Charles Darwin: Namna nadharia yake ilivyobadili mjadala kuhusu Mungu na Dini

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Dini nyingi ulimwenguni zinaamini Mungu alimuumba mwanadamu wa kwanza, aitwaye Adamu. Watu pia wanaamini wameumbwa na Mungu huyo huyo.
Kabla ya mwaka 1859 nadharia ya kwamba Mungu aliumba mwanadamu haikutikiswa. Ghafla mtu mwenye ndevu aliwasilisha nadharia ya mageuzi (theory of evolution).
Charles Darwin aliwasilisha utafiti wake, 'The Origin of Species by Natural Selection.' Anaeleza kuwa spishi mbalimbali zimetokea katika asili moja na zimebadilika kulingana na mazingira waliyoishi na kufika katika hali yao ya sasa.
Utafiti huu ulitilia shaka itikadi zote za hapo awali kuhusu Mungu, uumbaji, asili ya mwanadamu na mabadiliko katika maisha. Licha ya upinzani wa hapa na pale, ulimwengu wa sayansi haukuweza kuachana na nadharia ya Darwin.
Ilichukua miaka 20 kwa Charles Darwin kuleta matokeo ya utafiti wake kwa ulimwengu. Lakini hakukimbilia kuuchapisha.
Charles Darwin ni nani?

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Charles Robert Darwin alizaliwa Shrewsbury, Uingereza tarehe 12 Februari 1809 katika familia tajiri. Babu yake alikuwa mwanasayansi na baba yake alikuwa daktari.
Darwin awali alisomea afya katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, kwa amri ya baba yake, lakini badala yake alipendezwa na sayansi. Ndipo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Cambridge.
Mahali hapo palimpa Darwin muda zaidi wa kusoma sayansi, na alihitimu huko 1831. Alijifunza mambo mengi kutoka kwa maprofesa wa chuo hicho.
Safari ya Darwin Kuzunguka Dunia

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Mwaka 1831 Darwin alipata fursa ya kusafiri kwa pendekezo la profesa wa Chuo Kikuu cha Cambridge, kwenye meli ya kijeshi ya HMS Beagle, ambayo ilikuwa kwenye ziara ya Amerika Kusini.
Akitumia hii kama fursa ya utafiti wake, Darwin alitumia miaka mitano iliyofuata kusafiri zaidi ya kilomita 3,000 katika mabara 4 na kukusanya maelfu ya vielelezo vya spishi.
Katika safari hizi alipata ufahamu wa asili na mageuzi ya maisha. Alijifunza kwamba viumbe wa aina moja wanaoishi katika sehemu mbalimbali za dunia wana miundo tofauti ya mwili.
Baada ya kurudi kutoka msafara wa mwaka 1838, Darwin alianza kuandika kitabu chake On the Origin of Species. Hata hivyo, hakukichapisha.
Lakini wakati huo alikuwa amechapisha kitabu kuhusu safari yake kinachoitwa 'The Voyage of Beagle.'
Darwin alimuoa binamu yake Emma. Walizaa watoto 10. Lakini, mtoto wao mmoja wa kiume na mabinti 2 waliugua na kufariki.

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Emma aliamini kwamba hilo ni kwa sababu Darwin hakuwaona watoto wake na hakufuata imani za kidini. Kutokana na hilo, vita vya kihisia viliendelea kati ya wawili hao.
Baada ya miaka 20 tangu kuandika, the Origin of Species. Alfred Russel Wallace naye alikuwa amefanya utafiti wa nadharia hiyo hiyo, na wote wawili kwa wakati mmoja waliwasilisha nadharia zao kwa jarida la Linnean Society.
Darwin hakuchapisha kitabu chake mwanzo kwa sababu za kifamilia kama ilivyotajwa hapo juu. Lakini baadaye kitabu kilichapishwa. Na Darwin aliweka jibu la ukosoaji wa nadhari yake katika kila toleo.
Darwin aliweka wazi maelezo ya kisayansi kwamba spishi inaweza kuishi tu ikiwa itabadilika na kuendana na mazingira asilia inayoishi.
Upinzani dhidi yake

Chanzo cha picha, VENKATESAN
Ni kawaida mafundisho mapya yanapokuzwa dhidi ya mafundisho ya zamani ambayo tayari yanafuatwa, kutakuwa na upinzani. Licha ya upinzani dhidi ya nadharia ya Darwin bado nadharia hiyo imekuwa.
''Alikuwa akiipeleka familia yake kanisani na yeye hukaa nje. Hakuchukua msimamo wa kumkana Mungu, bali amehoji tu mafundisho ya dini. Kutokana na hili, hakukabiliwa na upinzani mkubwa,'' anasema mkuu wa zamani wa kitengo cha mionzi na ulinzi wa mazingira, katika kituo cha utafiti wa nyuklia cha Indira Gandhi, India, Dkt. R. Venkatesan.
Nadharia ya Darwin ilipokosolewa hadharani, mwanabiolojia Thomas Huxley ndiye aliyeitetea. Alizungumza na kuunga mkono nadharia za Darwin katika mikutano mingi mikubwa.
Ingawa Darwin alichapisha nadharia yake ya mageuzi miaka 170 iliyopita, R. Venkatesan anasema, nadharia hiyo ni muhimu wakati ambapo watu wengi bado wanafuata imani za zamani kuhusu asili ya binadamu.''















