Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kila kitu unachohitaji kujua kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo (ulcers)
Kwa muhtasati kidonda cha tumbo au duodenal ni jeraha la kina au kidonda ambacho hutokea kwenye utando wa ndani wa tumbo au sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum. Hutokea kutokana na kuvimba kwa muda mrefu kwa ukuta huu unaopendelewa na bakteria wanaofahamika kama helicopter pillory wanaopatikana kwenye njia ya utumbo.
Daktari wa magonjwa ya tumbo na mtaalam wa magonjwa katika kituo cha hospitali ya chuo kikuu cha Campus mjini Lomé, Togo, Dkt Roland Kogoe amezungumza na BBC na kustusaidia kuelewa vizuri ugonjwa huu.
Tumbo ni moja ya viungo vinavyounda mfumo wa usagaji chakula, jukumu lake ni kusaga chakula na kukihamisha kwenye utumbo. Liko upande wa kushoto wa ya tumbo chini ya mbavu na sehemu iliyofichwa na ini na diaphragm.
Tumbo huenea kusambaa hadi kwenye duodenum: limeunganishwa na umio, kwa ajili ya kuingizwa kwa chakula, na kwenye utumbo mdogo kwa ajili ya kutoa chakula kwenye tumbo.
Je, vidonda vya tumbo ni nini?
Vidonda husababishwa na kubanduka kwa utando ambako hutokea wakati ambapo sehemu ya nyama wa tumbo au utumbo zimeharibiwa.
Ni jereha lenye linalosababisha uwepo wa kidonda, kulingana na Dk Roland Kogoe, anasema mtaalamu wa magonjwa ya tumbo.
"Ukuta wa tumbo na duodenum ni pamoja na tabaka nne na mgonjwa husemekana kuwa na ugonjwa wa vidonda/ kidonda cha tumbo wakati kidonda kinapofikia safu ya tatu.
Kwa hivyo ni kidonda ambacho kitaondoa utando wa sehemu ya ndani ya tumbo mfululizo hadi kufikia kufikia kwenye utando laini wa nyongo ya kibofu . Ni wakati misuli imeathiriwa ndipo tutazungumza juu ya kidonda. Vinginevyo tutasema unasumbuliwa na tatizo gastritis (asisi ya tumbo) ,” anaeleza.
Kidonda kinachoitwa "gastric ulcer" kikiwa ndani ya tumbo na "duodenal ulcer" kinapokuwa kwenye sehemu ya mwisho ya tumbo husababisha maumivu ya papo hapo.
Je! ni kidonda/vidonda vya tumbo husababishwa na nini?
Chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo ni bakteria Helicobacter pylori (H. pylori) wanaopatikana katika asilimia 90 ya matukio na matumizi ya dawa za kuzuia maumivu zisizo na steroide (NSAIDs).
“Tunapozungumzia sababu za vidonda tutatofautisha aina mbili , kwanza ni maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori, ni bakteria ambao tunawapata tukiwa wadogo kwa kula vitu mbali mbali ambão husababisha uzalishaji mwingi wa asidi tumboni ambayo inaweza kusababisha kidonda,” anasema Dk Kogoe.
Sababu ya pili ya vidonda ni tabia fulani na mambo ya maisha, ambayo yanaweza kuchangia kuongezeka kwa bakteria hawa au kuzidisha vidonda vilivyopo.
"Ni ukweli, kwa mfano, kufunga, kuruka mlo, au kutumia dawa zenye asterods uchochezi, hususan aspirini au ibuprofen.
Sababu nyingine ni matumizi ya "pombe kwenye tumbo tupu. Kwa hivyo vitu hivi vitagusana moja kwa moja na utando wa tumbo au ule wa sehemu ya mwisho ya tumbo inayosafirisha chakula kwenye utumbo na kusababisha uvimbe ambao unaweza kusababisha kidonda," anasema Dk Kogoe.
Kuambukizwa na bakteria ya Helicobacter pylori ni moja ya magonjwa sugu yaliyoenea zaidi ulimwenguni: 20% hadi 90% ya watu wazima wameambukizwa katika nchi mbali mbali , kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
Maambukizi ni ya kawaida zaidi katika nchi zinazoendelea ni (80% hadi 90%) kuliko katika nchi zilizoendelea ambazo ni (25% hadi 30%).
Bakteria ya H.pylori hushambulia safu ya ute wa tumbo ambayo kwa kawaida hulinda tumbo na utumbo mwembamba dhidi ya asidi ya tumbo.
Zifuatazo ni baadhi ya tabia za kawaida ambazo zinaweza pia kusababisha uzalishaji wa asidi kali ndani ya tumbo na hivyo kuongeza uwezekano mkubwa wa kukua kwa vidonda vya tumbo:
- Uvutaji sigara: Uvutaji sigara umehusishwa na kuongezeka kwa hatari ya vidonda vya tumbo. Uvutaji sigara unaweza kuingilia kati safu ya kinga ya tumbo na pia inaweza kuchelewesha mchakato wa uponyaji wa vidonda vilivyopo.
- Unywaji pombe kupita kiasi: Unywaji pombe kupita kiasi unaweza kumomonyoa utando wa tumbo, hivyo kuongeza hatari ya kupata vidonda. Unaweza pia kuingilia kati mchakato wa uponyaji wa vidonda vilivyopo.
