Unaweza kuzitambua video zilizotengenezwa kwa AI?

s

Chanzo cha picha, Serenity Strull/Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 6

Kwa kuwa mitandao yako ya kijamii imefurika video zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba almaarufu AI, kuna zana ya bure inayoweza kukusaidia kubaini video hizi.

Sasa swali ni: je, nitazitambuaje? Zinaonekana kuwa picha zenye ubora duni?

Basi hilo limepata jibu.

Huenda tayari umeshadanganyika kupitia video zilizotengenezwa na AI, au labda umewahi kukaribia kudanganywa.

Katika miezi sita iliyopita, zana za kiteknolojia za kutengeneza video kwa AI zimeboreshwa sana kiasi kwamba uhusiano wake na kamera unaanza kupotea, kiasi cha kuweza kukufanya mara kwa mara kukutana na video bandia na umechoka kuhoji kila unachokiona.

Hata hivyo kwa sasa, kuna ishara fulani zinazoweza kutuonesha ikiwa video husika imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya AI.

Mojawapo ya ishara za wazi ni pale unapoona video yenye ubora hafifu iwe yenye ukungu, au ukijani hilo linapaswa kukupa tahadhari kwamba huenda unatazama video ya AI.

"Hili lilikuwa miongoni mwa mambo ya awali kufanyia uchunguzi," alisema Hani Farid, profesa wa sayansi ya kompyuta katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley, anayejihusisha na uchunguzi wa data kidijitali na mwanzilishi wa kampuni ya GetReal Security.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ukweli ni kwamba tutarajie zana za kutengeneza video kwa AI kuendelea kuboreshwa, na mapendekezo haya yatapoteza maana hivi karibuni.

Hilo linaweza kutokea katika miezi au miaka michache ijayo.

Ni vigumu kubashiri , lakini ukifuata mwongozo huu, huenda ukajiepusha na baadhi ya video bandia hadi ujifunze kubadili mtazamo wako kuhusu uhalisia.

Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba ubora wa video si ushahidi tosha kuwa video umetengenezwa na AI.

Video za AI si zote zinazoonekana mbaya, na zana nzuri zinaweza kuzifanya zionekane halisi zaidi.

Hivyo basi, video yenye ubora duni si lazima iwe ya AI. "Uonapo video yenye ubora wa chini sana, haimaanishi kuwa ni bandia, wala ya uongo," alisema Matthew Stamm, profesa na mkuu wa Maabara ya Usalama wa taarifa katika Chuo Kikuu cha Drexel nchini Marekani.

Lakini hoja kuu ni kwamba video za AI zilizofifia,au zenye ukungu zina uwezekano mkubwa wa kukudanganya kwa sasa.

Hii ni ishara kwamba unapaswa kuchunguza kwa umakini zaidi kile unachokitazama.

s

Chanzo cha picha, Serenity Strull/Getty Images

"Programu za maandishi hadi video kama vile Veo ya [Google] na Sora ya OpenAI bado hutoa video zenye kutofautiana kidogo," Farid alisema. "Lakini si rahisi kubaini kama maandishi yasiyoeleweka. Imejificha zaidi ya hapo."

Pia unaweza kusoma

Hata mifumo ya kisasa zaidi katika wakati huu inakabiliwa na changamoto, kama vile mitindo yenye utofauti au inayobadilika hasa katika nywele na mavazi, au vitu vidogo vya mandhari ya nyuma vinavyotembea isivyo kawaida au visivyo akisi ukweli.

Haya yote ni rahisi kupuuza, lakini kadiri picha inavyokuwa wazi, ndivyo unavyoweza kugundua dosari za AI.

Hayo ndiyo hufanya video iliyotengenezwa kwa ubora wa chini kuvutia sana. Kwa mfano, unapoitaka AI kupiga picha kitu kinachoonekana kama kilichorekodiwa kwenye simu ya zamani au kamera ya usalama, inaweza kuficha mambo ambayo yanaweza kuwapotosha watu.

Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, video kadhaa za AI zilizotengenezwa kwa hadhi ya juu zimewahadaa mamilioni ya watu, ambazo zote zina vitu vilevile: video bandia lakini nzuri ya sungura akiruka na kuvutia zaidi ya watazamaji milioni 240 kwenye TikTok, na mamilioni ya watumiaji wa mtandao kuvutiwa na kipande cha watu wawili walioonekana kupendana kwenye treni ya chini ya ardhi Jijini New York, lakini kujikuta wakisikitika baada ya kugundua kuwa ni bandia.

Mimi binafsi nilishangazwa na video iliyosambaa ikimuonesha mchungaji wa Marekani katika kanisa la kihafidhina akitoa mahubiri ya kushangaza ya mrengo wa kushoto.

"Ni mabilionea wachache pekee tunaopaswa kuwaogopa," alipiga kelele kwa lafudhi ya kusini. "Wana nguvu ya kuiharibu nchi hii!" Nilishangaa. Je, mipaka yetu ya kisiasa ni finyu kiasi hicho? Hapana, kuna video nyingi tu zilizotengenezwa kwa AI.

Hupaswi kufikiri kwamba ujumbe huu ni kweli kwa sababu tu mtu aliuandika. Unapaswa kujaribu kutafuta chanzo cha taarifa hiyo. Video za zamani zilikuwa na utofauti kwa sababu mara nyingi zilikuwa na ugumu ngumu kuiga, lakini zama hizo sasa zimekwisha.

