Jinsi Coolio alivyobadilisha ulimwengu wa hip-hop na wimbo "Gangsta's Paradise"

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gangsta's Paradise imeuza zaidi ya nakala milioni 6.

Coolio aliposikia sauti ya wimbo uliokuja kuwa Gangsta Paradise, alikuwa na maoni sawa na sisi wengine.

"Nilihisi, 'wow, napenda sana wimbo huu.'

Rapa huyo - mzaliwa wa Pennsylvania na kukulia huko Compton, Los Angeles - alikuwa nyumbani kwa meneja wake mnamo 1995 kuchukua hundi, alipomwona mtayarishaji Doug Rasheed akijaribu kuuandaa wimbo huo kwenye chumba kingine.

"Kwa hiyo nikamwambia Doug, 'Hey! Hii ni nini?'

"Alisema, 'Ni wimbo tu tunafanyia kazi.'

"Na mara moja nikasema, 'Ni wangu.'

"Niliboresha mstari mzima wa kwanza, kisha nikaketi na kuchukua kalamu na kuanza kuandika."

Wimbo huo ulitolewa mnamo Agosti 1995 na, ukichochewa na video ya kukumbukwa iliyomshirikisha Michelle Pfieffer, uligonga vichwa vya habari.

Ukishirikisha kwa kwaya ya malaika, pamoja na hadithi ya chapa ya biashara ya Coolio, ulikifanya kibao hicho kuvuma hewani papo hapo.

Ulikuwa wimbo wa kwanza "mzito" wa Rap kuingia katika chati za Uingereza na Marekani, ukifungua njia kwa wasanii kama 2Pac na Notorious BIG, ambao, hadi wakati huo, walikuwa wamechukuliwa kuwa wabaya sana kwa muziki maarufu.

Na umaarufu wake haikupungua. Wimbo uliouzwa zaidi mwaka wa 1995 nchini Marekani, Gangsta's Paradise , una mitiririko zaidi ya bilioni 1 kwenye mitandao ya Spotify na YouTube.

"Nilifikiri itakuwa rekodi itakayoachangmsha maeneo jirani," Coolio aliiambia The Voice 2017. "Sikuwahi kufikiria kuwa ingefikia ukubwa uliofikia: umri wote, rangi, jinsia, nchi na vizazi."

Bado, Gansta Paradise ililazimika kukabili vizuizi kadhaa kabla ya kufika ilipofikia. Tunakuambia jinsi njia hiyo ya kwenda juu ilivyokuwa ...

Mvulana kutoka Compton…

 Coolio alizaliwa na kupewa jina Artis Leon Ivey, huko Pennsylvania, na kuhamia hadi Crampton akiwa kama mtoto , kitongoji maskini cha Waafirika wa kusini mwa Marekani , mjini Los Angeles. Alipokuwa akisumbuliwa na pumu ya muda mrefu, alikuwa mwandishi wa vitabu na alifaulu katika masomo yake.

"Niliishi katika maktaba hiyo," aliambia jarida la Rolling Stone wakati wa ziara ya maeneo alioshi utotoni mwaka wa 1995.

 "Nilisoma vitabu vyote vya watoto walivyokuwa navyo."

Mambo yalianza kubadilika wazazi wake walipotalikiana baada ya kufikisha miaka 11.

Akitafuta kuingiliana na ulimwengu, alianguka katika maisha ya genge na kuishia kuwa picha ya kutisha, mitaani.

Miaka michache baadaye, alikamatwa kwa kuwa na bunduki shuleni. Kabla ya kufikisha miaka 20, alikuwa ametumikia kifungo kwa wizi.

Muziki wa hip hop

Coolio baadaye alisomea katika Chuo cha Jamii cha Compton, ambapo aligundua kipaji chake cha uimbaji. Chini ya jina lake jipya la kisanii-Coolio Iglesias, akimwiga mwimbaji Julio Iglesias-alitoa nyimbo chache mtaani , lakini matumizi mabaya ya dawa za kulevya yaliharibu kazi yake.

Akiwa na umri wa miaka 20, alihamia San José ili kuishi na baba yake, huku akifanya kazi ya kuzima moto; na baadaye akausifu Ukristo kwa kumsaidia kushinda uraibu wake wa dawa za kulevya.

Albamu yake ya kwanza, It Takes a Thief, iliwasili mwaka wa 1994 na ilisifiwa kwa mchanganyiko wake wa midundo ya kufurahisha na mashairi ya kijamii.

"Walinzi" wa hip-hop hawakupendezwa na udhanifu kama huo. Msimamo wa kupinga unyanyasaji na kukubalika kwa namna fulani ulifanya ionekane "laini". Alipata jina la utani lisilohitajika "Un-Coolio".

Lakini ukaja wimbo wa Gangsta Paradise .

Muziki mzuri

Siku moja, Doug Rasheed alitoa nakala yake ya albamu mbili za Stevie Wonder za mwaka wa 1976, Songs In The Key Of Life na kuchukua sampuli ya wimbo wa Pastime Paradise, wimbo wa huzuni, ambao ulikuwa mojawapo ya nyimbo za kwanza kuchukua nafasi ya okestra.

Rasheed aliongeza mdundo mkali na bezi ya kutisha, kisha akapeleka wimbo huo kwa mwimbaji Larry "LV" Sanders, ambaye alitoa sauti ya kuongezea kibao hicho.

"Nilikuja nikiimba 'Pastime Paradise,' lakini nikabadilisha kuwa 'Gangsta's Paradise,'" aliiambia Rolling Stone kuhusu hadithi ya wimbo huo mnamo 2015

"Niliimba sehemu zangu, sauti zote, na nilifanya kwaya. Kwaya hiyo yote unayosikia ilikuwa mimi, nilifanya sauto zote, kutoka soprano, tena hadi bezi."

LV Sanders alitaka rapper aonekane kwenye wimbo huo na akampa rafiki yake Prodeje, ambaye alikataa. Kisha Coolio akamsikia.

Akiwa amekasirika, alianza kuandika mashairi mara moja.

Barua

.

Chanzo cha picha, MICHELLE PFIFFER

Maelezo ya picha, Michelle Pfieffer na Coolio kwenye seti ya video ya Gangsta's Paradise.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Maneno ya ufunguzi, yenye kutegemea Zaburi ya 23, yalikuja akilini papo hapo: “Ninapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti/ nayatazama maisha yangu na kugundua kwamba bado hakuna mengi,” kisha nikaketi na kushika kalamu na kuanza kuandika," aliambia kipindi cha YouTube Hot Ones mnamo 2016.

"Ilikuwa wimbo wa kumuomba Mungu’’.

Coolio alikuwa na umri wa miaka 30 wakati wimbo huo uliandikwa, lakini msimulizi ana umri wa miaka 23 na hajui kama ataweza kufikisha 24. "Alilelewa mitaani", amezama katika maisha ya uhalifu na kulipiza kisasi. Mtu akivuka, ataishia "chaki".

Lakini hadithi hiyo haitukuzi kamwe maisha ya majambazi. Msimulizi huomba kila usiku, akijua kwamba amenaswa. Katika mstari wa mwisho, anashutumu serikali kwa kumtupa.

"Wanasema lazima nijifunze, lakini hakuna mtu hapa a kunifundisha / Ikiwa hawawezi kuelewa, wanawezaje kunifikia?"

Hadithi hii ni dondoo kutoka kwa maandishi ambayo unaweza kuyapata kwa Kiingereza, kwa ukamilifu, hapa.