Kwa nini fibroids huwaathiri wanawake weusi na nini kinachoweza kupunguza hatari?

Na Ambia Hirsi

Fibroids

Chanzo cha picha, Getty Images

Lilly- sio jina lake halisi alifanyiwa upasuaji kuondo uvimbe uliokuwa umeota ndani ya nyumba ya uzazi.

''Nilikuwa niyapoteze maisha yangu ama nifanyiwe uspasuaji. Huwezi kuambia kila mtu kuhusu kutokwa na damu, hata mumeo.''

Lilly anasema tangu alipokuwa mtoto, alikuwa anataabika, kwa kile wanachokiita kwait huko Ghana (Candidiasis), katika lugha ya mtaa inaitwa odepu.

''Sikuuchukulia kwa uzito, kwa sababu lilikuwa jambo la kawaida.'' Anasema walijaribu kutibu hali hiyo kwa kutumia maji moto na vitu vingine, lakini alipokua na kuanza kupata hedhi, ilikuwa nzito sana. ''Niligundua kuwa nilikuwa na uvimbe wa kizazi nilipokuwa na umri wa miaka 25. Tulijaribu kuutibu kwa kununua dawa, tulijaribu pia dawa za kiasili, lakini hatukufanikiwa.''

Lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi wa wa kina wa kimatibabu madaktari waliamua kuwa uvimbe huo utolewa. Lilly angepoteza maisha yake kimchezo tu laiti hangefanyiwa upasuaji huo muhimu.

Lakini ni je, Fibroids ni nini?

Fibroids ni vimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha, unaoota na kukua kwenye nyumba ya uzazi ya mwanamke.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwapo na wanawake wengi wanaokumbwa na tatizo hili na miongoni mwao huishia kufanyiwa upasuaji kwa ili kuuondoa uvimbe huo.

Fibroids husababishwa na nini?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Chanzo hasa cha kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.

Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi.

Wanawake wenye asili ya mchanganyiko wa wamarekani na waafrika (wamarekani weusi) nao wanaonekana kupatwa na fibroids zaidi ya wanawake wengine ingawa sababu bado haijajulikana.

Utafiti umeonyesha pia kuwa idadi ya wanawake wanaopatwa na fibroids katika kundi la wanawake ambao wamezaa watoto angalau wawili wakiwa hai huwa ni nusu ukilinganisha na wale ambao hawajazaa hata mara moja.

Hapa haieleweki kama kuzaa kulizuia wanawake hawa wasipate fibroids au fibroids ndizo zilizozuia wanawake wa kundi la pili wasizae. Utafiti kuhusu hilli bado unaendelea.

Dalili Za Fibroids

  • Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa dedhi
  • Kutokwa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi
  • Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga)
  • Kupata haja ndogo mara kwa mara
  • Maumivu ya mgongo
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu kwenye miguu
  • Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)
  • Uzazi wa shida
  • Mimba za shida
  • Kutopata mimba
  • Kutoka kwa mimba mara kwa mara

Chanzo: NHS

Tiba ya Fibroids

Kama mwanamke hapati usumbufu wa namna yo yote katika shughuli zake za kawaida, anaweza asipewe tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid kwa sababu mwanamke anapokaribia kukoma hedhi fibroids hunyauka zenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa.

Endapo tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali iliyopo.

Tiba kubwa ya fibroids ni kwa kutumia dawa aina ya GnRHA (gonadotropin released hormone agonist) ambayo hutolewa kama sindano.

Dawa hii huufanya mwili wa mwanamke upunguze utengenezaji wa estrogen hivyo kusababisha fibroids kunyauka kwenye nyumba ya uzazi.

Tiba nyingine ni Tranexamic acid, vidonge vya kuzuia maumivu, vidonge vya kuzuia mimba (kuzuia mwanamke asipate siku) na LNG-IUS (Levonorgestrel intrauterine system) ambacho ni kifaaa cha plastiki kinachowekwa kwenye Tiba ya dawa zikishindwa kufanya kazi, mgonjwa hufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe.