Mkutano wa G7: Kwa nini kuna viti vinane zaidi kwenye mwaka huu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Laiti G7 ingelikuwa karamu ya chakula cha jioni, mwenyeji angelikuwa anatafuta meza kubwa ambayo inaweza kurefushwa, kupekua kabati kutafuta vitambaa vya mezani na vijiko vya zaida
Mwenyeji wa mwaka huu, Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida, amewaalika wageni wengine wanane kwenye mkutano huo utakaoanza Ijumaa huko Hiroshima.
Hakika ni ishara ya ajenda ambayo ni mwiba ambayo ni kati ya vita vya Ukraine hadi kiasi cha chakula kinachofikia sahani zetu za chakula cha jioni. Na pia ni ushahidi wa mpangilio wa kimataifa unaobadilika kwa kasi, huku mazungumzo mengi yakizingatia nchi mbili ambazo haziko kwenye orodha ya wageni: Urusi na China.
Mkutano huo wa kila mwaka unajumuisha nchi saba tajiri zaidi za kidemokrasia duniani, Japan, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Canada na Italia. Umoja wa Ulaya, ingawa si mwanachama rasmi wa G7, pia hutuma wawakilishi. Hivi karibuni, waandaaji wamealika nchi zaidi kwa hiari yao.
Lakini uwezo wa kiuchumi wa G7 unapungua, mwaka 1990, kundi hilo lilichangia zaidi ya nusu ya Pato la Taifa la dunia, kulingana na Shirika la Fedha Duniani. Sasa ni chini ya 30%. Inahitaji marafiki wapya wenye ushawishi.
Kwa hiyo Bw Kishida, ambaye anatafuta muungano wa kimataifa zaidi badala ya Magharibi, ameongeza meza ili kuchukua nafasi ya Australia, India, Brazil, Korea Kusini, Vietnam, Indonesia, Comoro (inayowakilisha Umoja wa Afrika) na Visiwa vya Cook (vinawakilisha Visiwa vya Pasifiki.)
Waziri Mkuu wa Japan amefanya safari 16 za ng'ambo katika muda wa miezi 18 iliyopita, zikiwemo India, Afrika na Kusini, Mashariki mwa Asia, ili kuthibitisha kwa maeneo haya kwamba kuna njia mbadala ya pesa na nguvu za China na Urusi.
Na orodha yake ya wageni kwa Hiroshima inaakisi majaribio haya ya kuvutia kile ambacho wengi wanakiita "Global South" - neno linalotumika kwa nchi zinazoendelea za Asia, Afrika na Amerika ya Kusini, ambazo zote zina uhusiano mgumu wa kisiasa na kiuchumi na Urusi na China.
Mojawapo ya malengo yaliyo wazi zaidi ya Bw Kishida, kuonesha "umoja" kuhusu ajenda ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine pia itakuwa moja ya vikwazo vyake vikubwa.
Kundi la G7 linaripotiwa kujaribu kutekeleza vikwazo zaidi vinavyolenga nishati na mauzo ya nje kusaidia juhudi za vita vya Moscow.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lakini wengi wa wageni wa ziada hawatapenda hatua hii. India, kwa mfano, imekataa kuambatana na vikwazo vya Magharibi kwa uagizaji wa Urusi.
New Delhi pia haijalaani kwa uwazi uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Uhusiano wao wa muda mrefu kando, India pia inategemea uagizaji wa nishati na imetetea ununuzi wake wa mafuta, ikisema haiwezi kumudu bei ya juu.
Nchi zinazoinukia kiuchumi zimeathirika zaidi na kupanda kwa gharama, kwa kiasi fulani kutokana na vita vya Ukraine.
Sasa wanahofia kuwa vikwazo zaidi vinaweza kulazimisha Moscow kusitisha mkataba wa nafaka wa Bahari Nyeusi ambao utawezesha mauzo muhimu ya nje kutoka Ukraine. Hii inaweza kuongeza uhaba wa chakula na kuongeza bei zaidi.
