Tetesi za soka Ulaya: Man United inawafukuzia Gallagher na Stiller

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United wanataka kumsajili kiungo wa kati mwezi Januari, ambapo chaguo lao kuu ni Conor Gallagher wa Atletico Madrid (aliyewahi kuchezea Chelsea) mwenye umri wa miaka 25, na Angelo Stiller wa Stuttgart, raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24. (Give Me Sport)

United pia wanavutiwa na mchezaji wa Valencia, Javi Guerra, huku Atletico Madrid na AC Milan nao wakimfuatilia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22. (Fichajes)

United hawawezi kumrejesha mshambuliaji wa Denmark mwenye umri wa miaka 22, Rasmus Hojlund, kutoka kwa mkopo wake huko Napoli mwezi Januari. (Star)

Crystal Palace iko kwenye mazungumzo na kiungo wa England Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 21, kuhusu mkataba mpya baada ya kuanza msimu vizuri. (Give Me Sport)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham bado wanavutiwa kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, na wako tayari kulipa dau la £70 milioni linalohitajika na klabu hiyo ya Hispania kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Fichajes)

Kiungo wa Scotland Scott McTominay anataka Napoli imsajili aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Manchester United, Kobbie Mainoo, mwenye umri wa miaka 20, ambaye kwa sasa hapewi nafasi kwenye kikosi cha Old Trafford. (Sun)

Wolves watamuunga mkono meneja wao mpya anayetazamiwa kuchukua mikoba, Rob Edwards, katika dirisha la usajili la Januari, kwa lengo la kusajili wachezaji chipukizi wa ndani ya Uingereza. (NBC)

Mshambuliaji wa West Ham, Niclas Füllkrug, mwenye umri wa miaka 32, anasakwa na klabu ya Italia AC Milan mwezi Januari, huku West Ham wakifikiria kumruhusu kuondoka kwa mkopo. (Tuttomercatoweb)

Mabingwa wa Denmark Copenhagen wanataka kumsajili beki wa Sweden wa Newcastle, Emil Krafth, mwenye umri wa miaka 31, mwezi Januari. (Shields Gazette)