Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Chelsea inaendelea kumfuatilia Tonali

Muda wa kusoma: Dakika 4

Sandro Tonali yuko anafuatiliwa na Chelsea, Napoli wanaendelea kumwinda Kobbie Mainoo, huku Real Madrid ikiendelea kuvutiwa na Rodri.

Chelsea inamfuatilia kiungo wa kati wa Newcastle United, Sandro Tonali, kwa lengo la kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 25 msimu huu. (Football Insider)

Napoli bado ina nia ya kumsajili kiungo wa Manchester United Kobbie Mainoo, 20, lakini itaweza kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ikiwa winga wa Uholanzi Noa Lang, 26, ataondoka katika klabu hiyo ya Italia. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)

Real Madrid inaendelea kumfuatilia kiungo wa kati wa Uhispania Rodri lakini haitamchukua mchezaji huyo wa miaka 29 hadi msimu wa joto atakapoingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake Manchester City. (Marca - in Spanish)

Pia unaweza kusoma:

Chelsea wanapanga kutoa dau la euro milioni 150 (£130.6m) kwa kiungo wa kati wa England na Aston Villa Morgan Rogers, 23. (Fichajes - in Spanish)

Aston Villa wanamtaka winga wa Misri Omar Marmoush, 26, ambaye amekuwa akipambana kupata muda wa kucheza mara kwa mara Manchester City. (Teamtalk)

Beki wa Uingereza Jahmai Simpson-Pusey, 20, anatarajiwa kusafiri hadi Cologne kukamilisha uhamisho wa mkopo kutoka Manchester City. (Sun)

Dau la euro milioni 20 (£17.4m) la Fulham kwa kiungo wa kati wa Ufaransa Arthur Atta, 22 limekataliwa na klabu ya Udinese ya Italia. (Fabrizio Romano)

Barcelona wanaongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto, huku AC Milan na Bayern Munich pia wakimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia mwenye umri wa miaka 25. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)

Beki wa Manchester United, Muingereza Harry Amass, 18, anaweza kukatiza mkataba wake wa mkopo huko Sheffield Wednesday ili kujiunga na Stoke kipindi kilichosalia cha kwa msimu. (Sun)

Manchester City wako kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji wa Troyes, Mathys Detourbet, mwenye umri wa miaka 18, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Roma na Monaco. (L'Equipe - in French)

Liverpool wamejiunga na Manchester United na Tottenham katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Brighton mwenye umri wa miaka 22, Carlos Baleba. (CaughtOffside)

Hata hivyo, Liverpool wametupilia mbali nia yao ya kumsajili mlinzi wa Newcastle United Sven Botman kutokana na wasiwasi kuhusu matatizo ya jeraha ya Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 25 yanayoendelea. (Chronicle)

Tottenham wanamfuatilia winga wa Club Brugge na Ugiriki Christos Tzolis mwenye umri wa miaka 23. (Teamtalk)

Eintracht Frankfurt italipa euro milioni 1.5 (£1.3m) kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23, Arnaud Kalimuendo, kwa mkopo kutoka Nottingham Forest na mpango huo utajumuisha chaguo la kumnunua kwa takriban euro milioni 27 (£23.5m). (Florian Plettenberg)

Kiungo wa kati wa Lazio Matteo Guendouzi, 26, anahitajika na vilabu viwili vya Ligi Kuu lakini Fenerbache wamefanya hatua ya kwanza kwa kutoa euro milioni 27 (£23.5m) kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (L'Equipe - in French)

Roma wanataka kurekebisha safu yao ya ushambuliaji katika vipindi viwili vijavyo na winga wa Liverpool, Federico Chiesa, mwenye umri wa miaka 28, ni miongoni mwa walengwa wao. (Corriere dello Sport - in Italian)

Vinara wa michuano Coventry City wanavutiwa na winga wa Crystal Palace Romain Esse, 20, na kuwasili kwa Brennan Johnson kwa pauni milioni 35 kutoka Tottenham kunaweza kufanya kuondoka kwa Muingereza huyo kuwe rahisi zaidi. (Mail)