Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Anthony Joshua na Tyson Fury rasmi kuzichapa mwezi Disemba
Anthony Joshua amekubali masharti ya bingwa wa WBC Tyson Fury kwa ajili ya pambano la uzito wa juu linalowakutanisha waingereza litakalopigwa Disemba 3 mwaka huu.
Kampuni inayomsimamia bondia huyo, 258MGT inasema kwa sasa "anasubiri majibu", rasmi.
Joshua, 32, alipewa ofa na Team Fury, ambaye alipendekeza pambao liwe tarehe 3, disemba na mgao wa asilimia 60-40, bingwa Fury akipata asilimia 60.
Makubaliano ya Pambano yalifikiwa siku ya Ijumaa lakini tangazo lilicheleweshwa kutolewa kwa sababu ya kifo cha Malkia Alhamisi iliyopita.
Masharti ya awali yamekubaliwa lakini Joshua bado hajasaini mkataba. Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa Twitter ilisema: "258 na Matchroom Boxing wanaweza kuthibitisha, kwa niaba ya Anthony Joshua, kwamba tumekubaliana na masharti yote yaliyowasilishwa kwetu na timu ya Fury kwa ajili ya pambano hilo."
Fury, 34, alisema angestaafu baada ya kumpiga Dillian Whyte mwezi wa Aprili, na akarudia madai hayo mwezi uliopita, kabla ya kumpa 'challenji' bingwa wa zamani wa dunia Joshua kupitia video iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii.
Joshua alipigwa na Oleksandr Usyk wa Ukraine katika mechi yao ya marudiano nchini Saudi Arabia mwezi uliopita, kikiwa ni kipigo chake cha tatu katika mapambano yake matano iliyopita.
Kuna kipengele cha mechi ya marudiano chenye mgawanyiko wa mapato ya nusu kwa nusu (50-50) ikiwa Joshua atamchapa Fury, lakini uukumbi utakaochapiwa pambano hilo la Desemba, bado haujathibitishwa.
Uwanja wa timu ya Cardiff, Principality Stadium unapigiwa chapuo, huku Saudi Arabia au nchi nyingine ya Mashariki ya Kati pia inaweza kuwa mwenyeji wa pambano hilo.