Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Kiungo wa Man United Kobbie Mainoo avivutia vilabu viwili vya Itali

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kobbie Mainoo
Muda wa kusoma: Dakika 2

Napoli wamefanya mawasiliano na Manchester United kuhusu mkataba wa mkopo wa Januari kwa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mainoo pia anasakwa na klabu nyingine ya Serie A huku Roma ikihitaji mkataba wa Januari. (Soccer Italia)

Kiungo wa kati wa Newcastle na Italia Sandro Tonali anatamani sana kujiunga na AC Milan, huku Juventus pia wakivutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Corriere della Sera - In Itali)

Tonali hana kipengele cha kuachiliwa katika mkataba wake wa Newcastle na atajua mustakabali wake mwaka baada ya mwaka. (Sky Sports)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sandro Tonali

Kiungo wa kati wa Aston Villa na England Morgan Rogers, 23, anatazamiwa kusaini mkataba mpya ambao utafanya mshahara wake kuwa zaidi ya £100,000 kwa wiki. (Mail)

Bayern Munich wanawasiliana na msafara wa mlinzi wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, kuhusu uhamisho unaowezekana. (Bild - via Get German Football News)

Liverpool na Chelsea huenda wakamnunua beki wa Newcastle Mholanzi Sven Botman, 25. {Offside)

Tottenham wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 29, mwezi Januari kutoka klabu ya Al-Ahli ya Saudi Pro League na mkufunzi wa Spurs Thomas Frank tayari amefanya naye mazungumzo. (TeamTalks)

.

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Ivan Toney

Alexis Mac Allister ana furaha akiwa Liverpool na kiungo huyo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 26 hana nia ya kuhama mara moja licha ya kutakiwa na Real Madrid. (Football Insider)

Aliyekuwa kocha mkuu wa Wolves Gary O'Neil anapigania sana kibarua cha meneja katika timu ya Southampton, pamoja na mkufunzi wa zamani wa Middlesbrough Michael Carrick. (Telegraph - Subscription Required)

Liverpool hawana uwezekano wa kuwasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo mwezi Januari, lakini The Reds wanaweza kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 msimu ujao. (Fabrizio Romano via Give Me Sport)

Beki wa Italia Alessandro Bastoni anataka kusalia Inter Milan, uamuzi ambao ni pigo kwa Manchester United, Manchester City na matumaini ya Liverpool kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Fichajes - Spanish)