Kwa wengine, hii sio tu kuhusu gharama ya binafsi ya vikwazo.
"Vietnam ina uhusiano wa karibu kihistoria na Urusi, ambayo hutoa angalau 60% ya silaha zao na 11% ya mbolea," anasema Nguyen Khac Giang, mtembeleaji mwenzake katika Taasisi ya Mafunzo ya Asia Kusini Mashariki huko Singapore.
"Indonesia, ingawa haitegemei sana Urusi, ni muuzaji mkubwa wa silaha za Urusi na inadumisha uhusiano mzuri na Moscow.
"Kwa sababu hizi, siamini kwamba Hanoi na Jakarta zitapinga kwa uwazi, au kuunga mkono, vikwazo zaidi dhidi ya Urusi. Kufanya hivyo kutaleta hatari kubwa za kiuchumi na kisiasa, huku kukitoa faida kidogo kwao."
Kile ambacho Bw Kishida lazima atarajie ni kwamba mji alikozaliwa wa Hiroshima, ambako bomu la atomiki liliua zaidi ya watu 100,000, litakazia kuhusu tishio la nyuklia ambalo Urusi inaleta.
Ziara za kuzunguka jiji zitakuwa ukumbusho wa mara kwa mara wa uharibifu ambao silaha , na pia kuunga mkono ujumbe kwamba walioalikwa wana jukumu la kuhakikisha kuwa silaha kama hiyo haitumiki tena.
Shinikizo pia litakuja kutoka kwa Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky ambaye atakuwa huko kwa hakika ili kutoa ombi la huruma kwa watu wake ambao tayari wamelipa gharama kubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hiyo, hata hivyo, inaweza isitoshe kutatua mgawanyiko wa jinsi vikwazo vinapaswa kuwa. Na pia kuna hali ya kuchanganyikiwa inayoongezeka miongoni mwa nchi zilizo nje ya G7 kwamba sauti zao mara nyingi zimepuuzwa na nchi za Magharibi. Lakini wachambuzi wanaamini kusikiliza na kuzichukulia nchi hizi kama washirika angalau ni mwanzo.
"Inatoa fursa ya kuwasilisha matatizo yao na viongozi wa G7 kuhusu masuala mengi, kuanzia vita vya Ukraine na kudorora kwa uchumi wa dunia, hadi hatari za usalama katika Asia Mashariki, hasa kuhusu mzozo wa Bahari ya Kusini ya China na Taiwan," anasema Nguyen Khac Giang wa Vietnam na ushiriki wa Indonesia.
Kukabiliana na China
Taiwan na mivutano katika bahari inayoizunguka bila shaka imekuwa moja ya migogoro mikubwa katika mwaka uliopita.
Na kama kiongozi wa kundi pekee la Asia G7, Bw Kishida anauona mkutano huo kama fursa ya kujibu ongezeko la nguvu za kijeshi la China katika kisiwa hicho kinachojitawala, ambacho inadai.
Ujumbe wa Tokyo kwa nchi za Magharibi ni wa moja kwa moja, pambano lako nchini Ukraine pia ni pambano letu, lakini hilo lazima lifanyike kwa njia zote mbili.
Lakini China, ambayo imeshonwa kikamilifu katika minyororo ya usambazaji wa kimataifa, labda ni changamoto ngumu kuliko hata Urusi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika safari ya hivi karibuni huko Beijing, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alionya kwamba Ulaya haipaswi "kushikwa na machafuko ambayo sio yetu". Maneno yake yalizua mzozo mdogo huko Magharibi, lakini pia yalizidisha hofu ya kuachwa kote Asia Mashariki.
Wengi watakumbuka maneno ya Seneta wa Republican Lindsay Graham ambaye, katika kilele cha mvutano na Korea Kaskazini, alionya: "Ikiwa maelfu watakufa, watakufa huko." Kisha kikaja kitisho cha Rais Donald Trump kupunguza wanajeshi wa Marekani nchini Korea Kusini.
