Kisspeptin: 'Baada ya kutumia homoni hii nilijifungua mtoto wa kiume'

Chanzo cha picha, PA
Tafiti mbili za hivi majuzi zimeonyesha kuwa wanaume na wanawake walio na hamu ya chini ya ngono wanapopewa homoni ya kisspeptin, eneo la ubongo linalohusishwa na hamu ya ngono huimarika.
Watafiti wa Uingereza wanasema kwamba kisspeptin inaweza kutatua kwa ufanisi tatizo la kupungua kwa hamu ya ngono, ambayo huwapata takriban asilimia 10 ya watu.
Watafiti katika Chuo cha Imperial London wanasema kwamba watu wazee wana uwezekano mkubwa wa kusema kwamba tamaa zao zinapungua kuliko watu wengine
Hata hivyo, watu wengi hupuuza. Lakini tatizo hili pia huwalemaza baadhi ya watu kiakili na kijamii.
Peter mwenye umri wa miaka 43 (jina limebadilishwa) pia alikuwa akisumbuliwa na tatizo hilohilo. Pia alishiriki katika mojawapo ya tafiti hizi.
Alisema, "Nimechoka sana. shinikizo ni kubwa. Sasa mimi ndiye ninayetoa visingizio vya kusema hapana".
"Sikuwaambia wazazi wangu kuhusu hili. Kwa sababu niliogopa kwamba wanaweza kufikiri kwamba siwapendi wasichana" aliongeza.
Kisspeptin ni homoni asilia inayozalishwa katika mwili.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ina jukumu kubwa katika kutolewa kwa homoni nyingine zinazohusiana na ngono katika mwili.
Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa homoni hii inaweza kuchochea ovari kuzalisha mayai kwa wanawake.
Kwa upande mwingine, imepatikana pia kuboresha hisia kwa wanaume.
Hata hivyo, ni mara ya kwanza imejaribiwa jinsi inavyofanya kazi kwa watu walio na tamaa ya kiwango cha chini kushiriki ngono.
"Watu wengi wenye tamaa ya kiwango cha chini kushiriki ngono hufikiria sana kufanya ngono. Matokeo yake ni kwamba wanateseka kwa kujidharau. Na mara nyengine hakuna msisimko katika sehemu zao za siri," alisema Dkt Alexander Kamninos, ambaye aliongoza utafiti huo.
"Suluhisho la kisspeptini linaweza kuonyesha uukosefu wa usawa huu," anasema.
Homoni hii hufanya kazi tofauti kidogo na dawa ya Viagra katika kuboresha usambazaji wa damu kwa sehemu za siri za kiume.
Wanaume 32 wenye umri wa miaka kati ya 21-52 na wanawake 32 wenye umri wa miaka kati ya 19-48 walishiriki katika tafiti mbili ili kubaini utendaji wake. Wote wanakabiliwa na ugonjwa wa kupungua kwa hamu ya ngono.
Wakati mwingine walipewa kisspeptini na wakati mwingine placebo. Wakati huo, tabia zao pamoja na sehemu za ubongo zilichunguzwa kwa msaada wa vipimo vya MRI. Harakati za sehemu za siri miongoni mwa wanaume pia zilichunguzwa.

Chanzo cha picha, Getty images
‘Nilimzaa Babu'
Peter alisema ilikuwa ni jambo la ajabu kuchunguzwa sehemu zake za siri akiwa kwenye skana, lakini kushiriki katika utafiti huo kulikuwa na manufaa.
"Sasa nina mtoto wa kiume. "Babu alizaliwa baada tu ya mimi kutumia homoni hiyo," alisema.
Lakini, je homoni hii ndio iliohusika na hili? Alisema kuwa ni vigumu kuthibitisha ukweli, lakini sasa tamaa yake ya kutaka kushiriki tendo la ngono imeongezeka.
Uchunguzi umeonyesha kuwa kisspeptini huwezesha maeneo muhimu ya ubongo yanayohusiana na hamu ya ngono kwa wanaume na wanawake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata kwa wale ambao hawana tamaa, hali yo huimarika kwa kiwango kikubwa. Wanaume waliotumia kisspeptini waliongeza ugumu wa uume wao kwa asilimia 56 ikilinganishwa na placebo.
"Katika hali nyingi huwa na matokeo chanya. Kwa kweli tulichunguza ubongo katika maabara. Katika chumba kimoja cha kulala au mahali pengine nyumbani, hali inaweza kuwa bora,'' anasema Camminos.
Wanawake waliripoti kuhisi kuwa na hamu ya kushiriki ngono zaidi baada ya kutumia kisspeptini, wakati wanaume waliripoti kuongezeka kwa viwango vya furaha wakati wa ngono.
Utafiti huo uliowahusisha wanaume na wanawake ulichapishwa katika Jarida la Mtandao wa JAMA.
Matatizo ya uhusiano, mfadhaiko, upungufu wa nguvu za kiume, kukauka kwa uke, kukoma hedhi na uchovu baada ya kuzaa vyote vinaweza kuchangia kupunguza hamu ya ngono, kulingana na tovuti ya NHS.
Aina fulani za dawa za mfadhaiko na vidonge vya kudhibiti uzazi pia vinaweza kupunguza hamu. Unywaji wa pombe pia unaweza kukuathiri
Magonjwa sugu kama vile magonjwa ya moyo, kisukari, tezi dume, saratani pia wakati mwingine yanaweza kupunguza hamu












