Mbuzi wanaokabiliana na moto wa porini Marekani

Mbuzi wa malisho wamekuwa jambo la kawaida huko Los Angeles - je, suluhisho hili la kale la moto wa nyikani linaweza kuzuia miali mikubwa zaidi na mioto mikali?

Hawa sio tu mbuzi wa kawaida - ni silaha mpya ya siri ya California katika vita dhidi ya moto wa nyikani, na wanapelekwa nyikani kulisha kalika jimbo zima.

"Mapokezi ni mazuri sana popote tunapokwenda," anasema mchungaji wa mbuzi Michael Choi. "Ni hali ya kushinda-kushinda kadiri ninavyoweza kusema."

Choi anaendesha Fire Grazers Inc, biashara ya familia ambayo hukodisha mbuzi kwa wakala wa jiji, shule na wateja wa kibinafsi ili kusafisha miteremko ya milima na ardhi ambayo ni ngumu kufikiwa. Kampuni hiyo ina mbuzi 700, na hivi majuzi walilazimika kupanua kundi lao ili kuendana na mahitaji.

"Nadhani watu wanapofahamu zaidi wazo hilo, na athari za kimazingira, wanakuwa na ufahamu zaidi kuhusu mbinu wanazotaka kutumia kwa ajili ya kuondoa magugu na kulinda mazingira dhidi ya moto. Kwa hiyo, kwa hakika kuna mahitaji makubwa zaidi, na ni mwelekeo unaokua. ," anasema.

California imekuwa tovu cha mapambano dhidi ya moto wa nyikani, ambao umekuwa ukizuka mara kwa mara, kusababisha uharibifu mkubwa tangu 1980. Mnamo 2021, California ilikabiliwa na hali ya moto "isiyo na kifani", kulingana na CalFire (Idara ya California ya Misitu na Ulinzi wa Moto ya serikali ya jimbo), huku moto mmoja pekee ukiteketeza zaidi ya ekari 960,000 (kilomita za mraba 3,885). Mvua za wakati unaofaa zinaweza kuleta ahueni, hata kama hali ikiwa mbaya. Msimu wa moto wa porini mnamo 2022 ulielezewa kuwa "mdogo" kwa serikali - zaidi ya ekari 300,000 (km 1,214 za mraba) ziliteketezwa ikilinganishwa na wastani wa miaka mitano wa ekari milioni 2.3 (km 9,307 za mraba).

Mwaka huu, mwezi Agosti ilikuwa baridi na mvua kuliko wastani huko California. Bado, zaidi ya robo ya ekari milioni zimeungua, na watu wanne walifariki.

Tofauti na mbuzi wengine, mbuzi hawa wana midomo nyembamba, yenye kina ambayo huwaruhusu kulisha vichaka vya miti bila wasi wasi. Wanasimama kwa miguu ya nyuma na kufikia urefu wa wastani wa 6.7ft (2m), na wana ndimi na midomo ya ustadi.

"Pia wana uwezo wa kuondoa sumu mwilini na hivyo wanaweza kula mimea yenye sumu," Launchbaugh anaongeza.

Mambo kama vile hali ya joto, ukame zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ni vichochezi muhimu katika kuongeza hatari na ukali wa moto huo, utafiti unaonyesha.

Lakini pia kuna tafiti zinazoashiria kwamba usimamizi wa ardhi unaweza kuwa na jukumu muhimu, kwani mrundikano wa miti iliyokufa na vichaka kavu vinachochea hatari ambayo inaweza kusababisha moto mkubwa, mkali.

Wasimamizi wa ardhi tangu jadi walitegemea dawa za kuulia magugu na kazi ya mikono kupunguza vichaka, lakini mashirika na maafisa wa jiji pia wanajaribu mbinu zingine, zinazoweza kuwa endelevu na za gharama nafuu - kama vile mbuzi.

"Mbuzi ni muhimu sana katika maeneo kama California na Mediterania kwa sababu ya vichaka - mbuzi wana vifaa vya kutosha kwa hilo, wana midomo sahihi," anasema Karen Launchbaugh, profesa wa ikolojia katika Chuo Kikuu cha Idaho ambaye amefanya tafiti nyingi juu ya malisho ya kondoo, mbuzi na ng'ombe. "Wameumbwa kula vichaka."

Launchbaugh anasema anaona maafisa zaidi wa jiji na wasimamizi wa ardhi wakiwa tayari kujaribu mbuzi kama mbinu mpya ya kupunguza hatari ya moto wa nyika. "Nimefurahi kwa sababu tulipoanza kutafiti hili, hatukujua lingefika wapi. Na sasa kuna kazi ya kutosha kwa ajili ya watu kujikimu kutokana na malisho - na miji na kaunti ziko tayari kulipia kwa sababu wanajua inaleta mabadiliko."

Mbuzi wana hamu ya kutoshiba, na hula magugu, vichaka, majani yanayoning'inia- yote hii kuni zinazochochea moto.

Mwongozo wa kujiandaa kwa moto wa nyika wa California unaelekeza wakazi kuondoa mimea iliyokufa, na kukata nyasi hadi inchi nne (10cm) - kila kitu ambacho mbuzi angefanya kwa kawaida, kwa shauku, na bila kukumbushwa. Mbuzi pia hawasumbuki kilisha kwenye hali ya joto ya hadi nyuzi joto la (37.7C na zaidi.

Katika jiji la Glendale, jimbo la Los Angeles, mbuzi 300 wanafanya kazi kwa bidii kwenye matuta ya Milima ya Verdugo, wakifyeka ekari 14 (hekta 5.6) katika muda wa wiki mbili.

Jiji limeainishwa kama eneo la "hatari kubwa sana ya moto". Ili kupunguza hatari hiyo, Patty Mundo, mkaguzi wa usimamizi wa mimea wa Idara ya Moto ya Glendale, ametumia mbuzi wa Choi tangu 2018.

Madhumuni yao ni kuunda eneo salama kati ya nyumba na maeneo wazi ya ardhi ili kupunguza kasi ya moto endapo utazuka. - au hata kuzui kabisa. Kuwa na eneo salama husaidia kulinda nyumba dhidi ya moto, muhimu katika hali ambapo zaidi ya jamii 60,000 ziko hatarini kutokana na moto wa nyika.

Huko Sacramento Magharibi, mifugo ya mbuzi imetumika tangu 2013 katika hatua za kuzuia moto kama "njia ya ubunifu na endelevu ya mazingira" ili kudhibiti moto, anasema Jason Puopolo, msimamizi wa shughuli za mbuga za jiji.

Mbuzi huja mjini mara mbili kwa mwaka - mara moja katika chemchemi ili kulisha nyasi zilizomea kutokana mvua za msimu wa baridi, na mara moja katika msimu wa vuli ili kulisha kwenye vichaka kavu.

Msimu uliopita jiji lililipa kampuni ya kuchunga mbuzi ya Western Grazers jumla ya $150,000 kufanya kazi ya shamba hilo.

Kazi ngumu ya mbuzi hao imezaa matunda kiasi kwamba shirika la zimamoto jijini humo lilitoa sifa kwa mifugo kwa kusaidia kuzima moto wakati wa moto wa 2022, kuokoa makazi tata.

“Mkuu wetu wa zimamoto alisema ikiwa mbuzi hawangelisha uwanjani hapo awali, moto ungekuwa mbaya zaidi,” Puopolo anaendelea.

Mbuzi pia ni muhimu linapokuja suala la kudhibiti spishi vamizi, kama vile mimea ya haradali nyeusi isiyo ya asili.