Video zote zinaonekana kupigwa picha katika ubora wa kiwango cha chini, kama video ya sungura wa AI zimetengenezwa kuonekana kama picha za viwango vya kawaida za CCTV zilizopigwa usiku.

Kuhusu video ya wapenzi wanaosafiri katika treni ya chini ya ardhi, upigaji picha umezimwa.

Vipi kuhusu video ya mhubiri wa kufikirika? Video inaonekana kukuzwa sana, na inaonekana kuna vipengele vingine muhimu katika video.

"Mambo matatu ya kuangalia ni ubora, na urefu," Farid anasema.

Urefu ndio rahisi zaidi. "Mara nyingi, video za AI ni fupi sana, fupi zaidi kuliko video za kawaida unazoziona kwenye TikTok au Instagram, ambazo zina urefu wa takriban sekunde 30 hadi 60.

Video nyingi ninatengenezwa kwa AI zina urefu wa sekunde sita, nane, au 10." Hiyo ni kwa sababu video za AI ni ghali kuzitengeneza, kwa hivyo zana nyingi hutumia video fupi sana.

Zaidi ya hayo, kadiri video inavyokuwa ndefu, ndivyo uwezekano wa AI kufanya makosa unavyoongezeka.

"Unaweza kuunganisha rundo la video za AI, lakini utagundua namna ilivyokatwa katika kila baada ya sekunde nane hivi."

Vipengele vingine viwili ni ubora na uthabiti.

Ingawa hizo mbili zinahusiana, ni tofauti. Uthabiti unarejelea idadi au ukubwa wa picha, huku mkazo huwekwa katika mchakato unaopunguza ukubwa wa faili la video kwa kupunguza baadhi ya maelezo, mara nyingi huacha mifumo iliyozuiliwa na kingo zilizofifia.

Kwa kweli, Farid anasema, video bandia zenye ubora mdogo zinavutia sana kiasi kwamba wahalifu hushusha kiwango cha kazi zao kimakusudi.

"Ikiwa najaribu kuwadanganya watu, nifanye nini? Ninatengeneza video bandia na kupunguza ubora ili uweze kuiona, uweze kubaini maelezo kidogo. Kisha ninaongeza mgandamizo ili kuficha mabaki yoyote," Farid anasema. "Hii ni mbinu ya kawaida."

s

Chanzo cha picha, Serenity Strull/Getty Images

Maelezo ya picha, Picha zenye ubora wa kiwango cha chini zina pikseli chache, lakini zote huficha mambo ambayo hurahisisha kutofautisha video zinazotengenezwa na AI.

Lakini tatizo ni kwamba, unaposoma haya, makampuni makubwa ya teknolojia tayari yanatumia mabilioni ya dola kufanya AI iwe ya kweli na halisi zaidi.

"Nina taarifa mbaya kwako. Ikiwa picha hizo zinaonekana sasa, hazitatokea hivi karibuni," Stamm alisema. "Ninatarajia alama hizi zitatoweka zisionekane kwenye video ndani ya miaka miwili, na zile zilizo wazi, kwa sababu zimetoweka kabisa kutoka kwenye picha zinazotengenezwa kwa AI. Huwezi kuamini macho yako."

Hiyo haimaanishi kwamba ukweli umepotea. Watafiti kama Farid na Stamm wanapochunguza maudhui, wana mbinu za hali ya juu zaidi.

"Unapounda au kuhariri video, huacha nyuma alama ndogo za taarifa ambazo macho yetu hayawezi kuona, sawa na alama za vidole katika masuala ya uhalifu," Stamm anasema.

"Tunashuhudia kuibuka kwa mbinu ambazo zinaweza kusaidia kufichua alama hizi za vidole." Wakati mwingine, usambazaji wa pikseli katika video bandia unaweza kutofautiana na video halisi, lakini hata mambo haya si ya kupuuza.

Kampuni kadhaa za teknolojia zinaendeleza viwango vipya vya kuthibitisha taarifa za kidijitali.

Kimsingi, kamera zinaweza kuingiza taarifa kwenye faili mara tu zinapoundwa, na kusaidia kuthibitisha kuwa ni halisi. Vile vile, zana za AI zinaweza kuongeza maelezo sawa kwenye video na picha ili kuthibitisha kuwa ni bandia.

Stamm na wengine wanasema juhudi hizi zinaweza kusaidia.

Mtaalamu wa elimu ya kidijitali Mike Caulfield anasema suluhisho halisi ni sisi sote kuanza kufikiria tofauti kuhusu kile tunachokiona mtandaoni.

Kuangalia vidokezo vilivyoachwa na AI si ushauri "endelevu" kwa sababu vinabadilika kila mara.

Caulfield anasema hatupaswi kudhani video au picha yoyote ina maana yoyote bila kujali muktadha.

"Mtazamo wangu ni kwamba video kwa kiasi kikubwa itakuwa kama maandishi mwishowe, ambapo chanzo [cha video] kitakuwa jambo muhimu zaidi, si sifa za juu juu, na tunapaswa kuwa tayari kwa hilo," Caulfield alisema.

"Nikizidisha taarifa kidogo, nadhani hii ndiyo changamoto kubwa zaidi ya usalama wa taarifa katika karne ya 21," Stamm alisema.

"Lakini imekuwapo kwa miaka michache tu. Idadi ya watu wanaoifanyia kazi ni ndogo, lakini inakua kwa kasi. Tunahitaji kupata suluhisho, elimu, sera bora, na mbinu shirikishi ya teknolojia. Siko tayari kukata tamaa bado," alihitimisha.