Unajua wewe ni kizazi gani? Millennials, Baby Boomers au Gen Z?

s

Chanzo cha picha, Google AI Studio

Muda wa kusoma: Dakika 4

Najua umeyaona na kuyasikia maneno haya: millennials ni wavivu, Baby Boomers wana mali nyingi, na Generation Z wanatumia muda mwingi zaidi na simu zao kuliko familia zao. Lakini kweli maneno haya yanamaanisha nini, na je, mitazamo inayohusishwa na vizazi hivi ina ukweli wowote ndani yake?

Dk. Alexis Abramson, mtaalamu wa "generational cohorts" (vizazi vinavyotambuliwa), anasema tunagawanya vizazi kwa sababu: "Mwaka ulipozaliwa mtu unaathiri mitazamo yake, maadili yake, mtazamo wake, na tabia zake." Hii inamaanisha kila kizazi kina sifa zake za kipekee.

Duniani kuna kama vizazi 8 vinavyotambulika.

The Greatest Generation -au GI Generation (Waliozaliwa 1901–1927)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kizazi hiki cha GI kinapotea sasa, waliosalia ni wachache na watu wazima sana

Kizazi kinachojulikana kama The Greatest Generation (au GI Generation) waliishi kipindi cha uchumi uliyoyumba zaidi duniani na baadaye wakaenda kupigana katika vita kuu ya pili ya dunia.

Hawa ni maarufu pia kwa muziki wa jazz na swing, lakini usidanganyike na misisimko ya utamaduni wa wakati huo, pamoja na hayo yote, changamoto za maisha waliyopitia, ikiwemo kulea familia katika mazingira magumu, ziliwafanya kuthamini sana sifa kama kufanya kazi kwa bidii, ustahimilivu na moyo wa kupambana. Ni kizazi cha kina Jomo Kenyatta (1897 – 1978) rais wa kwanza Kenya, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza Tanzania aliyezaliwa mwaka 1922, akiwa watoto wa mwishoni kuzaliwa kwenye kizazi hivi.

Silent Generation (1926–1945)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Hili ndilo kizazi cha pili Kinachojulikana kizazi che hekaheka za vita. Wanarejea waliokulia wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Jina "Silent" lilitokana na makala ya Time magazine katika miaka ya 1950, likimaanisha watoto wa kizazi hiki walifundishwa kuwa "waonekane na si kusikika." Sifa zao ni: Nidhamu, watiifu na wenye maadili

Wanapendelea mawasiliano ya ana kwa ana badala ya kutumia teknolojia.

Baby Boomers (1946–1964)

d

Chanzo cha picha, Getty Images

Kizazi hiki kimefafanuliwa na shirika rasmi la serikali ya Marekani, US Census Bureau. Jina linatokana na kuongezeka kwa idadi ya watoto baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Sifa zao ni: Wenye kujitolea, kujitegemea na wenye ushindani mkubwa (labda kutokana na wingi wa watu katika kizazi hiki).

Hapa na kizazi kinachofuata ndipo viongozi wengi wa sasa wa Afrika wapo, kina Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania), aliyezaliwa mwaka 1960, Jenerali Twaha Ulimwengu ni sehemu ya kizazi hiki, alikuwa kinara wa wabunge wa Tanzania walioidai Tanganyika walioitwa G-55.

Kizazi ama Generation X (1966–1980)

Waliokulia wakati teknolojia ilikua haraka, lakini haikuwa rahisi kupata kama ilivyo leo. Wanaelewa dunia ya kidijitali na ile ya "kawaida." Sifa zao ni: Wenye ubunifu, wenye mantiki, wenye ujuzi wa kutatua matatizo. William Ruto wa Kenya (1966) ni wa kizazi hiki.