- Msongo wa mawazo: Ingawa mfadhaiko wenyewe hausababishi vidonda vya tumbo moja kwa moja, unaweza kuzidisha hali zilizopo. Msongo wa mawazo wa kudumu unaweza kusababisha mabadiliko ya kitabia ya tumbo, kama vile ulaji usiofaa au kuongezeka kwa matumizi ya pombe na tumbaku, ambayo yanaweza kuchangia ukuaji wa vidonda.
- Unywaji wa kafeini kupita kiasi: Ingawa unywaji wa kafeini wastani kwa ujumla huchukuliwa kuwa salama kwa watu wengi, unywaji wa kupita kiasi unaweza kuchochea utengenezaji wa asidi tumboni na uwezekano wa kuchangia ukuaji wa vidonda.
- Kula kupita kiasi: Kula milo mikubwa kunaweza kuweka shinikizo kubwa kwenye tumbo, na kusababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa asidi. Hii inaweza kuharibu utando wa tumbo na kuchangia kutokea kwa vidonda.
- Kupuuza Dalili za Vidonda: Kupuuza dalili kama vile maumivu ya tumbo, kutokwa na damu au kiungulia na kutomuona daktari kunaweza kufanya vidonda kuwa mbaya zaidi. Utambuzi wa haraka na matibabu unaweza kuzuia shida.
- Matumizi kupita kiasi ya Antacids: Ingawa antacids (dawa za kuzuia asisi ya kupindukia) zinaweza kupunguza dalili, kuzitegemea kupita kiasi bila kushughulikia sababu kuu kunaweza kufunika dalili na kuchelewesha utambuzi na matibabu sahihi.
Je, ni dalili za kidonda cha tumbo?
Vidonda vya tumbo hujidhihirisha kwa maumivu ya epigastric: epigastrium ni kiungo kilichopo katikati ya juu ya tumbo.
Mgonjwa huhisi hali ya kuungua kukandamizwa kwenye tumbo la juu. Maumivu haya huwa makali sana katika saa za kwanza baada ya kula na hupungua unaposhiba.
Ugonjwa huo pia unajidhihirisha na dyspepsia, yaani, hisia ya kuvimbiwa tumbo, tumbo kushindwa kumeng’enya chakula kama kawaida, kichefuchefu au kutapika au katika hali mbaya zaidi kwa kutokwa na damu.
Kidonda husababisha maumivu makubwa kwa sababu kinagusana moja kwa moja na asidi iliyopo kwenye njia ya utumbo.
“Naomba nitoe ufafanuzi, kwa sababu kwa ujumla tunaona watu ambao kila wakiumwa tumbo hujitangaza kuwa wana vidonda. Kuwa makini, kuna viungo vingi ndani ya tumbo vinavyoweza kusababisha maumivu. Maumivu yanaweza kufanana na vidonda vya tumbo wakati sio na kwa hiyo wakati unakabiliwa na maumivu ya tumbo, ni bora kupata ushauri wa daktari’’, inabainisha Dkt Roland Kogoe.
Utambuzi wa vidonda au kidonda cha tumbo kwa kweli hauwezekani kufanikiwa kwani dalili ambazo zake huwa ni za sawa na magonjwa mengine.
Kwa hiyo ni muhimu kufanyiwa vipimo vya fibroscope ya gastroduodenal ambavyo huruhusu kubaini uwepo na kiwango cha vidonda na kuchukua sampuli (biopsy) ambayo itachambuliwa katika maabara.
Je ni dalili za vidonda vya tumbo ni zipi?
Vidonda vya tumbo hujidhihirisha kwa maumivu ya epigastric: epigastrium ni kiungo kilichopo katikati ya juu ya tumbo.
Mgonjwa huhisi hali ya kuungua kukandamizwa kwenye tumbo la juu. Maumivu haya huwa makali sana katika saa za kwanza baada ya kula na hupungua unaposhiba.
Ugonjwa huo pia unajidhihirisha na dyspepsia, yaani, hisia ya uzito wa tumbo, tumbo kushindwa kumeng’enya chakula kama kawaida, kichefuchefu au kutapika au katika hali mbaya zaidi kwa kutokwa na damu.
Kidonda husababisha maumivu makubwa kwa sababu kinagusana moja kwa moja na asidi iliyopo kwenye njia ya utumbo.
“Naomba nitoe ufafanuzi, kwa sababu kwa ujumla tunaona watu ambao kila wakiumwa tumbo hujitangaza kuwa wana vidonda. Kuwa makini, kuna viungo vingi ndani ya tumbo vinavyoweza kusababisha maumivu. Maumivu yanaweza kufanana na vidonda vya tumbo wakati sio na kwa hiyo wakati unakabiliwa na maumivu ya tumbo, ni bora kupata ushauri wa daktari’’, inabainisha Dkt Roland Kogoe.
Utambuzi wa vidonda au kidonda cha tumbo kwa kweli hauwezekani kufanikiwa kwani dalili ambazo zake huwa ni za sawa na magonjwa mengine.
Kwa hiyo ni muhimu kufanyiwa vipimo vya fibroscope ya gastroduodenal ambavyo huruhusu kubaini uwepo na kiwango cha vidonda na kuchukua sampuli (biopsy) ambayo itachambuliwa katika maabara.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi