Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini kilemba hiki ni muhimu kwa Wapalestina?
Shambulio la Hamas dhidi ya Israel Oktoba 7 na jibu la Israel lilisababisha vifo na uharibifu, na maandamano kote ulimwenguni.
Katika maandamano hayo, washiriki wawe niWaarabu au la, walionekana wakiwa wamevalia kilemba cha kitamaduni kinachojulikana kama Kufiya.
Baadhi ya watu waliifunga shingoni mwao; huku wengine wakiinua juu ya vichwa vyao.
Umuhimu wa kilemba hiki hauwezi kupuuzwa.
Wapalestina wengi wanaichukulia kuwa ni chombo cha kitamaduni na kisiasa, ishara ya ujasiri na upinzani.
Ni chombo cha kitamaduni na kisiasa ambacho kimekuwepo kwa miaka 100 iliyopita.
Inajulikana kama "bendera isiyo rasmi" ya Palestina.
Kilemba hiki kimetoka wapi? Imekuwa ishara lini na ni muhimu kiasi gani leo?
Chimbuko lake
Japo haijulikani ilitoka wapi, baadhi ya wanahistoria wanasema huenda inaweza kuhusishwa na karne ya 7, haswa mji wa Iraqi wa Kufa (kama inavyoonyeshwa katika jina lake Kufiya).
Wengine wanadai kwamba asili yake ni ya zamani, hata kabla ya Uislamu.
Ukweli ni kwamba kwa miaka mingi matumizi yake yameenea. Lakini sio lazima itumike tu kiutamaduni na kisiasa.
Mwanzoni mwa karne ya 20, kilemba hiki mara nyingi kilivaliwa na Waarabu wa vijijini ili kujikinga na jua, upepo, mchanga wa jangwani au baridi.
Mijini, hata hivyo, kuna uwezekano wa kuona Wapalestina wamevaa kilemba hiki.
Wanapendelea kuvaa nguo za kisasa kama vile Fez, pia inajulikana kama Tarbush, ambalo ni vazi la zambarau lililojulikana na kiongozi wa Ottoman Mahmud II.
Lakini utafiti unasema kwamba katika miaka ya 1930, kilemba hiki kilikuwa na maana maalum kwa jamii ya Wapalestina.
Kwa sababu ya hili, matumizi yake yameongezeka.
Maasi ya 1936
Katika miaka ya 1930, Palestina ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia.
Utawala huo uliokuwa kati ya 1920 na 1948, ambao haukuwafurahisha Wapalestina, zaidi ya hayo, waliona kwamba Uingereza inaiunga mkono Israel.
Zama hizo idadi ya Waisraeli iliongezeka katika eneo laMashariki ya Kati.
Hali ambayo ilifanya uasi wa Waarabu kuendelea kwa miaka mitatu (kutoka 1936 hadi 1939) na kusababisha migogoro.
Katika migogoro hii, kilemba hiki kilikuwa na jukumu kubwa.
Kilemba hiki kina maanisha nini?
Kilemba hiki kinapatikana kwa aina tofauti na rangi tofauti. Lakini Rangi inayotumiwa sana na Wapalestina ni weusi na weupe. Ina vipengele vitatu:
- Majani ya mizeituni: Inahusishwa na mzeituni wa eneo hilo na uhusiano wake na ardhi hiyo.
- Nyekundu: inaashiria wavuvi wa Palestina na uhusiano wao na Bahari ya Mediterania.
- Ndimu nyeusi: zinaashiria njia za biashara na upendo wa jirani huko Palestina.
Katika miaka iliyofuata ya maasi hayo, kilemba kilipata umaarufu miongoni mwa Wapalestina kama ishara maalum.
Wanahistoria wanakubali kwamba inaweza pia kuhusishwa na Nakba, au "dhoruba," wakati maelfu ya Wapalestina walihamishwa au walilazimika kukimbia vita vilivyosababisha kuanzishwa kwa taifa la Israel mnamo Mei 14, 1948.
Nakba ni historia ya kusikitisha zaidi ya Wapalestina.
Lakini katika miaka ya 1960, kilemba kilikuwa maarufu ulimwenguni.
Aliyeipatia umaarufu ni Rais wa zamani wa Palestina Yasser Arafat.