Biden atakwenda wapi baada ya kuondoka Ikulu?

Chanzo cha picha, Reuters
Daima Joe Biden amekuwa akiyahesbu maeneo mawili kama nyumbani - Ireland na Delaware. Atakapoondoka Ikulu katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo ataelekea Delaware.
Umri wake wa miaka 81 – ulikuwa chanzo cha kuondoka kwenye kinyang'anyiro cha urais baada ya muhula mmoja.
Baba yake Kathy Magner alifanya kazi na baba wa Biden miaka 50 iliyopita na amemjua Biden kwa miongo kadhaa.
"Naamini muda ambao amebakisha baada ya urais, anaweza kuufurahia akijua kuwa alifanya vyema kwa kadiri ya uwezo wake," anasema.
Kathy anasaidia kuendesha Kanisa la Limestone Presbyterian huko Wilmington na moja ya kazi zake ni kuweka ujumbe wenye maana mbele ya jengo hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Siku chache kabla ya uchaguzi, Marekani itakapo amua kati ya Kamala Harris na Donald Trump, ujumbe unasema: 'Kamwe chuki haisuluhishi matatizo. Inayaunda.'
Inaonekana maneno hayo yanaakisi jinsi miezi michache iliyopita mambo yalivyokuwa kuhusu mgawanyiko wa kisiasa.
"Kuna watu katika familia ambao wamekataliana kwa sababu ya tofauti za kisiasa," anasema Kathy.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
“Nina wifi yangu ambaye sizungumzi naye, kwa sababu nikimpigia simu tunaishia kuzozana na nitakata simu tu.
Mwaka jana Limestone Presbyterian aliwakaribisha vijana wa Kikristo kutoka Ireland ya Kaskazini kama sehemu ya mpango wa mjumuiko wa kijamii.
Kasisi wa kanisa hilo anasema ziara hizo zilimpa matumaini kwamba wanaweza kuishinda migawanyiko iliopo Marekani.
Lakini katikati mwa Wilmington, nje ya kituo cha reli kilichopewa jina la Joseph R Biden Jr., ilikuwa wazi kwamba mgawanyiko huo ulikuwepo.
Mfuasi mmoja wa Trump aliniambia Marekani imekuwa mahali pabaya sana kwa sasa kwa sababu ya Biden.
Na nilipomuuliza urais wake utakumbukwa kwa nini, alisema maneno mawili: “Uzee wake.”
Rais anayemaliza muda wake ni mtu anayefahamika hapa. Na mojawapo ya sehemu anazopenda sana kwenda kula ni Charcoal Pit diner.
Ndani ya mkahawa huo wa tangu miaka ya 1950, kuna picha za ziara na Biden na Barack Obama – ambaye Biden alikuwa makamu wake.
Licha ya kuwa mgeni asiyetembelea mara kwa mara katika miaka minne iliyopita, wafanyakazi wa eneo hilo wanasema bado anakuja akichukua chakula anapokuwa Delaware.

"Hula mkate wa nyama na baga. Na aiskrimu," anasema mpishi Lupe Avilez. "Na anazungumza nawe kama anakujua kwa muda mrefu."
Kama ilivyo kwa mke wa Lupe Mary – mwenye asili ya Ireland, anasema mapenzi ya Biden kwa kisiwa hicho yako wazi.
Biden Nchini Ireland

Chanzo cha picha, Getty Images
Ziara ya rais Joe Biden nchini Ireland mwaka jana ilikuwa ya kukumbukwa, ya kibinafsi na ya kisiasa.
Safari hiyo ilikuwa ni sherehe juu ya asili yake lakini pia nafasi ya kusukuma maendeleo ya kisiasa katika Ireland Kaskazini.
Wakati fulani wanasiasa wa Marekani walichanganyikiwa juu ya kura ya watu wenye asili ya Ireland na Marekani. Uchaguzi huu umeonyesha ni kwa kiasi gani umuhimu wao umefifia hadi sasa, huku timu zote mbili za kampeni zikiwa na wasiwasi zaidi kuhusu kupata kura za watu Weusi na Walatino kwenye sanduku la kura.
Wachambuzi wengi wa siasa wanasema kwamba sauti na mijadala ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa Wamarekani wengi wanatazama matatizo yao ya ndani, katika kuamua ni nani anafaa kuwa kiongozi anayefuata.
Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Yusuf Jumah












