Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mabaki ya ndege ya kivita ya Marekani iliyopotea yapatikana
Maafisa wa kijeshi wamepata vifusi vya ndege ya kijeshi ya F-35 ambayo ilitoweka baada ya rubani kutupwa Carolina Kusini.
Mabaki ya ndege hiyo yenye thamani ya dola milioni 100 - ambayo ilitoweka Jumapili alasiri - yalipatikana katika eneo la mashambani katika kaunti ya Williamsburg, mamlaka zilisema.
Rubani alitoka kwenye chumba cha rubani na kutua kwenye eneo salama katika kitongoji cha North Charleston kwa kutumia mwavuli.
Watu walikuwa wameombwa kusaidia kutafuta ndege hiyo.
Katika taarifa siku ya Jumatatu, maafisa wa kijeshi mabaki hayo yalipatikana "saa mbili kaskazini-mashariki mwa Kituo cha Pamoja cha Charleston".
Maafisa walikuwa wameelekeza utafutaji wao karibu na Ziwa Moultrie na Ziwa Mabaki yaliyopatikana yamethibitishwa kuwa ya ndege iliyotoweka, msemaji wa jeshi aliambia BBC.
"Hitilafu hiyo kwa sasa inachunguzwa, na hatuwezi kutoa maelezo ya ziada ili kuhifadhi uadilifu wa mchakato wa uchunguzi," Kikosi cha Wanamaji kilisema Jumatatu baada ya shughuli ya kuitafuta kukamilika.
Ndege hiyo ya kivita iliachwa katika hali ya kujiendesha yenyewe wakati rubani alipokimbilia usalama, msemaji waKituo cha pamoja cha kijeshi mjini Charleston aliiambia NBC News, na kuongeza kuwa huenda ilikuwa imeruka kwa muda, na hivyo kutatiza ugunduzi wake.
Ndege aina ya FB-35B Lightning II, ilikuwa ya Kikosi cha Mafunzo ya Mashambulizi ya Marine Fighter Attack Squadron 501, ambacho kinafanya kazi ya kutoa mafunzo kwa marubani, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti.
Rubani aliyetolewa alipelekwa hospitalini na alikuwa katika hali nzuri.
Ndege ya pili ya F-35 iliyokuwa ikiruka wakati huo huo ilirudi salama kwenye kituo cha Charleston, msemaji wa jeshi Maj Melanie Salinas aliambia Associated Press.
Imetengenezwa na Lockheed Martin na inafikiriwa kugharimu karibu $80m (£65m) kila moja, na ni mojawapo ya ndege za kivita zenye teknolojia ya juu zaidi duniani.
F-35 ndio mradi kubwa zaidi na ghali zaidi ya silaha za aina yake ulimwenguni.
Mnamo mwaka wa 2018, jeshi la Marekani lilisitisha kwa muda ndege zake zote za kivita za F-35 baada ya ajali huko South Carolina.
Joint Base Charleston alikuwa amechapisha kwenye X - zamani Twitter - akiomba umma usaidizi wa kupata ndege hiyo.
Ombi hilo lilizua utani mtandaoni na ukosoaji kutoka kwa wabunge.
Nancy Mace, mbunge wa Republican wa Carolina Kusini, aliuliza kwenye X, zamani Twitter: "Je! unapotezaje ndege ya F-35?
"Vipi hakuna kifaa cha kufuatilia na tunauliza umma nini, tafuteni ndege hiyo mkipata muirudishe kituoni"
Mapema Jumatatu, Jeshi la Wanamaji la Marekani lilitangaza kusitisha kwa siku mbili kwa operesheni za anga katika tawi zima la jeshi wiki hii.
Taarifa kwa vyombo vya habari ya Jeshi la Wanamaji Jumatatu ilisema maafisa wanapanga "kujadili masuala ya usalama wa anga na mbinu bora" baadaye wiki hii." Wakati wa zoezi hilo la usalama, makamanda wa anga wataongoza majadiliano na Wanajeshi wao wakizingatia misingi ya uendeshaji salama wa ndege," ilisema. taarifa kwa vyombo vya habari.
Ilisema kuwa ndege iliyopotea ilifikia "ajali ya daraja la tatu" katika wiki sita zilizopita - aina ya tukio ambalo husababisha uharibifu wa zaidi ya $ 2.5m. Haikufafanua matukio yaliyopita.
Mnamo Agosti, Wanamaji watatu walikufa katika ajali iliyohusisha ndege ya Osprey tilt-rotor na Marine mwingine aliuawa wakati ndege yake ilipoanguka wakati wa mazoezi karibu na San Diego.
Mnamo mwaka wa 2018, jeshi la Marekani lilisimamisha kwa muda meli zake zote za ndege za F-35 baada ya ajali huko South Carolina.
Ni nini kinachoifanya ndege ya F-35 kuwa ya kipekee duniani?
Haionekani na maadui. Wakati ndege ya F-35 inaposhiriki katika mazoezi, kawaida huzishinda ndege za adui kwa kiwango cha 20 kwa 1.
Ingefanya vivyo hivyo wakati wa vita dhidi ya wanajeshi wa Urusi au Wachina, kwa sababu iliundwa kunyonya au kupotosha nishati ya rada, kwa hivyo marubani wa ndege za adui hawawezi kuiona kabla haijashambulia.
Kwa kuongezea, F-35 ni ndege ya siri - kumaanisha fremu ya anga, vitambuzi na mifumo imeundwa kufanya kazi bila kutambuliwa na rada ya adui.
Iwapo ndege ilikuwa inaruka kuelekea kwenye njia zilizopangwa awali, eneo lake la ajali huenda lilibainishwa na lini mafuta yake yangeisha.
Kasi inayojulikana na urefu wakati wa kutolewa, pamoja na kiasi gani cha mafuta kilichosalia, kingeweza kuifanya kuwa zoezi rahisi la hesabu ili kubainisha eneo iliyokuwa.F-35 ina mfumo wa hali ya juu ambao unadanganya au kukandamiza rada za adui, angani na ardhini.
Rada hizo zinaweza kugundua kitu kwa mbali, lakini haziwezi kuifuatilia au kuishambulia F-35.
Pia, injini ya ndege hiyo ina uwezo wa kupunguza joto kabla ya makombora yanayotafuta joto kuishambulia.
Ni zaidi ya ndege ya kivita . F-35 sio tu ndege ya kupambana bali pia ni ndege inayoweza kuishi muda mrefu kuwahi kuundwa.
Katika jukumu lake, ina uwezo wa kusafisha anga za ndege za maadui ambazo zinatishia majeshi ya Marekani.