Vitisho wanavyopokea Wasomali wasioamini kwamba Mungu yuko

Two people looking at computers

Raia wa Kisomali wasioamini kwamba kuna kuna Mungu wanaoishi ughaibuni wana kundi lao katika mtandao wa Facebook linalopinga imani za raia wa Kisomali ambao ni Waislamu lakini mara huwa wanapokea vitisho vya vifo, amesema wanahabari Layla Mahmood.

"Mimi nitakuua. Nitakutafuta. Na nitakata kichwa chako," ni moja ya vitisho alivyopokea Ayaanle ambaye anaishi Canada. raia wa Kisomali asiyeamini kuwa Mungu.

"[Lakini] hali kama hiyo ni kawaida," mwasisi wa ukurusa wa Somali Freedom Page anasema hivyo anapozungumzia vitisho anavyopokea kupitia simu yake.

Kundi hilo maarufu kwenye mtandao wa Facebook, ambalo lina watu zaidi ya 80,000 linaongozwa na waliokuwa Waislamu ambao kwa sasa wamebadilika na kuwa wasioamini Mungu kama wanavyojiita wenyewe.

Awali, kundi hill liliundwa ili kutengeneza mazingira ya kujadili masuala ya kidini lakini sasa linaendeleza uhuru wa kujieleza kwa raia wa Kiislamu ambao wanahisi kutengwa na jamii inayozingatia utamaduni wa Kisomali.

Ayaanle hakutaka kutoa majina yake kamili wakati anaelezea shughuli za kundi lao.

Man looking at a computer screen

Niliondolewa kwenye kundi hilo.

Karibia mwaka 2016, alikutana na kundi hilo la Wasomali katika mtandao wa Facebook ambalo lilionekana kutengeneza mazingira ya kuzungumzia mijadala kwa uwazi.

"Nikaanza kuchangia mijadala kuhusu dini na kila mmoja akaanza kuchangia mjadala huo kwa nguvu yake yote. Wakabadilika na kuwa kama makombora jinsi wanavyorusha maneno makali. Wakanifanya nihisi kama mtu ambaye nimetekeleza mauaji."

Akaondolewa taratibu kwenye kundi hilo jambo la kawaida kwa wale wenye kuwa na maoni tofauti katika mijadala ya haina hii kwa majukwaa ya mtandao ya kijamii ya Wasomali.

'Mtandao wa kuwa huru'

Ayaanle akahisi kwamba njia pekee ya kutatua changamoto hiyo ilikuwa ni kufungua ukurasa mpya wa majadiliano kwa uhuru litakalokuwa na sheria mpya.

"Nilitaka kuwa na mtandao ambao watu wangejadili kwa uhuru kila wanachopenda."

Kilichompa Ayaanle msukumo ni imani ya kwamba majadiliano ya Wasomali wa sasa kuhusu dini yamekuwa na masharti mengi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu.

"Uislamu haubadiliki. Huwezi kuikosoa dini hiyo au kusema lolote kuhusu Uislamu.

"Kwa sasa hivi vijana wanabadilika, wanaweza kuvumilia kidogo katika mijadala na kukosolewa.

"[Lakini] wengi wa walio kulia nchini Somalia na kwenda nchi za Magharini baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe wazo la ikiwa atakubali mtu kukosoa Uislamu kwao adhabu ya mtu huyo ni kuuawa. Wanafikiria kwamba hatua hiyo ni haki yao. "

Na hiyo ndio sababu amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa.

"Hayo ni baadhi ya yale ambayo ninataka kuyaweka kwenye ukurasa wa mtandaoni - kuonesha kwamba Uislamu sio kuwa ni dini ambayo haikosolewi. Pia nayo inaweza kukosolewa. Inaweza kujadiliwa na inaweza kuzungumziwa kwa uwazi."

PICHA

Man walking out of prison

Nchini Somalia, na katika jimbo la Somaliland, kukufuru au kukashifu dini ni kosa ambalo mtu anastahili kufungwa na mtandao alioufungua Ayaanle umekabiliana na changamoto hiyo.

Kundi hilo lilifanya kampeni na kuchangisha pesa za msomi Mahmoud Jama Ahmed-Hamdi. Alikuwa mhariri wa chuo kikuu ambaye alikamatwa kwa kuandika kwenye mtandao wa Facebook ujumbe ambao unahoji uhalali wa kumuomba Mungu kama njia ya kukabiliana na kiangazi mwaka 2019.

Alihudumia kifungo cha miezi 10 kabla ya kutolewa kwa msamaha wa rais lakini bado yuko katika hatari ya kushambuliwa na makundi yenye msimamo mkali. Imam mmoja mashuhuri alitoa wito wa kuuawa kwake.

Tukio hilo linaonesha nguvu ya madaraka nchini Somalia na Somaliland, huku kukiwa na sintofahamu kati ya msimamo wa viongozi wa kidini na serikali.

Hofu ya kutambulishwa kwa watu

Wasomali sio kwamba wamekuwa wakitumia tu kundi hili kama jukwa la kujadiliana lakini pia wakati mwengine kama njia ya watu kuendeleza maisha ya kila siku.

Baadhi ya makundi yaliyo katika hatari nchini Somalia ambao wameweka ujumbe wao katika mtandao uliofunguliwa na Ayaanle, ni Wakristo, wale wasioamini kwamba kuna Mungu na wapenzi wa jinsia moja.

