Utabiri Ligi kuu ya Uingereza: Timu gani itashika nafasi ipi msimu wa 2023-24?

    • Author, Phil McNulty
    • Nafasi, BBC

Utabiri kwamba Manchester City watakuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita, ulikuwa sahihi. Hivyo hebu tuweke utabiri mwingine wa ligi hiyo kwa msimu ujao - wakati bado kuna wiki kadhaa kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa.

uiuyui

Chanzo cha picha, getty image

1. Manchester City

Ni vigumu kutabiri asiyekuwa Manchester City kushinda taji la msimu ujao. Ingawa Gundogan na Riyad Mahrez, wameondoka lakini kikosi cha kutisha kinasalia na kuongezwa wachezaji wawili kutoka Crotia, Mateo Kovacic, ambaye ataongeza uzoefu na ubora katika safu ya kati, na beki Josko Gvardiol. Erling Haaland na Kevin de Bruyne, na wachezaji wengine wengi, watabaki katika timu hiyo kwa msimu huu.

w

Chanzo cha picha, Getty Images

2. Liverpool

Ilishika nafasi ya tano msimu uliopita. Msimu huo haukuwa mzuri kwa meneja Jurgen Klopp na wachezaji wake, miezi 12 baada ya kushinda Kombe la FA na Kombe la Carabao. Kubweteka kutokana na ushindi huo kulielezwa kama ndio chanzo cha kufeli kwao.

Natarajia kufufuka kwa Liverpool, haswa kwa kuwa wanajivunia nguvu ya safu ya ushambuliaji ya Mohamed Salah, Cody Gakpo, Luis Diaz, Diogo Jota na Darwin Nunez.

3. Arsenal

Msimu uliopita ilishika nafasi ya pili. Arsenal walikuwa bora msimu uliopita lakini walishindwa na nguvu za Manchester City. Kikosi cha meneja Mikel Arteta kilicheza kandanda bora.

Declan Rice alisajiliwa kwa ada kubwa. Timu hiyo pia imetumia pesa nyingi kumnunua Kai Havertz kutoka Chelsea. Beki wa Uholanzi, Jurrien Timber, anaweza kuonyesha kiwango kingine cha juu wakati Arsenal ikijiandaa kwa kampeni ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 2016-17.

Hayo yote ni pamoja na ubora ambao wachezaji wa Arsenal walikuwa nao akina Bukayo Saka, nahodha Martin Odegaard, Gabrial Martinelli na wengineo. Ushindi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City uliongeza morali. Je, naiona Arsenal kama washindi wa taji? Hapana. Je, naiona Arsenal kama washindi wa makombe? Ndiyo.

4. Manchester United

Msimu uliopita walishika nafasi ya tatu. Erik ten Hag anaendelea kuijenga timu hiyo baada ya msimu wake wa kwanza kuleta Kombe la EFL - kombe la kwanza la United tangu 2017 - na kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa, na kufika hadi fainali ya Kombe la FA, ambayo ilimalizika kwa kushindwa na Manchester City. United inaendelea kujiboresha lakini hakuna nafasi ya kutwaa taji.

5. Aston Villa

Msimu uliopita ilishika nafasi ya saba. Nina hisia tutaona Aston Villa yenye nguvu sana msimu huu. Wameonyesha nia ya kweli katika soko la uhamisho. Beki mpya Pau Torres amekuwa akizingatiwa sana. Winga wa Ufaransa Moussa Diaby anatizamiwa kuwika katika nafasi ya ushambuliaji. Youri Tielemans pia anaweza kuthibitisha kuwa ni uhamisho bora kutoka Leicester City.

6. Chelsea

Msimu uliopita ilishika nafasi ya 12. Chelsea sasa inaongozwa na Mauricio Pochettino baada ya masaibu ya muhula uliopita, ambapo mameneja watatu - Thomas Tuchel, Graham Potter na Frank Lampard – walifurushwa na timu kumaliza katikati ya jedwali.

Cesar Azpilicueta, Mason Mount, Kai Havertz, Christian Pulisic, Kalidou Koulibay na N'Golo Kante wote wameondoka. Ingawa kuna talanta isiyo na shaka kutoka kwa Enzo Fernandez, huku Mykhailo Mudryk akitumai kuonyesha kiwango chake cha kweli. Levi Colwill anaweza kuwa nyota mkubwa katika safu ya ulinzi.