Sauti ya China, wachambuzi wanasema, inasikika waziwazi kwa sababu, tofauti na demokrasia za Magharibi, msimamo wake haubadiliki kila baada ya uchaguzi.
Bila shaka, Marekani, katika mwaka uliopita, haijayumba katika msaada wake kwa Ukraine, au katika ahadi yake kwa Taiwan. Na imeweka onesho lake huko Pasifiki, pamoja na washirika Japan, Korea Kusini, Ufilipino na Australia.
Lakini G7 hailengi tu malengo ya kijeshi ya China. Pia wana wasiwasi kuhusu kile wanachokiita "shurutisho la kiuchumi" na Beijing kulipiza kisasi kwa vitendo vyovyote vinavyoonekana kuwa vya kukosoa China, kama vile kupunguza uagizaji wa Australia mnamo 2019, au kulenga biashara ya Korea Kusini mnamo 2017.
Haijulikani ni hatua gani za kukabiliana na G7 zitachukua, au ikiwa inaweza hata kukubaliana na washirika wake wa EU kuhusu jinsi ya kutenda pamoja. Baada ya yote, Japan na EU zote zinahesabu China kama mshirika mkuu wa biashara.
Lakini sehemu ngumu zaidi itakuwa kuzishawishi nchi nyingine kufanya hivyo, kwa sababu sehemu kubwa ya Kusini mwa Ulimwengu inafungamana zaidi kiuchumi na Beijing.
Biashara ya China na Amerika ya Kusini inastawi, kwa mfano. Beijing sasa inachangia 8.5% ya Pato la Taifa la kanda, wakati Brazil ni miongoni mwa nchi ambazo zina ziada ya biashara na China. Lakini barani Afrika, mataifa kadhaa, zikiwemo Ghana na Zambia, yana deni kubwa kwa China na yanatatizika kurejesha mikopo.
Beijing imetoa maoni yake kuhusu hatua zozote zinazoongozwa na G7: "China yenyewe ni mwathirika wa shurutisho la kiuchumi la Marekani na siku zote tumekuwa tukipinga vikali kulazimishwa kiuchumi na nchi nyingine," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin alisema wiki iliyopita.
Uwanja mpya wa vita
Kuna eneo moja ambalo vita vya ushawishi bado vinaendelea - Visiwa vya Pasifiki. Inaeleza kwa nini taifa dogo la Visiwa vya Cook, ambalo linawakilisha nchi za Visiwa vya Pasifiki, liko kwenye orodha ya wageni.
Yakiwa katika hatari kubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa, mataifa haya ya visiwa yanatumia umuhimu wao wa kimkakati na Marekani na China.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka jana, Beijing ilitia saini mkataba wa usalama na Visiwa vya Solomon na kusababisha wasiwasi kwamba itajenga kambi ya kijeshi katika eneo hilo. Marekani ilijibu haraka, na kutangaza mpango, ikiwa ni pamoja na $810m katika msaada wa kifedha, na mataifa 14.
Sasa juhudi za Bwana Kishida za kujenga muungano pia zitategemea jinsi G7 itakubali kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa nishati, sio kwa sababu hiyo inaweza kupunguza utegemezi wa nchi kwa mafuta na gesi ya Urusi, au msaada wa China.
Baada ya mkutano huo, Rais Joe Biden alielekea Papua New Guinea, na kuwa rais wa kwanza wa Marekani kuzuru Visiwa vya Pasifiki.
Sasa anakatisha safari yake kwa sababu ya mzozo unaozuka nyumbani kutokana na kikomo cha deni la Marekani. Hiyo ni kikwazo, kulingana na Richard Maud, mfanyakazi mwandamizi katika Taasisi ya Sera ya Jumuiya ya Asia na mkuu wa zamani wa ujasusi wa Australia.












