Tamasha maarufu la Filamu la Cannes linavyokumbatiwa Bollywood

Cannes Festival

Chanzo cha picha, Pascal Le Segretain

    • Author, Na Suparna Sharma
    • Nafasi, BBC

Bollywood ilikutana kufanya maamuzi kuhusu filamu bora dunia siku ya Jumanne huku mwigizaji nyota Deepika Padukone akijiunga na kundi la majaji tisa katika Tamasha la 75 la Filamu la Kimataifa la Cannes nchini Ufaransa kuzungumza na waandishi wa habari.

Baraza la majaji, linaloongozwa na mwigizaji Mfaransa Vincent Lindon, lilitatazama filamu 21 na kuchagua moja ambayo itapata tuzo la Palme d'Or taji la kifahari zaidi duniani la filamu bora zaidi.

Bi Padukone, 36, mwigizaji anayelipwa zaidi Bollywood ambaye anajulikana kwa uhusika wake katika Padmaavat, Piku na katika filamu ya hivi maajuzi zaidi ya Gehraiyaan, alisema anatazamia kutazama filamu, ''kufurahia mchakato huu wa ubunifu na kukumbatia uzoefu''.

Bi Padukone ndiye atakayepigwa picha nyingi na kuzungumzwa zaidi kuhusu nyota wa Kihindi katika Tamasha la Filamu la Cannes mwaka huu, lakini si yeye pekee anayeongeza ladha kwenye filamu za Kihindi katika sherehe inayozingatiwa zaidi na kuchukuliwa kuwa kuu ya filamu duniani.

Cannes Festival

Chanzo cha picha, Pascal Le Segretain

Maelezo ya picha, Tamasha la 75 la Filamu la Cannes

Karibu na mahali ambapo Bi. Padukone atakuwa akitazama na kutoanuamuzi wake kuhusu filamu hizo, kikosi cha filamu za kihindi, kikiongozwa na waziri wa habari na utangazaji wa India Anurag Thakur, kimefika kwa ajili ya kufanya biashara katika ukumbi wa Marché du Film, soko kubwa la filamu duniani linaloendeshwa kwa wakati mmoja na Tamasha la Filamu la Cannes.

Kila Mei, soko hilo la hadhi ya juu lakini linaloendeka kwa urahisi la kifahari maeneo ya pwani ya Cannes kwenye Mto wa Riviera wa Ufaransa huchukua muda wake kusonga mbele kwa mwendo wake wa pole, hata kuonekana kusitasita tamasha la filamu linapokaribia.

Wasiwasi wa kila mwaka unaeleweka kwani takriban watu 120,000 wanafika katika mji wa watu 74,000 kuhudhuria Tamasha la Filamu la Cannes, ambalo husherehekea sanaa ya utengenezaji wa filamu, na 'Marché du Film' ambapo mikataba yenye thamani ya mamilioni inafanywa kwa uuzaji, usambazaji wa filamu.

Cannes Festival

Chanzo cha picha, Joe Maher

Lakini mwaka huu, jiji linapoondoka na sheria za kufungiwa kuwasababu ya Covid-19 na kiwewe, mhemko umekuwa wa tofauti.

Sasa hakuna tena kuvaa barakoa na kuna hamu kubwa ya kurejea kwa hali ya kawaida.

Na ili kuanzisha upya mapenzi ya filamu, Cannes iko katika kukumbatiana kabisa na filamu za India ambazo zinapendwa na wengi.

Mwaka huu India, mtayarishaji mkubwa zaidi wa filamu duniani, imefanywa kuwa ''Nchi ya Heshima'' katika Marché du Film.

Kama nchi ya kwanza kupata hisani hii, India itapewa jukwaa, kihalisia kabisa, kuonyesha talanta yake.

Wakurugenzi, watayarishaji na wasambazaji wa Kihindi watapata fursa za kupeleka filamu zao kwenye masoko mapya na kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya ushirikiano.