Millennials (1980–1995)

A
Maelezo ya picha, Kizazi hiki cha Millennials kimekutana uhalisia na na mwanzo wa teknolojia

Hili ndilo kizazi ambacho kimeshikiliwa sana katika vyombo vya habari. Wanaonekana "wavivu" kwa baadhi ya watu, wakitumia pesa zaidi kwenye starehe kuliko kuokoa kwa nyumba, lakini pia ndilo kizazi cha kwanza "digital natives" - wanatumia teknolojia kufanikisha maisha yao.

Sifa zao ni kujiamini, udadisi na kuuliza maswali kwa mamlaka (ambayo vizazi vya zamani vinaweza kuona ni jambo baya kuhoji)

Kizazi Z au Gen Z (1997–2012)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Waliokulia wakiwa na teknolojia kila mahali, ndio maana pia wanaitwa iGen. Sifa zao ni kujiamini kupita kiasi, watoto wa kidijitali na wenye malengo na matamanio makubwa na ya haraka. Hiki ndicho kizazi kinachofanya maandamano sana sasa duniani.

Vilevile, Dk. Abramson anasema: Ingawa kugawanya vizazi kunasaidia, hatuwezi kuelewa zaidi ukamilifu wake kupitia kizazi kimoja. Ni sawa na masuala ya nyota (astrology) unaweza kujitambua na baadhi ya sifa za alama ya nyota, lakini huwezi kufanana kabisa na kinachoelezwa kinyota. Hivyo pia kwa vizazi; ikiwa vizazi vinapewa sifa hasa kwenye vyombo vya habari, watu wanaweza kujipa na kujiweka ndani ya sifa hizo.

Silent Generation na Baby Boomers kwenye mawasiliano walitegemea mahusiano ya ana kwa ana, na hivyo wanajihusisha zaidi na jamii zao halisi. Vizazi vya vijana wanaunda jamii zao mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii. Tofauti hizi zinaweza kusababisha migongano, hasa kazini: wazee wanaweza kukasirika wakiona vijana wanapendelea kutuma ujumbe badala ya kuuliza maswali uso kwa uso. Pia, vijana wanaona wazee wamepitwa na teknolojia.

Ufumbuzi, Dk. Abramson anasema, ni kwamba "vizazi vya vijana vinaweza kufundisha vizazi vya wazee, na vizazi vya wazee vinaweza kufundisha vijana." Hii inamaanisha uhusiano wa 'mentor-mentee' unaweza kwenda kwa pande zote. Kwa mfano, vijana wanaweza kufundisha teknolojia mpya, huku wazee wakifundisha uzoefu na maarifa ya muda mrefu kazini.

Kizazi cha Alpha- Gen A' (2010-2024)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Kizazi kijacho ni Generation Alpha, hiki ni kile kinachokomaa sasa kilichozaliwa kuanzia 2010. Wanaotarajiwa kuwa na uhusiano wa karibu wa kifamilia na kuwa "watumwa wa digitali" zaidi kuliko vizazi vyote vilivyopita. Pia, Dk. Abramson anasema vizazi hivi vinaashiria mabadiliko makubwa: jamii haitakuwa na utofauti mkubwa wa kijinsia, rangi, au mitazamo ya kijamii, na itakuwa huru zaidi.

Kwa ujumla, kugawanya vizazi kunasaidia kuelewa tofauti za mitazamo, tabia, na mahitaji ya kila kundi, lakini hatuwezi kufafanuliwa kikamilifu na kizazi kimoja pekee.

Kizazi Beta - waliozaliwa kuanzia 2025

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Kizazi Beta kinarejea kundi la watu watakaozaliwa kati ya mwaka 2025 hadi 2039, baada ya kizazi Alpha waliozaliwa mpaka 2024. Kizazi hiki kinatarajiwa kukua kikiwa kimeunganishwa kwa kiwango cha juu na teknolojia na akili bandia (AI) tangu kuzaliwa, kikikulia katika mazingira ambayo vitu kama magari yanayojiendesha yenyewe vitakuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Pia watakabiliwa na changamoto kubwa, ikiwemo mabadiliko ya tabianchi.