Tiba ya majaribio ya saratani ya matiti 'ilivyomaliza saratani'

Mwanamke mwenye saratani aliyeambiwa ataishi chini ya mwaka mmoja aliambiwa kuwa ugonjwa umeisha baada ya kushiriki majaribio ya tiba.

Jasmin David, mwenye umri wa miaka 51, mkazi wa Manchester, alipatikana na saratani ya matiti inayosambaa haraka mwaka 2017.

Miaka miwili baadaye saratani ilikuwa imesambaa na ndipo alipoanza majaribio, akitumia dawa za majaribio pamoja na dawa za kumuongezea kinga ya mwili, katika hospitali ya Christie.

Alisema alihisi kana kwamba "amezaliwa upya" baada ya uchunguzi kuonesha kuwa hakuna ushahidi wa saratani.

Christie alisema Bi David alipata uvimbe juu ya chuchu mwezi wa Novemba 2017.

Alifanyiwa matibabu ya mionzi na mastectomy mwezi Aprili 2018, kufuatia mizunguko 15 ya mionzi ambayo yalimaliza saratani katika mwili wake.

Lakini mwezi Oktoba mwaka 2019 saratani ilirejea, na uchunguzi ukaonesha ilikuwa imesambaa hadi katika mapafu, na mifupa na aliambiwa alikuwa amepewa matibabu duni.

'Athari za kuogofya'

Miezi miwili baadaye, mama huyo wa watoto wawili alijitolea kufanyiwa katika hospitali ya Christie ambapo alifanyiwa majaribio ya tiba pamoja na Atezolizumab, ambayo ni dawa ya kumuongezea kinga ya mwili.

Madaktari wamemwambia kwamba kwa sasa haonyeshi ushahidi wa ugonjwa.

"Wakati nilipopewa ofa ya kufanyiwa majaribio sikujua iwapo itanisaidia, lakini nilidhani walau ninaweza kufanya kuwasaidia wengine na kutumia mwili wangu kwa ajili ya kizazi kijacho," Bi David anasema.

"Mara ya kwanza nilikuwa na athari nyingi za kutisha ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa na kupanda kwa viwango vya joto mwilini, kwahiyo nilikuwa hospitalini wakati wa Krismasi na nilikuwa na hali mbaya sana. Halafu nashukuru nilianza kupata kuhisi vizuri kutokana na tiba.

"Miaka miwili na nusu iliyopita nilidhani ilikuwa mwisho na ninahisi kama nimezaliwa upya."

Bi David aliiambia BBC Radio Manchester kuwa: Niko hapa ninaishi kutokana na Christie na utafiti wa tiba ."

Alisema baada ya kurejea kutoka India kumtembelea mama yake mwenye umri wa miaka 97 katika mwezi Aprili akaamua kustaafu mapema na "kuishi maisha yangu nikimshukuru Mungu na sayansi ya tiba".

Bi David alisema kuwa alikuwa na "hisia" za kurejea kutoka India na kupata "taarifa njema’’ baada ya kupita miaka miwili kabla ya kumwambia kwaheri.

Matibabu ya majaribio ya tiba yataendelea hadi Disemba 2023.

Profesa Fiona Thistlethwaite, daktari wa tiba ya saratani na Mkurugenzi wa kliniki katika The Christie, ambaye amekuwa akiongoza majaribio, alisema: "Inafurahisha kwa kila mtu unapoona mtu anapona kama inavyokuwa kwa Jasmin."