''India ina simulizi nyingi za kusimuliwa na nchi hiyo ina uwezo mkubwa wa kuwa kitovu cha maudhui ulimwenguni,'' Bw Thakur alitweet, akimnukuu Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Ili kuimarisha hali yake kifilamu, Bw Thakur ameleta filamu kadhaa mpya, waigizaji na mtunzi wa muziki aliyeshinda tuzo ya Oscar AR Rahman ambaye naye ameleta filamu yake, Le Musk.

Filamu hiyo inatarajiwa kuwa na onyesho lake la kwanza la dunia katika soko la Filamu za Cannes.

Filamu nyingine ya Kihindi inayosubiriwa kwa hamu na ambayo itaonyeshwa kwa mara ya kwanza duniani kwenye soko la filamu ni 'Rocketry: The Nambi Effect.'

Rocketry ni wasifu kuhusu Nambi Narayanan, mhandisi wa anga wa India ambaye alishtakiwa kwa uwongo kuwa kijasusi, kukamatwa, kukashifiwa na baadaye kuachiliwa huru.

Filamu hii inasura ya mwigizaji maarufu Shah Rukh Khan.

Cannes Festival

Chanzo cha picha, Getty Images

Tamasha la Cannes, litakaloanza tarehe 17 hadi 28 Mei, lina safu ya kusisimua ya maonyesho ya kwanza ya ulimwengu ya filamu kubwa zaidi za Hollywood (Tom Cruise Top Gun: Maverick, Baz Luhrmann Elvis), na baadhi ya waigizaji mahiri kama (Javier Bardem na Mads Mikkelsen, miongoni mwa wengine), sinema bora zaidi ya jumba la sanaa na vile vile filamu mbili za Kihindi zilizofasiriwa.

Filamu ya Satyajit Ray ya mwaka 1970, Pratidwandi (The Adversary), na G. Aravindan Thamp (The Circus Tent) itaonyeshwa kwenye tamasha hilo na sasa hivi ni vigumu kupata tikiti kwa kuwa zilishaisha.

Lakini uwepo wa kupendeza na wa kushangaza zaidi wa Wahindi huko Cannes mwaka huu ni makala kuhusu jitihada za ndugu wawili wa Delhi kuokoa ndege - hasa, tai weusi - ambao wanauawa na uchafuzi wa mazingira unaoongezeka jijini.

Cannes Festival

Chanzo cha picha, Pascal Le Segretain

'All That Breaths' ni miongoni mwa filamu 12 ambazo zitacheza katika sehemu isiyo ya mashindano, pamoja na filamu ya kwanza wa uongozaji wa mtu binafsi wa Ethan Coen, Jerry Lee Lewis: 'Trouble in Mind.'

Filamu nyingine ya Kihindi katika orodha rasmi ya Cannes mwaka huu ni Nauha.

Iliyoundwa na Pratham Khurana, mwanafunzi wa shule ya filamu mwenye umri wa miaka 23, ya dakika 26, Nauha (ambayo inamaanisha ''maombolezo'' kwa Kihindi), inahusu mvulana mdogo ambaye anamtunza mzee wa miaka 75 anayekufa.

Cannes Festival

Chanzo cha picha, Dominique Charriau

Imechaguliwa kati ya zaidi ya maigizo 1,500 yaliyowasilishwa na shule za filamu kutoka kote ulimwenguni na ni mojawapo ya filamu 16 zinazoshindaniwa kupata tu

Wakati huohuo, Bi Padukone, alionekana mtu mdogo aliyevalia nguo nyingi lakini mwenye kustaajabisha katika kitambaa cha kichwani na mkufu wa dhahabu ambao ulionekana kana kwamba unadondosha mawe ya thamani.

Lakini alikuwa tayari kuchukua jukumu la kuwa jaji alisema.

Akiongeza kuwa wakati wa kutazama filamu atajaribu ''kusahau kwamba kwa kweli tuna mzigo na jukumu hili'' la kuchagua mshindi, na badala yake kukumbuka ''watazamaji ... mtoto huyo mdogo ambaye amekua akitazama sinema na kuhamasishwa''

''Nadhani filamu ni chombo chenye nguvu katika mawasiliano. Ina uwezo wa kuathiri na kubadilisha maisha ya watu,'' Bi Padukone alisema.