Hao ndio watu ambao huwa na hofu katika maisha yao ya kufahamika na wengine na kushambuliwa au kufungwa jela.

Njia moja ya mtandao huo kutoa msaada wake ni kuchangisha pesa ambazo zinatumika kununua tiketi za ndege na kusaidia katika mahitaji ya kila siku.

Hali ilikuwa hivyo kwa mwanamke raia wa Kisomali nchini Kenya ambaye aliacha utambulisho wake baada ya kutoa maoni kwenye mtandao wa Ayaanle.

Mara moja alitafutwa na video inayomuonesha akiburutwa kutoka kwenye taxi nchini Kenya ikasambaa sana katika mitandapo ya kijamii ya Wasomali.

Washambuliaji walitishia kusema ukweli yeye ni nani kwasababu alimkosoa Mtume Mtume Muhammad kwenye ukurasa huo.

Ukurasa wa Ayaanle ulifanya maandalizi ya kumuhamisha katika nchi tofauti na kwa sasa hivi yuko salama katika jamii ya Kikiristo.

Uchunguzi wa kina

Lakini sio tu kwa wasio Waisilamu, waliokuwa Waislamu au wapenzi wa jinsia moja ambao waliwasiliana na kundi hilo.

PICHA

A woman being man-handled

Raia mmoja wa Kisomali aliyekuwa anaishi Sudan aliwasiliana na mtandao wa Ayaanle baada ya kushambuliwa mwili wake mtaani na kundi la wanaume ambao anaamini ni wale Wahhabism - Waislamu ambao mara nyingi huusishwa na kuwa na msimamo mkali hasa katika utafsiri wa Korana na mafundisho ya Mtume Muhammad.

Alitambuliwa baada ya kukosoa Hadithi katika mtandao wa Facebook wa Ayaanle yenye kuhusishwa na Mtume Muhammad. Mtandao wa Ayaanle ulifanya maandalizi na kumhamisha nchini Sudan hadi eneo salama.

Maombi yanayopokelewa na msimamizi wa kundi hilo kuna maamnisha kwamba yanahitaji kutathminiwa na kupitiwa kwa makini.

PICHA

A woman smiling

"Tunatafiti na kuchunguza," Kahaa Dhinn, mwanamke mwenye kutetea haki za wanawake nchini Norway ambaye sasa hivi amekuwa kama kiongozi wa kundi hilo katika ukurasa huo anasema.

"Tunawauliza kabila na familia zao. Kisha tunaangalia ukurasa wao wa Facebook na kuzungumza na watu wa kundi hilo kuangalia kama kuna yeyote anayewajua. Ikiwa hatuweza kubaini kabila lake, tunajua kwamba wanadanganya."

Kahaa anashirikiana na mtandao wa Ayaanle lakini ana ukurasa wake wa Facebook na akaunti ya Youtube anaotumia kama jukwaa la kujadili masuala yanayoathiri jamii ya Kisomali.

'Najua unako ishi'

Angalizo lake kubwa ni kuwezesha wanawake wa Kisomali lakini kwa Ayaanle pia naye ni mzungumzaji mzuri tu ambaye haamini kama kuna Mungu na hilo limemfanya kuwa moja ya malengo yake.

"Walitishia kuniua kwa visu na kusema Waislamu watakuua na utakufa mikononi mwao'.

Lakini tishio hilo linaonekana kutozima ndoto yake: "Siwaogopi. Wanataka kuninyamizisha kwa kunitia hofu."

Raia wa Norway aliyekamatwa

Ujasiri wa kutoogopa kwake kunatokana na ufahamu wa kuwa anaishi katika nchi ambayo vitisho vina athari zake.

Nchini Somalia, mauaji na mashambulio ni mara chache sana huwa yanachunguza lakini nchini Norway polisi huusika.

"Wanaume wawili walionitishia walikuwa wanatumia ukurasa wa wasifu wao na maafisa wa polisi walifanikiwa kuwakamata," anasema.

Ayaanle anaunga mkono maoni hayo lakini anajua kwamba kuna wale ambao hawana bahati hiyo.

"Wasomali wengi ambao wako kwenye ukurasa ule huwa hawaoneshi sura zao - wale ambao wanasema hawaamini kuwa Mungu yupo - kwasababu wanahofia maisha yao," anasema.

'Nahisi kufarijika'

Ukweli wa kwamba Ayaanle na Kahaa wamejitenga na Uislamu haimaanishi kwamba wamejitenga na kuwa Wasomali licha ya kwamba wawili hao maono yao yanaendana.

"Nahisi kuwa mimi ni Msomali, kwasababu huko ndio kwenye mizizi yangu," anasema Kahaa.

Lakini Ayaanle anasisitiza kwamba lengo la kundi hilo sio kubadilisha Wasomali Waislamu na kuwa wasioamini kama Mungu yupo, au kuwaingiza katika dini yoyote nyengine ile bali ni kujenga mazingira ya kuimarisha uhuru wa kuzungumza. Kitu ambacho anaamini kwamba kwa sasa hivi kinapatikana kwa Wasomali kuliko nyakati nyengine yoyote ile.

"Kwa hiyo hatua inapigwa japo kidogo kidogo. Lakini tunaendelea kupata uungwaji mkono. Tunaamini kwamba watu wanastahili kuamini kile wanachotaka wao maishani.