Je, Iran inaweza kufunga mkondo wa bahari wa Hormuz, na itaathiri vipi dunia?

    • Author, BBC News Farsça ve BBC Dünya Servisi
    • Akiripoti kutoka, Londra
  • Muda wa kusoma: Dakika 8

Wakati Marekani ikiimarisha uwepo wake wa kijeshi katika Ghuba ya Uajemi, Iran imeonya kuwa mkondo wa bahari wa Hormuz, njia muhimu zaidi ya dunia ya usafirishaji wa mafuta, utalazimika kufungwa endapo vita vitatokea.

Jalal Dehghani Firouzabadi, Katibu wa Baraza la Mahusiano ya Kigeni ya Kimkakati la Iran, alisema kuwa katika tukio la vita, "usalama wa nishati utakuwa hatarini na mkondo wa bahari wa Hormuz utafungwa."

Takriban sehemu moja ya tano ya mafuta ghafi duniani husafirishwa kupitia mkondo huu wa bahari, ambao una upana wa kilomita 40 tu katika sehemu nyembamba zaidi.

Marekani inaendelea kuongeza uwepo wake wa kijeshi katika eneo la Ghuba kutokana na mvutano unaoongezeka kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Mazungumzo kati ya pande hizi mbili yanaendelea, lakini tarehe 9 Februari, Idara ya Usafirishaji ya Baharini ya Marekani ilitoa tahadhari ikiwashauri meli za kibiashara zenye bendera ya Marekani kuepuka maji ya eneo la Iran kadiri iwezekanavyo.

Baada ya tangazo hili, bei za mafuta zilipanda zaidi ya asilimia 1%, kabla ya kushuka kidogo siku iliyofuata.

Wakati mvutano uliokuwa mkubwa katika eneo hili hapo awali, Sir Alex Younger, aliyekuwa mkuu wa Huduma ya Kijasusi ya Kigeni ya Uingereza (MI6), aliwaambia BBC, "Kufunga mkondo wa bahari wa Hormuz kwa hakika kutakuwa tatizo kubwa la kiuchumi, kutokana na athari zake kwenye bei ya mafuta."

Je, ni mafuta kiasi gani yanayopitia mkondo wa bahari wa Hormuz?

Kulingana na kampuni ya uchambuzi wa data, Vortexa, zaidi ya mabareli milioni 20 ya mafuta ghafi, kufanywa zito (kioevu chenye unyepesi wa chini kinachotengenezwa kutoka gesi asilia), na mafuta ya viwandani husafirishwa kupitia mkondo wa bahari wa Hormuz mwaka uliopita kwa wastani wa kila siku.

Hii ni sawa na takriban thamani ya dola bilioni 600 za nishati zinazozungushwa kila mwaka kupitia njia za baharini.

Iran, pamoja na Saudi Arabia, Falme za Kiarabu (UAE), Kuwait, na Iraq, husafirisha mafuta yake mengi kupitia mkondo wa bahari wa Hormuz, hasa kwenda Asia.

Kukatika kwa njia hii kunaweza kusababisha ucheleweshaji mkubwa wa usafirishaji wa mafuta duniani na kupanda kwa bei mara moja.

Hata hivyo, wachambuzi wanatoa tahadhari kuwa matokeo mabaya zaidi yanaweza kuwa ongezeko la mvutano kati ya Israel na Iran.

Veri analiz firması Vortexa'ya göre, Hürmüz Boğazı'ndan geçen yıl, ortalama günde 20 milyon varilden fazla ham petrol, kondensat (genellikle doğal gazdan üretilen düşük yoğunluklu bir sıvı) ve yakıt geçti.

Bu, deniz yolları üzerinden taşınan yıllık yaklaşık 600 milyar dolarlık enerji ticaretine denk geliyor.

İran, Suudi Arabistan, Birleşik Arap Emirlikleri (BAE), Kuveyt ve Irak ile birlikte ham petrolünün büyük kısmını, çoğu Asya'ya olmak üzere, Hürmüz Boğazı üzerinden ihraç ediyor.

Su yolundaki herhangi bir aksama, küresel petrol teslimatında önemli gecikmelere ve fiyatlar üzerinde anında zincirleme etkiye neden olabilir.

Ancak analistler, potansiyel olarak daha ciddi bir sonucun, İsrail ve İran arasındaki gerginliğin artması olacağı uyarısında bulunuyor.

Mkondo wa bahari wa Hormuz ni mwembamba kiasi gani?

Hormuz ni mkondo wa bahari ulioko kati ya Iran na Oman. Upana wake kwenye kuingia na kutoka ni takriban kilomita 50, huku sehemu nyembamba katikati ikiwa takriban kilomita 40.

Hata hivyo, mkondo huu una kina cha kutoshea meli kubwak katika sehemu ya katikati pekee.

Ramani za usafirishaji wa baharini zinaeleza njia salama ya kuingia, njia salama ya kutoka, na eneo salama kati ya hizo, hasa kwa meli kubwa za mafuta.

Kwa jumla, meli kubwa lazima zipitie chaneli yenye upana wa takriban kilomita 10 pekee. Wakati meli zinapoingia Ghuba ya Uajemi, zinakaribia visiwa vya Greater na Lesser Tunb, ambavyo ni maeneo yenye utata kati ya Iran na nchi za Kiarabu.

Kulingana na wataalamu wengi, njia inayowezekana zaidi ya kuingilia usafirishaji wa baharini ni kwa kutumia nguvu za kijeshi. Hii ilitokea wakati wa vita vya Iran na Iraq kati ya 1980 na 1988.

Mfumo wa ulinzi?

Wachambuzi wanasema kufunga mkondo wa bahari wa Hormuz kunachukuliwa kama "kizuizi cha kuonya" kwa Iran, kama vile kumiliki silaha za nyuklia.

Jamii ya kimataifa kwa muda mrefu imekataa mpango wa nyuklia wa kijeshi wa Iran. Nguvu kuu za dunia zimekuwa zikisema kuwa hazitaruhusu Tehran kutumia eneo lake la kimkakati kuvuruga usambazaji wa nishati duniani.

Wataalamu wanakisia kuwa Iran inaweza kufunga mkondo wa bahari wa Hormuz kwa muda mfupi.

Hata hivyo, wengi pia wana uhakika kuwa Marekani na washirika wake wanaweza kurejesha haraka usafirishaji wa baharini kwa kutumia nguvu za kijeshi.

Iran inaweza kufunga mkondo wa bahari wa Hormuz vipi?

Kulingana na ripoti ya 2012 ya Huduma ya Utafiti ya Bunge la Marekani, Iran inaweza kuchukua hatua baada ya hatua katika mkondo wa bahari wa Hormuz:

  • Kutangaza marufuku ya usafirishaji katika mkondo wa bahari wa Hormuz bila kuelezwa wazi madhara ya kukiuka marufuku hayo.
  • Kutangaza kuwa meli zinazopitia mkondo huo zinaweza kukaguliwa au kushikiliwa.
  • Kupiga risasi za onyo kwa meli zinazopita.
  • Kulenga meli fulani kwa nguvu za kijeshi.
  • Kuweka mabomu ya kutega ya baharini (naval mines) katika mkondo wa Hormuz na Ghuba ya Uajemi.
  • Kutumia meli za chini ya maji (submarines) na makombora kulenga meli za kibiashara na kijeshi.

Wakati wa vita vya Iran-Iraq, Iran ilitumia makombora ya Silkworm dhidi ya meli za mafuta na kuweka mitego ya mabomu ya baharini. Moja ya minara hiyo ilipiga USS Samuel B Roberts, na Marekani ikajibu.

Iran haijafanikiwa kufunga Mkondo wa Hormuz kikamilifu, lakini imeongeza sana bima za meli, jambo lililosababisha msongamano kwenye kutoka kwa Ghuba.

Wataalamu wanakisia nini?

Wataalamu wanakadiria kuwa mojawapo ya njia bora zaidi za Iran kuzuia takriban meli 3,000 zinazopitia mkondo wa bahari wa Hormuz kila mwezi ni kwa kuweka mitego ya mabomu kwa kutumia boti za mwendokasi na nyambizi.

Jeshi la majini la Iran na la Revolutionary Guard Corps linaweza kushambulia meli za kigeni za kivita na kibiashara. Hata hivyo, meli kubwa za kijeshi pia zinaweza kuwa nyenzo rahisi kwa mashambulizi ya hewa ya Israel au Marekani.

Boti za mwendokasi za Iran mara nyingi ziko na makombora ya kushambulia meli. Tehran pia ina meli mbalimbali, magari yanayoweza kuzamishwa nusu, na nyambizi.

Hivi sasa, tovuti za ufuatiliaji wa baharini zinazotumia picha za satelaiti zinaonyesha harakati za meli za kijeshi za Iran karibu na mipaka ya baharini ya kusini ya nchi hiyo.

Ni nchi zipi zitaathirika zaidi mlango wa bahari wa Hormuz ukifungwa?

Kulingana na utafiti wa Vortexa, Saudi Arabia husafirisha takriban mabareli milioni 6 ya mafuta ghafi kwa siku kupitia mlango wa bahari wa Hormuz, hii ni zaidi kuliko nchi jirani yoyote.

Kulingana na Idara ya Nishati ya Marekani (EIA), asilimia 84 ya mafuta ghafi yaliyogeuzwa kuwa mazito na asilimia 83 ya gesi asilia iliyosafirishwa kupitia mlango wa bahari wa Hormuz mwaka 2024 ilielekezwa kwenye masoko ya Asia. China, India, Japan, na Korea Kusini ziko miongoni mwa waagizaji wakubwa wa mafuta kupitia mlango huo.

Marekani ilisafirisha takriban mabareli 500,000 ya mafuta ghafi na yaliyogeuzwa kuwa mazito kwa siku kupitia mlango huo mwaka 2024, sawa na asilimia 7 ya jumla ya uagizaji wa mafuta na asilimia 2 ya matumizi ya mafuta nchini.

Hali hiyo inaonyesha kuwa nchi za Kiarabu na Asia ndizo zingeathirika zaidi na hatua kama hiyo.

Ndio maana, nchi nyingi za Asia hudumisha uhusiano mzuri, hata wa karibu, na Iran.

Ushawishi wa China

China ni mmojawapo ya watumiaji wakubwa wa mafuta yanayopitia mkondo wa bahari wa Hormuz. Sehemu kubwa ya mafuta haya inauzwa na Iran kwa bei chini ya viwango vya soko la dunia, jambo linalosaidia uchumi wa Tehran kukabiliana na vikwazo vya Marekani.

EIA inakadiria kuwa China itanunua takriban asilimia 90 ya mafuta yanayouzwa na Iran mwaka 2024. Firouzabadi alisema kuwa ikiwa mkondo wa bahari wa Hormuz utafungwa, "China itapata hasara kwanza, na kwa hivyo mazungumzo ni muhimu pia kwa China."

Beijing, mmojawapo wa wateja wakubwa wa mafuta ya Iran, haiwezi kukubali ongezeko la bei au usumbufu wa njia za usafirishaji. Inatarajiwa kutumia nguvu zake za kidiplomasia kuzuia kufungwa kwa mkondo huu wa bahari muhimu.

Anas Alhajji, mshirika wa kampuni ya ushauri wa nishati Outlook Advisors, alisema kuwa kufungwa kwa mkondo wa bahari wa Hormuz kuna uwezekano kuumiza zaidi washirika wa Iran kuliko maadui wake.

Anas Alhajji alisema, "Wao [Wairani] hawataki kufanya jambo lolote ambalo lingewadhuru wenyewe kwanza."

Je, kuna njia mbadala za kuepuka kufungwa?

Tishio la muda mrefu la kufungwa kwa mkondo wa bahari wa Hormuz limezua nchi za Ghuba zinazouza mafuta kuendeleza njia mbadala za usafirishaji.

Mwaka 2019, Saudi Arabia ilirejesha kwa muda bomba la gesi asilia lililokuwa na uwezo wa kusafirisha mafuta ghafi.

UAE imeunganisha mashamba yake ya mafuta ya ndani na Bandari ya Fujairah katika Ghuba ya Oman kupitia bomba lenye uwezo wa mabareli milioni 1 kwa siku.

Iran ilitumia mradi wa bomba la Goreh-Jask mnamo Julai 2021, linalokusudia kusafirisha mafuta ghafi hadi Ghuba ya Oman. Kwa sasa, bomba hili linaweza kusafirisha takriban mabareli 350,000 kwa siku, lakini bado halijafikia kiwango kilichokusudiwa.

Juni iliyopita, EIA ilibaini kuwa takriban mabareli milioni 2.6 kwa siku ya uwezo usiotumika wa mabomba ya UAE na Saudi Arabia inaweza kutumika kuepuka mkondo wa bahari wa Hormuz.

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid