Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Shahed: Nini kinafichwa ndani ya ndege hizi zisizo na rubani za Iran?
Tangu msimu wa vuli wa mwaka jana, sababu mpya nzito imeonekana katika vita vya Urusi na Ukriane - ndege zisizo na rubani za Shahed za Irani. Urusi inatumia ndege hizi kushambulia miundombinu ya kiraia na kijeshi ndani ya Ukraine.
Tehran haikukubali kwa muda mrefu kwamba ilikuwa ikisambaza ndege hizi aina ya UAV kwa Urusi, na Kremlin, kwa upande wake, ilisema hilo lilikuwa linahusu Urusi pekee.
Walakini, mnamo Novemba 2022, Waziri wa Mambo ya nje wa Irani Hussein Amir Abdollahian alikiri kwamba nchi yake ilikuwa imesambaza ndege zisizo na rubani za Kamikaze kwenda Urusi. Lakini, kulingana na yeye, hii ilitokea miezi michache kabla ya kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine.
Hatahivyo, kwa mujibu wa mamlaka nchini Ukraine, Urusi inaendelea kununua UAV za Irani na tayari imepokea zaidi ya Shahed 1,500. Kufikia katikati ya Januari mwaka huu, ulinzi wa anga wa Ukraine uliripoti kusambaratisha takriban ndege za aina hii 500.
Ikiwa majaribio ya kwanza ya kutumia "Shahed" katika msimu wa joto wa mwaka 2022 yalifanikiwa kabisa, lakini hivi karibuni Ukraine inadai baada ya mashambulizi kwamba imezitungua karibu UAV zote.
Ndege isiyo na rubani ya Irani iliweza kupata umaarufu ulimwenguni kama kifaa chenye ufanisi. Tehran inatangaza kwa uwazi kwamba wanajivunia silaha hizi. Ni nini siri ya Shaheeds, na je, Ukraine inaweza kutengeneza zake za aina hii ya UAV?
Mara nyingi, wanajeshi wa Urusi hutumia ndege zisizo na rubani za Shahed-136 dhidi ya Ukraine, ambayo nchini Urusi inaitwa Geran-2. Uzinduzi wa Shahed-131 ndogo na Zenye nguvu zaidi (au Geran-1) pia Ulirekodiwa. Aidha jeshi la wana anga la Ukraine liliripoti kuwa waliidungua ndege isiyo na rubani ya Mohajer ya Iran.
Faida muhimu za "shaheeds" ni uwezo wa kusafiri umbali mrefu kwa uhuru na kwa usahihi na kushambulia lengo lililokusudiwa. Kifaa hiki ni kidogo sana kwa ukubwa - kina urefu wa mita 3.5 na uzito hadi kilo 200 - na kinaweza kuruka kwa umbali wa karibu kilomita elfu 2.
Lakini injini ya pistoni ya UAV inafanya kazi kwa kutoa sauti kubwa, ambayo tayari imepokea jina la utani la kudharau "moped" kutoka miongoni mwa waukraine.
Mara ya kwanza "Shahed" ilitumiwa nyuma huko Ukraine katikati ya Septemba mwaka jana. Tangu wakati huo, ndege hizo mara kwa mara kushambuliwa miundo mbinu katika miji mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Kyiv.
Wakati huo huo, wachambuzi kadhaa na vyombo vya habari waligundua kuwa Shaheda haiwezi kuitwa kwa 100% kwamba ni bidhaa ya Irani. Idadi kubwa ya vipuri vinavyotengeneza vifaa hivyo huagizwa kutoka nje.
Wanahabari kutoka kituo cha runinga cha Amerika CNN waligundua kuwa kati ya sehemu 52 za Shaheda-136, sehemu 40 zimetolewa na kampuni 13 tofauti za Marekani. Meneo mengine 12 ni vifaa vilivyotengenezwa na kuingizwa kutoka Canada, Sweden, Japan, Taiwan na Uchina.
Kwa mujibu wa Shirika la Uingereza la Utafiti wa Silaha za Migogoro, ambalo lilitathmini ndege zisizo na rubani za Iran zilizodunguliwa nchini Ukraine, 82% ya vifaa vyote vinavyounda ndege hizo vimetotolewa na makampuni yaliyoko Marekani.
Wakati huo huo, waandishi wa uchapishaji hawakupata ushahidi wowote kwamba makampuni yoyote ya viwanda yanakiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kwa makusudi kusafirisha sehemu za ndege za kivita za Iran.
Je, Shahed zinafanyaje kazi gani?
Mtaalam wa masuala ya mawasiliano ya Jeshi Sergey Beskrestnov, anabainisha kuwa drone ama ndege hizi zisizo na rubani za Shahed ni rahisi kuziunda, lakini vifaa vyake vya elektroniki vimefanywa vizuri sana, ingawa inaweza kuonekana kuwa za zamani.
Beskrestnov huzingatia ukweli kwamba Shahed ina mfumo wa processor wenye nguvu wa kudhibiti ndege. Zaidi ya hayo, baadhi ya vifaa vyake (relays na vifungo vya bodi) vinatengenezwa katika viwanda vya kijeshi vya Kirusi.
Walakini, Sergei anabainisha, sasa ni ngumu kusema ni kiasi gani Urusi ilihusika katika utengenezaji wa ndege hzi aina ya UAV.
"Ni vigumu kusema hapa kwamba sehemu ya vifaa vilizalishwa kabisa nchini Urusi, au Urusi ilipeleka teknolojia na vifaa vya kuunda ndege hizi nchini Iran kwa ajili ya uzalishaji wake," alielezea katika mahojiano na BBC.
Ndege isiyo na rubani zinafuata njia kamili za ndege kulingana na mfumo wa kuongoza ndege wa setelaiti.
Lakini wanajeshi wa Ukraini hawawezi kubana mawimbi ya satelaiti ya GPS au kubadilisha chagizo zake, mtaalamu wa vita vya kielektroniki adokeza.
Beskrestnov anaeleza kuwa jambo la msingi ni kutumia teknolojia ya CRPA (Antena zinazodhibitiwa za Mapokezi - mfumo wa kuunganisha ishara): "CRPA, kwa kusema kwa mfano, ni mfumo wa antena 4.
Inakata uingiliaji wote unaotoka chini kutoka kwa vita vyetu vya kielektroniki.
Kwa mfano, unaweza kurusha ndege, drones au probes za EW ambazo zitaingilia kati mawasiliano ya satelaiti kutoka juu, lakini sio kutoka chini.
Injini ya Shaheda, kwa mujibu wa Sergei Beskrestnov, ni kifaa chenye gharama kubwa zaidi kwenye ndege hizo.
"Sio ngumu, lakini inapaswa kutegemewa kwa kuruka kwa masafa marefu," anasema.
Injini za UAV hii ni nakala ya mfano wa mafanikio wa Ujerumani, inazalishwa katika viwanda vya Iran na China. Tabia yake muhimu zaidi ni uzito wake mdogo licha ya kuwa na nguvu.
Kasoro yake ni kwamba zina kelele kubwa, sawa na sauti ya moped. Jeshi la Kiukreni linatumia vifaa maalumu kama rada za acoustic, pamoja na rada za redio na kutambua Shaheeds.
Je, Ukraine inaweza kuzalisha ndege zake za Shaheed?
Je, Ukraine inaweza kuzalisha ndege zake za Shaheda, drone za gharama nafuu, lakini yenye ufanisi na rahisi? Beskrestnov hana shaka juu ya hili. Shida pekee ni wapi kupata vifaa vya elektroniki kwa ajili ya kuziunda.
"Ukraine ina wataalamu na uwezo wote muhimu kwa ajili ya utengenezaji wa ndege hizo zisizo na rubani. Utata utakuwa tu katika vifaa vya elektroniki.
Injini, na bodi, vyote vinawezekana, lakini kuunda mfumo wetu wa CRPA sio rahisi, lakini tunaweza kununua uliotengenezwa katika nchi nyingine ", anasema mtaalam.