Kiungo ni eneo ambalo linahitaji kushughulikiwa, Moises Caicedo wa Brighton akionekana wazi kuwa ndiye aliyechaguliwa ikiwa dili litafanyika. Chelsea haitakuwa karibu na taji, lakini ninaamini Pochettino atawaweka kwenye kiwango bora.

7. Newcastle United

Matumizi ya Newcastle yamekuwa makubwa, tangu walipochukuliwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi. Mbinu hiyo imeendelea msimu huu wa joto huku kiungo wa kati wa Italia Sandro Tonali akiwasili kutoka AC Milan kwa pauni milioni 55 na kipa wa Harvey Barnes alisajiliwa kutoka Leicester City. Beki wa pembeni anayechipukia Tino Livramento kutoka Southampton ni tegemeo.

Sina uhakika itamaliza nne bora lakini timu hiyo inasonga mbele kuelekea kwa kasi.

8. Tottenham Hotspur

eewe

Chanzo cha picha, getty image

Maelezo ya picha, Je, Will Harry Kane atabaki Tottenham msimu huu?

Msimu uliopita ilishika nafasi ya 8. Sakata la muda mrefu la uhamisho wa Harry Kane kwa mara nyingine tena limetoa manufaa kwa Spurs, huku Ange Postecoglou akiwa amewasili kutoka Celtic kuchukua majukumu mapya.

Ikiwa Kane atasalia, basi Spurs inaweza kufika mbali. Spurs wameimarika baada ya kuwasili kwa kiungo wa kati wa Uingereza James Maddison kutoka Leicester City, huku kipa Guglielmo Vicario akitumai kuwa mrithi wa Hugo Lloris. Micky van de Ven anakuja na sifa kubwa huku beki wa Uholanzi chini ya umri wa miaka 21 akijiunga kwa mkataba wa pauni milioni 43 kutoka Wolfsburg.

9. Brighton

Msimu uliopita ilimaliza nafasi ya 6. Brighton ilikuwa na mchanganyiko mzuri sana wa soka ya kusisimua ya kushambulia na mpangilio mzuri chini ya Roberto de Zerbi.

Ninatarajia watakuwa na msimu mwingine mzuri wakati huu, ingawa watamkosa Alexis Mac Allister, na mustakabali wa Moises Caicedo haujuulikani. Iwapo Brighton watampata mchezaji wa Ajax, Mohammed Kudus itaongeza nguvu yao ya kushambulia.

Brighton wameleta mshambuliaji Joao Pedro kutoka Watford, huku kipa wa Uholanzi chini ya miaka 21 Bart Verbruggen akiwasili kutoka Anderlecht. Beki wa kati wa Brazil, Igor Julio ataongeza nguvu ya ulinzi kufuatia kuhama kutoka Fiorentina, na usajili wa James Milner kutoka Liverpool.

10. Brentford

Msimu uliopita ilishika nafasi ya 9. Brentford itamkosa mshambuliaji wake Ivan Toney hadi atakaporejea Januari baada ya kusimamishwa kwa kukiuka sheria za kamari za Shirikisho la Soka.

Nathan Collins atafanya vyema katika safu ya ulinzi kufuatia usajili wake wa pauni milioni 23 kutoka Wolverhampton Wanderers. Frank pia anatafuta kuongeza nguvu safu ya mashambulizi.

Time nyingine

feeff

Chanzo cha picha, getty image

Maelezo ya picha, Sean Dyche kocha wa Everton

11 West Ham ilishika nafasi ya 14 msimu uliopita.

12 Crystal Palace ilishika nafasi ya 11.

13 Fulham nafasi ya 10 msimu uliomaliza.

14 Nottingham Forest nafasi ya 16.

15 Bournemouth ilishika nafasi hiyo hiyo msimu uliomaliza. 17 Burnley ilishika nafasi ya kwanza Championship.

16 Everton nafasi ya 17 msimu uliomaliza.

18 Wolverhampton Wanderers nafasi ya 13 msimu ulioisha.

19 Sheffield United nafasi ya pili Championship, msimu uliopita.

20 Luton nafasi ya tatu Championship, msimu uliotamatika.