakteria duniani. Na hauitaji darubini ili kuona: kiumbe kipya kilichogunduliwa kina ukubwa na umbo sawa na kope za mwanadamu.

Urefu wa takriban 1cm, ni takriban mara 50 zaidi ya bakteria wengine wakubwa wanaojulikana na wa kwanza kuonekana kwa macho.