Kwanini maigizo ya 'Echoes of War' yanaigonganisha Siasa na Sanaa Kenya?

Mchezo huo, ulioonyeshwa wakati wa onyesho la awali, unaonyesha baadhi ya matatizo makubwa ya Kenya
Maelezo ya picha, maigizo katika tamasha linaloendelea nchini Kenya
    • Author, Mariam Mjahid
    • Nafasi, BBC Swahili
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Katika siku chache hizi kumetokea kisa cha kipekee nchini Kenya kinachodhihirisha mgongano kati ya sanaa na siasa , Shule ya wasichana ya Butere, kwa mara ya pili ndani ya miaka 12 imejipata matatani kwa kuzalisha igizo ambalo linakosoa vikali utawala na uongozi wa juu wa Kenya.

Igizo hilo huonyesha kufeli ama kufanya vibaya kwa uongozi na mapambano yanayotakiwa ili kulikomboa taifa.

Mwaka huu katika Tamasha la kitaifa ya nyimbo na michezo ya kuigiza, Kaunti ya Nakuru, katika shule ya Lions Academy, zimehusisha maigizo yenye utata likiwemo lililoandikwa na aliyekuwa Seneta wa kaunti ya Kakamega Cleophas Malala.

Shule hiyo ilikuwa imepigwa marufuku kuonyesha igizo la lililopewa jina la ''Echoes of War'' kwa misingi kuwa igizo hilo linashutumu vikali serikali.

April 03, 2025 Mahakama ya Nanyuki, ilibatilisha barua ya kupigwa marufuku kwa igizo hilo kuonyeshwa, ambapo hakimu Wilfrida Okwany aliwaidhinisha kuendelea kushiriki na kutumbuiza umma.

Katika hali ya siutafahamu wanafunzi wa shule ya sekondari ama upili ya wasichana ya Butere nchini Kenya walisusia kutumbuiza wakidai hawakuruhusiwa kuwa na urembo na vifaa vinavyohitajika ili kunogesha maigizo yao yaliyokuwa yanasubiriwa kwa hamu na waiofika kwa tamasha hilo.

Wakionyesha kuchukizwa na mazingira magumu ya kutumbuiza waliimba wimbo wa taifa na kuondoka jukwaani.

Kulingana na wakili wa shule hiyo Ken Echesa aliyekuwa amehudhuria ameapa kurejea mahakamani kumshtaki Mkurugenzi wa wizara ya elimu ukanda wa magharibi bwana Abiero kwa kutofuata agizo la mahakama kikamilifu.

Kulingana na Eugene Wamalwa aliyekuwa waziri wa ulinzi na wakili wa mwandishi wa igizo hilo, amesema serikali inapaswa kuwajibishwa kwa kukiuka haki za watoto kwa kuwatuma maafisa wa polisi takriban hamsini kusimamia tamasha hizo hali ambayo sio ya kawaida.

Tafrani zilipozidi baada ya wanafunzi hao kuondoka jukwaani ghafla maafisa wa polisi walitupa vitoa machozi katika shule moja walimoweka makaazi wanafunzi wa Butere ili kuwatawanya.

Maudhui ya maigizo haya yakoje?

Jalada ya tamthilia inayoibua hisia mseto Kenya

Chanzo cha picha, facebook

Maelezo ya picha, Jalada ya maigizo ama tamthilia inayoibua hisia mseto Kenya
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Na wengi wanajiuliza maudhui ya maigizo ama wengine wanaita tamthilia hiyo ambayo yamevutia hisia ni yepi?

Tamthilia ya 'Echoes of War' inaangazia mapambano ya vijana kuhusu uhuru wa kiraia, utawala na haki ya kijamii.

Maudhui yake yanachora taswira ya taifa la Kenya linalopona kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe huku vijana wakitarajiwa kuwa nguvu kubwa katika ujenzi wa taifa.

Kinachotia tumbo joto wandani wa utawala wa sasa nchini Kenya ni kuhusu mtirirko wa maigizo hayo.

Tamthilia hiyo inajikita katika mazingira ya uongozi maeneo ya ghuba na kuendeleza namna vijana walivyokosa imani na wazee kuhusu maswala ya uongozi.

Ikionyesha jazanda jinsi wazee wanaleta uzoefu huku vijana wakichangia na ubunifu wao.

Katika tamthilia hii ambayo mazingira yake ni ya mataifa ya kiarabu ,ufalme huo unajumuisha wazee wengi ambao hawana imani na kizazi kipya.

Jambo ambalo linawakera vijana ambao wanahisi wazee hawataki kubadilika na maisha.

Kulingana na mwandishi wa maigizo ama tamthilia hiyo Cleophas Malala akizungumza na televisheni moja ya Kenya amesema

''Tamthilia hii inachora picha kamili changamoto wanazopitia wanarika wa Gen z".

Katika tamthilia hii mhusika mkuu ni sultan ambaye ni bwenyeye na anasifa za mtu mwenye mamlaka.

Naye mama hanifa ni mwanamke ambaye amejikita kwenye dini na linamsononesha zaidi ni hulka za bintiye.

Kwa ufalme huo, vijana walitumia mitandao ya kijamii kuwaleta pamoja kupinga uongozi wa kiimla ulioambatana na utekaji nyara wa vijana waliopinga mfalme Sultan.

Naye Hanifa ambaye ni mama kijacho anatarajiwa kuzaa uongozi bora, afya bora na taifa lisiloendekeza ufisadi.

Mfalme sultan anapuuza hayo yote na kupoteza ushawishi miongoni mwa anaotawala.

Hisia zinazoendelea kuibuliwa

Muktadha huu ukitafisiriwa na wachanganuzi kuwa ni picha ya yaliyotokea Mwezi Juni mwaka jana ambapo vijana wa Kenya walijikusanya kupitia mitandao ya kijamii na kuandamana wakitaka uwajibikaji wa viongozi.

Hali ambayo ilisababisha vijana 60 kuuawa katika hali tatanishi na utekaji nyara huku Rais William Ruto akisalimu amri na kufanya mageuzi katika baraza lake la mawaziri.

Kulingana na Waziri wa Elimu nchini Kenya Julius Ogamba serikali haikuzuia Shule ya Upili ya Wasichana ya Butere kucheza mchezo wao wa 'Echoes of War' katika Tamasha za Kitaifa za Drama.

Hata hivyo alishangazwa na kwanini mtu asiye na taaluma ya ualimu kuhusika na kuunza tamthilia kwa wanafunzi wa shule ya Umma.

Kauli ambayo pia iliibuliwan a waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen akitoa onyo kusiwe na muingilio wa kisiasa katika sekta ya elimu.

Kupitia ukurusa wa X chama cha ODM kimesuta vikali serikali kwa kuingilia ubunifu wa wanafunzi katika maigizo ya shuleni.

''Funzo kubwa kutoka kwayo ni kwamba hata sauti za watoto wa shule zina umuhimu, na kwa kweli hazina hatia, sauti zao zinahitajika katika kuendesha mjadala wa kitaifa. Hakika tunaifananisha na igizo maarufu la Afrika Kusini la Sarafina'' ODM ilisema.

Naye Mwenyekiti wa chama cha KANU, Gideon Moi, amekashifu serikali kwa kuwanyima wanafunzi hao fursa ya kutumia kipaji chao.

Wakati huo huo, Amnesty International Kenya imelaani vikali hatua za polisi kuvuruga kwa nguvu onesho la tamthilia na kutaka Tume ya IPOA kuchunguza kwa uwazi na haraka vitendo vya polisi waliohusika, na kuhakikisha uwajibikaji.

Vipi fasihi ilijumuishwa katika mtaala wa elimu Kenya?

Mnamo mwaka wa 2010, Wizara ya Elimu ilianzisha sera ya mageuzi iliyojulikana kama "Demokrasia katika Elimu," ikiwa na dhamira ya kuimarisha ushirikishwaji wa wanafunzi katika masuala ya usimamizi wa shule na kukuza mazingira ya mawasiliano ya wazi kati ya walimu, wanafunzi, na wadau wengine wa elimu.

Miongoni mwa vipengele muhimu vya sera hii ni:

  • Kuanzishwa kwa baraza la wanafunzi katika shule, kama jukwaa la majadiliano ya wazi kati ya uongozi wa shule na wanafunzi.
  • Uwekaji wa masanduku ya maoni ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kueleza mawazo yao kwa njia ya faragha na huru.
  • Marekebisho kupitia Sheria ya Elimu ya Msingi ya mwaka 2013, yaliyojumuisha wawakilishi wa wanafunzi na walimu katika Bodi za Usimamizi za shule, hatua iliyolenga kuimarisha ushirikiano wa pande zote.
  • Kufutwa rasmi kwa adhabu ya viboko, kama hatua ya kulinda haki za wanafunzi na kukuza mbinu mbadala za nidhamu.
  • Kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi moja kwa moja na wanafunzi wenyewe, hatua iliyolenga kukuza maadili ya uongozi na uwajibikaji miongoni mwa vijana.

Kwa miaka mingi nchini Kenya, wanafunzi pia wamekuwa wakifundishwa kazi za fasihi zinazochambua kwa kina hali ya jamii.

Miongoni mwa kazi hizo ni Betrayal in the City, Masaibu ya Ndugu Jero, Damu Nyeusi, Mashetani, Kifo Kisimani, na Mstahiki Meya.

Kazi hizi za kifasihi zimekuwa zikiibua mijadala kuhusu maovu ya kijamii, ukandamizaji wa haki, na changamoto za kiuongozi katika jamii.

gg

Chanzo cha picha, facebook

''Sanaa ni kioo cha Jamii''

Sanaa, hususan michezo ya kuigiza, imekuwa daima kioo cha jamii.

Hata hivyo, wanaharakati wameibua hisia katika tukio la hivi majuzi lililohusisha kuingiliwa kwa mchezo wa kuigiza wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Butere na kuzua maswali kuhusu nafasi ya sanaa katika kueleza ukweli wa kijamii.

Na sio tamthilia hii pekee ambayo imezua mihemko nchini Kenya mwaka 2013, ''Shackles of Doom," iliyoangazia unyanyasaji wa True people of Kana na jamii tajiri ambayo ilivamia rasilimali yao ya mafuta iliibua gumzo.

Wakati wa utawala wa Rais wa pili wa Kenya Daniel Moi tamthilia ya ''I WILL MARRY WHEN I WANT'' ulipigwa marufuku wiki chache baada ya kuchapishwa na mwandishi Ngugi wa Thiong'o.

Mchezo huo ambao ulikuwa na fursa ya kuelimisha na kuamsha fikra, ulizimwa katika mazingira yenye utata, na hivyo kuvuta hisia za umma na kuibua mjadala mpana kuhusu uhuru wa kisanii nchini Kenya.