Madhila ya kila siku ya kuishi katika nchi iliyofilisika

Nchini Sri Lanka kwa sasa, unahangaika hata kabla uamke. 

Kukatika kwa umeme kunakochelewa hadi usiku mwingi huiba saa za usingizi huku feni zikikoma; familia nzima zilizoamka zikiwa zimedhoofika kutokana na kesi iliyodumu kwa miezi kadhaa ya kusawazisha maisha yao kutokana na kukatika kwa umeme kila siku baada ya nchi kufilisika na kukosa mafuta.

Kuna siku ndefu za kuishi; siku za kazi, safari za kuendeshwa, vitu muhimu vya kila siku vya kununuliwa kwa bei mara mbili ya bei ilivyokuwa mwezi uliopita. 

Haya yote, unaanza kuvunjika zaidi kuliko ulivyokuwa wiki iliyopita.

Mara tu unapopata kifungua kinywa - kula kidogo kuliko ulivyokuwa ukifanya, au labda bila kula chochote - vita vya kutafuta usafiri vinakungoja.

Katika miji, foleni za mafuta huzunguka vitongoji kama vile chatu wakubwa huwa zaidi na kuongezeka siku hadi siku, hali ambayo inaathiri riziki watu.

Madereva wa Tuk-tuk wakiwa na matangi yao ya lita nane wanalazimika kutumia siku kupanga foleni kabla ya kuandesha shughuli zao tena, kwa saa 48 labda, kabla ya kulazimishwa kujiunga tena na foleni, kuleta mito, mabadiliko ya nguo na maji ili kuwaona shida.

Kwa muda, watu wa tabaka la kati na la juu walikuwa wameleta pakiti za chakula na vinywaji baridi kwa wale waliokuwa wakipanga foleni katika mitaa yao.

Hivi karibuni gharama za chakula, gesi ya kupikia, nguo, usafiri, na hata umeme ambao serikali itakuwezesha kuwa nao, imepanda sana huku thamani ya Rupia ikiporomoka, kiasi kwamba hata pesa nyingi kutoka kwa wenye fedha zimekuwa haba.

Katika makazi yaliyo na watu walio na ajira, wafanyakazi na familia zimeanza kuungana kupika pamoj kwa kutumia jiko la kuni, kuandaa milo rahisi zaidi - wali, na samboli ya nazi.

Hata dhal, chakula kikuu kote Asia Kusini, imekuwa anasa. Nyama? Kwa mara tatu ya bei ilivyokuwa? Sahau.

Samaki hapo awali walikuwa wanapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu. Sasa, wavu haziwezi kwenda baharini, kwa sababu boti hazina dizeli. 

Sri Lanka: Ya Misingi

  • Sri Lanka ni taifa la kisiwa kutoka kusini mwa India: Ilipata uhuru kutoka kwa utawala wa Uingereza mwaka 1948. Wasinhala, Watamil na Waislam - ambao wanachangia 99% ya wakazi milioni 22 wa nchi hiyo.
  • Kina kaka wa familia moja imetawala nchi hiyo kwa miaka mingi: Mahinda Rajapaksa alikua shujaa kati ya Wasinhali walio wengi mwaka wa 2009 wakati serikali yake ilipowashinda waasi wanaotaka kujitenga wa Kitamil baada ya miaka mingi ya vita vikali na vya umwagaji damu vya wenyewe kwa wenyewe.
  • Kaka yake Gotabaya, ambaye alikuwa waziri wa ulinzi wakati huo, ndiye rais wa sasa lakini anasema anajiuzulu.
  • Sasa msukosuko wa kiuchumi umesababisha ghadhabu mitaani: Kupanda kwa mfumuko wa bei kumesababisha baadhi ya vyakula, dawa na mafuta kukosekana, kuna uhaba wa umeme na watu wa kawaida wameingia mitaani kwa hasira huku wengi wakilaumu familia ya Rajapaksa na serikali yao kwa hali hiyo.

Wengi wa watoto wa Sri Lanka sasa wamelazimika kuishi kwa lishe isiyo na virutubisho kamili. Huu ni mzozo ambao umeathiri kila ngazi ya maisha kutoka kwa uchumi mkuu hadi wa molekuli.

Je, ubongo wa watoto, viungo vyao, misuli yao, mifupa yao, wanapata kile kinachohitajika? maziwa ya unga, ambayo nyingi huagizwa kutoka nje, haijaonekana kwenye rafu za soko kwa miezi kadhaa.

Umoja wa Mataifa sasa unaonya juu ya utapiamlo na mgogoro wa kibinadamu. Kwa wengi hapa, mgogoro umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa.