Kwanini Putin amemuondoa mshirika wake Sergei Shoigu kama waziri wa ulinzi Urusi?

Chanzo cha picha, EPA
Mawazo machache juu ya mabadiliko nchini Urusi.
Wazo namba moja: Yeyote anayeketi karibu na meza ya baraza la mawaziri nchini Urusi, kuna mtu mmoja tu anayechukua maamuzi muhimu nchini - na huyo ni Rais Putin.
Katika Urusi ya kisasa mfumo mzima wa kisiasa umejengwa karibu naye. Inastahili kuzingatia wakati wa kujadili nani yuko ndani na nani yuko nje ya serikali. Sera ya kati haiwezekani kubadilika.
Je, hiyo inamaana kwamba mabadiliko ya serikali ya Urusi hayapendezi, au sio muhimu?
Hapana, haifanyi hivyo. Kuondoka kwa Sergei Shoigu kutoka kwa wizara ya ulinzi kunavutia katika ngazi nyingi.
Baada ya yote - na hii inatuleta kwenye wazo namba mbili - mabadiliko ni jambo adimu katika Urusi. Angalau, kwa kadiri wahusika mashuhuri wa kisiasa wanavyohusika.
Mchukue Sergei Lavrov, waziri mkongwe wa mambo ya nje wa Urusi. Amekuwa na kazi hiyo kwa miaka 20. Sergei Shoigu alikuwa waziri wa ulinzi kwa miaka 12 (wakati huu wote, Uingereza imepitia makatibu sita wa ulinzi).
Bw Shoigu anachukuliwa kuwa mshirika wa karibu wa Rais Putin.
Wazo la tatu: Kuwa karibu na Putin, kwenda kwenye safari za uvuvi na uwindaji na rais (ndio, Sergei Shoigu alifanya hivyo - hata, kwa umaarufu, walienda kuchuma uyoga pamoja), hakuna dhamana yoyote utailinda kazi yako.

Chanzo cha picha, AFP
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Sergei Shoigu amebadilishwa kama waziri wa ulinzi na mwanauchumi wa teknolojia Andrei Belousov. Bw Shoigu hajafutwa kazi lazimishwa Yeye ataongoza Baraza la Usalama la Urusi badala ya Nikolai Patrushev.
Lakini haionekani kama amepandishwa hadhi.
Kwa hivyo kwa nini mfuasi wa Putin amehamishwa kutoka kwa wizara ya ulinzi?
Mbona mchumi amechukua nafasi yake? Na hii inatuambia nini kuhusu Vladimir Putin?
Usishangae, uvumi ulienea kwamba Sergei Shoigu anaweza kutengwa. Mmoja wa manaibu wake, Timur Ivanov, alikamatwa hivi majuzi kwa tuhuma za ufisadi.
Zaidi ya hayo, kumbadilisha Bw Shoigu na kuchukua mwanauchumi ni jambo la maana, unapozingatia kiasi kikubwa cha fedha ambacho mamlaka imekuwa ikimwaga katika vita vya Urusi nchini Ukraine.
Matumizi ya ulinzi nchini Urusi yamefikia hadi wastani wa 7% ya Pato la Taifa. Ni kana kwamba uchumi wa Urusi unawekwa kwenye msingi wa vita.
Kuna mantiki ya kuwa na waziri wa ulinzi anayeelewa fedha, mipango ya uchumi na hitaji la ufanisi - mtu ambaye pia hana uhusiano na tuhuma za ufisadi zinazochunguzwa kwa sasa.

Chanzo cha picha, Reuters
Lakini cha kufurahisha ni kwamba Vladimir Putin alichagua wakati huu kufanya mabadiliko. Rais aliamua kusalia na Shoigu mnamo 2022 wakati Urusi ilikuwa ikikabiliwa na vikwazo vya kijeshi nchini Ukraine.
Alisalia naye tena mwaka wa 2023 wakati waziri huyo alipozozana hadharani na aliyekuwa mkuu wa mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin, ambaye alikuwa amemshtumu Shoigu kwa ufisadi na kutaka afutwe kazi.
Sasa, wakati Urusi inadai kuwa kifua mbele katika mstari wa vita , kiongozi wa Kremlin amembadilisha waziri wake wa ulinzi. Inaonyesha tena kwamba Vladimir Putin hapendi kuchukua hatua chini ya shinikizo. Anachukua maamuzi kwa wakati anaochagua.
Lakini kuna kipengele kimoja zaidi cha mabadiliko ya serikali ya Urusi. Daima hukuacha ukiuliza maswali. Kuna mengi baada ya hii.
Hivyo basi tunauliza
Nini kinafuata kwa Sergei Shoigu? Je, anaweza kutengeneza msingi mpya wa mamlaka katika Baraza la Usalama, au ni jambo lisiloepukika kwamba katika wadhifa wake mpya mamlaka yake yatapunguzwa?
Ni nini kinachofuata kwa mtu anayechukua nafasi yake katika Baraza la Usalama, Nikolai Patrushev?
Kwa muda mrefu akizingatiwa kuwa mmoja wa watu wenye nguvu zaidi nchini Urusi, je, Bw Patrushev atahifadhi ushawishi wake? Na kwa mwonekano gani?
Je, uteuzi wa waziri mpya wa ulinzi unamaanisha kwamba, wakati fulani hivi karibuni, kutakuwa na mkuu mpya wa majeshi badala ya Valery Gerasimov?
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












